TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

Pasco...I know you know something, hebu tuwekee "chochote" hapa kuhusiana na shujaa huyu.
Especially kuhusu kile kikao cha Dodoma kilichomuengua Mzee wetu!
Gwama, issue ya huyu Mzee ni ndogo tuu, baada ya kuona Zanzibar inabanwa, akautumia Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mgoa Wolfgang Dourado kuandaa hati za kisheria za serikali tatu, ziende BMW, Zanzibar iwe na mamlaka yake kamili. Wakamshirikisha Maalim Seif wakati huo kijana kada maarufu wa CCM, toka UV-CCM. Seif akapanda boat usiku usiku na kuzikabidhi hizo documents kwa Mwalimu, Mwalimu akaitisha kikao cha NEC cha dharura Dodoma, kwenye kikao Jumbe akaenda kama rais wa Zanzibar, akaonyeshwa document, kimya, akavuliwa nyadhifa zote na kurejea kama mfungwa, akutupwa kizuizini cha nyumbani kwake mpaka umauti ulipomkuta. Dourado yeye aliozea jela kwa muda mrefu, kisha akaachiliwa na kujifia!.

Tangu pale alikuwa kifungoni cha nyumbani kwake mpaka Mungu alipomuita. Hata hivyo, wakati wa kifungo hicho, serikali iliendelea kumhudumia kwa kumpatia stahiki zake zote kama rais mstaafu wa Zanzibar!.

Huyu Maalim Seif wa leo ambaye ni mpinzani Mkuu wa CCM Zanzibar, alikuwa ni CCM, and was once a snitch! . Once a snitch, always a snitch!, naye siku zake zinahesabika, what goes around, comes around! .

RIP Alhaj Aboud Jumbe, wengine soon watafuatia na wote mtakutana huko mbinguni na mtayamaliza kiutu uzima hukohuko mliko! .

Pasco
 
Farewell Sheikh Aboud Jumbe mmungu akulaze mahala pema peponi, sisi ni wa mmungu na kwake tutarudi
 
Innalillah nasikia alizuiliwa kutoka nje ya maeneo yanyumbani kwake tokea enzi za nyerere mpaka alipopata naumauti hio ndio nguvu ya chama chenye mapinduzi
 
Nadhani kunajambo alisahau yakuwa alikuwa kiongoz na aliapa kuzikubali sheria na katiba huku akiwa ameshika Quran sasa nilazima ajuwe atazikwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi zakuwazika viongozi. RIP mzee

TumainiE! Nadhani Na Wewe umesahau Kwamba Alhaji Abdul Jumbe Mwenye Ez Mungu amrehemu alivuliwa uongozi Na kwa mujibu wa katiba Na sheria za nchi hawezi kuzikwa Kama kiongozi.
 
Hivi baada ya kujivua/kuvuliwa nyadhifa zake zote za uongozi, je, aliendelea kupata stahiki zake kama kiongozi wa hadhi yake?

Je, alikuwa akifanya shughuli gani ya kujikimu kimaisha tangu 1984?

Askari/walinzi waliokuwa wakilinda nyumbani kwake mji mwema walikuwa wakifanya shughuli hiyo kama ulinzi wa kiongozi mstaafu au mtu aliyewekwa kizuizini?

Je, mitaala ya somo la historia na uraia ya Tanzania inafundisha kuhusu Aboud Jumbe? Kama jibu ni 'ndio', anatajwa kama nani na kiwango gani/mipaka ipi? Kama jibu ni 'hapana', kwa nini?

Natumai wajuvi mtatuelewesha kwa kutujibia naswali haya.

Kaka ...
 
Wewe ulikaaa mlangoni kuona kama wanakwenda au hawaendi
Sasa wewe unataka kuleta kongamano au?,inajulikana kisiasa marehemu Jumbe alitengwa,na hii yote ilisababishwa na mchawi mmoja ambae sasa hivi anatumikia marungu ya moto kule kaburini kwake,na viongozi uchwara kwa kulinda matumbo yao na kujipendekeza kwa mabwana zao nao wakaogopa hata kumjulia hali yule mzee,mambo yako wazi na hakuna siri duniani hapa,kama wewe hujui basi kaa kimya sio kurukia watu na kuwauliza maswali ya kishoga.
 
Sidhani mkuu...alikuwa mkweli kivitendo na kinafsi...!
....msomi "aliesoma" kwa kujifunza...!
....ukitaka kujua pia somo la "mambo ya kikulacho", na yote yenye kuambatana na dhulma ya usaliti ktk siasa, fuatilia maisha ya kisiasa ya waliomsaliti, al marhum, Aboud Jumbe Mwinyi!
...yeye alijiamulia kuishi maisha yake ya kawaida, nje na mbali na siasa zetu za kitanzania!
...Allah, amjaalie rehma, toba, na maghurfilla...
AAAAAMEEEEN BRO INSHALLAH.
 

image-jpeg.381456

SHEIKH ABOUD JUMBE MWINYI

1972 -1984

Amezaliwa 1972

Amefariki 1984!
 
Back
Top Bottom