Mwanagandila
Senior Member
- Oct 9, 2011
- 182
- 100
Yule askari maarufu wa jeshi la polisi jijini Dar es salaam kwa kuongoza magari/kuelekeza njia za kupita kukiwa na foleni Sajenti Ally Kinyogori amefariki usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Mwandege nje kidogo ya jiji la Dar.
Kinyogori alijizolea umaarufu katika kipindi cha redio One kila siku asubuhi alipokua akitoa taarifa za hali za barabarani zikiwemo njia zenye foleni kwa wakazi wa jijini.
Marehemu ameuwawa na watu wasiojulikana kwa risasi baada ya kwenda nyumbani kwake Mwandege wakiwa na pikipiki, na baada ya kumpiga risasi wakatokomea bila ya kuchukua chochote.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen.

Watu wasiojulikana wakiwa na pikipiki aina ya Boxer, usiku wakuamkia leo wamemuuwa kwa kumpiga risasi kadhaa katika sehemu mbalimbali za mwili wake Askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani, Ally Kinyogoli nyumbani kwake Mwandege, Mkuranga mkoani Pwani.
Watu hao wawili wasiofahamika walienda nyumbani kwa askari huyo mwenye No. 1839 Sajenti Ally Kiwagoli kwa pikipiki aina ya Boxer na kumtoa ndani kwake na kumpiga risasi tumboni na kichwani na kupoteza maisha.
Watu hao hawakuchukua chochote nyumbani kwake kwa hiyo ni kifo ambacho kina pazia nyuma, sikiliza mahojianao zaidi hapa