TANZIA: Aliyekuwa RC Ruvuma, Said Mwambungu afariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu amefariki dunia katika hospitali ya Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya figo.

Mwenyezi Mungu amlaze Mahala Pema,Amina.

Mwambungu.jpeg

4a.1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha na kumkabidhi vitendea kazi Ndg. Said Said Thabit Mwambungu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es salaam Marchi 15,2016.

Alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Thabit Mwambungu alihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako Rais Magufuli alisema atapangiwa majukumu mengine. Nafasi yake ilijazwa na Dkt. Binilith Satano Mahenge.​

Akizungumzia kifo cha Mwambungu, Nkinda alisema amefariki dunia akiwa JKCI alikokuwa amelazwa kwa matibabu dhidi ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.

“Mwambungu aliletwa JKCI Mei 10, mwaka huu akitokea Emergence (Idara ya Magonjwa ya Dharura), alipelekwa wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu kwa matibabu, ambako alifariki dunia,” alisema Nkinda.

Itakumbukwa kuwa Mwambungu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma tangu mwaka 2011, enzi za utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na hata Rais Dk. John Magufuli alipoingia madarakani aliendelea naye.

Marehemu Mwambungu aliondolewa katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais Magufuli Juni, 2016 na kurudishwa kuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Dar es Salaam, ili kupangiwa kazi nyingine.
 
"We are dust and in dust we return"
May the soul of our lovely Father rest in enternal peace...

Mungu awape nguvu wafiwa wote katik kipindi hiki kigumu...
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Poleni Wafiwa.Chachu umefanya vizuri sana kuweka picha.Jina nilikuwa nalikumbuka sura ilishapotea.Apumzike kwa amani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom