TANZIA: Kapteni Keenan Mhaiki, amefariki dunia

jsenyinah

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
249
500
OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki, amefariki dunia jana saa 5:25 asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Alilazwa katika hospitali hiyo Alhamisi iliyopita, kabla ya sikukuu ya Krismasi, kwa ugonjwa wa saratani ya ini.

Kaka mkubwa wa marehemu, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sheria, Oliver Mhaiki alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na HabariLeo.

Mhaiki alisema Kapteni Keenan ambaye ameendesha marais wa awamu zote tano, alianza kuumwa Julai mwaka huu kwa kusumbuliwa na pingili ya ‘lumber’, hali iliyoelezwa na madaktari ni kwa sababu ya kukaa muda mrefu.

Alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na maumivu na Oktoba mwaka jana alipokwenda India kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ndipo baadaye alirudi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

“Kilichomuua sio hicho, inaonekana alikuwa na saratani ya ini muda mrefu, hakuigundua, hivyo wiki mbili zilizopita alibadilika rangi kuwa njano, alipoenda hospitali wakagundua ni saratani,” alisema kaka huyo wa marehemu.

Alisema marehemu ameacha mke na watoto wawili na kwamba anatarajiwa kuzikwa Songea. Alisema hivi sasa wanasubiri wadogo wa marehemu waliopo nje ya nchi.

Alisema katika familia yao, wamezaliwa watoto nane.

Chanzo: Habari leo
 
Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
8,731
2,000
Bosi Ndege za Serikali afariki

Chanzo: Habari Leo
 
Jics

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
235
500
naomba Mungu wa milele awape faraja wafiwa kwenye kipindi hiki kigumu
na raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umwangazie roho ya marehemu ipumzike kwa amani Amina.
 
BlessedHope

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,970
2,000
R.I.P Kapten Keenan Mhaiki..pole ndugu jamaa na marafiki mke na watoto wa marehemu Mungu awatie nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba
 
bibiinna

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
652
500
Familia yake ninaipa pole kwa msiba huu mkubwa.Nawatakia uvumilivu na subra pamoja na afya ya kuweza kuhimili huu msiba.
Sasa aliwaendesha maraisi watano au aliwarusha
 
comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,315
2,000

OFISA Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki, amefariki dunia jana saa 5:25 asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam.

Alilazwa katika hospitali hiyo Alhamisi iliyopita, kabla ya sikukuu ya Krismasi, kwa ugonjwa wa saratani ya ini.

Kaka mkubwa wa marehemu, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Sheria, Oliver Mhaiki alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na HabariLeo.

Mhaiki alisema Kapteni Keenan ambaye ameendesha marais wa awamu zote tano, alianza kuumwa Julai mwaka huu kwa kusumbuliwa na pingili ya ‘lumber’, hali iliyoelezwa na madaktari ni kwa sababu ya kukaa muda mrefu.

Alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na maumivu na Oktoba mwaka jana alipokwenda India kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ndipo baadaye alirudi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

“Kilichomuua sio hicho, inaonekana alikuwa na saratani ya ini muda mrefu, hakuigundua, hivyo wiki mbili zilizopita alibadilika rangi kuwa njano, alipoenda hospitali wakagundua ni saratani,” alisema kaka huyo wa marehemu.

Alisema marehemu ameacha mke na watoto wawili na kwamba anatarajiwa kuzikwa Songea. Alisema hivi sasa wanasubiri wadogo wa marehemu waliopo nje ya nchi.

Alisema katika familia yao, wamezaliwa watoto nane.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom