Tanzania yetu na TTCL

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
TGIF-Katika vita ya utashi na maarifa ,anayeshindwa ni yule mwenye uwezo mdogo wa maarifa na utashi na mshindi ni yule mwenye hazina ya maarifa na mbinu za ushindani.

Naitizama Tanzania yangu na mambo yote yanayoendelea kwa sasa na kuona mambo kwa jicho la tatu.Vodacom,Tigo na Airtell ndio wanaonufaika kwa kila jambo ambalo linatokea kwa sasa .

TTCL bado wanashangaa kwa kila jambo,jaribu kutafakari kama watu 3,000,000 wakanunua kifurushi cha MB cha Tsh 1000/- kwa siku moja kwa mwezi wataingiza Tsh ngapi?

Kabla ya kuanza kujenga viwanda yatakiwa tuanze kuboresha Company ya TTCL kuwa mshidani na company zingine za simu kama Tigo,Vodacom na airtell.Always forgive your enemies but never forget their names.
 
Mkuu hii TTCL kutoboa kazi sana. Mfano kwa Mwanza wameweka 3G tu, hamna 2G wakati watuamiaji wa smartphones ni wachache ukilinganisha na feauture phones.
Nilipata kumdadisi moja ya mfanyakazi (boss) aliniambia, 2G itaacha kutumika Tz.

Swali ninalojiuliza je, ni muda muafaka kwetu kufanya hivyo?!
 
Soon watakuwa wapo juu! Tuwape Muda Kidogo.DATANG shilika la Simu la Serikali ya China kama TTCL hapa kwetu.Wapo Mbioni kuwapatia 4.5 G network Nchi nzima mpaka Vijijini .muda si mrefu. Na Pia DATANG watawafungia TTCL 5 G network mara tu hii teknolojia itakapopata green light toka UTI
Prosperous TTCL coming
2212a958f20d5ae465e855fd38d5957d.jpg
 
Watanzania wanependa vitu vyao sana ila viongozi wa serikali wanashindwa kuona hili swala. Ukitaka kuamini soma pages za TTCL za Facebook, au Instagram watu wanaulizia sana kama huduma imefika kwenye maeneo yao. Yaani roho inauma sana kuona kuona jinsi kampuni kama halotel wamekuja juzi tu hapa lakni wanawateja 2 million, Walijipanga kwelikweli walitangaza kama cheap network na mtandao uliosambaa zaidi vijijini wananchi walisaidia sana kuipa promo hii kampuni. TTCL kuna vijana wazuri sana wazalendo ambao ni wazuri sana w kwenye marketing naamini wapo tayari kujitolea kwa ajili ya nchii yao . Leo hii malamiko ya wateja wa TTCL ikiwemo na mimi upatikanaji wa vocha kwa urahisi, mtandao kutokuwa wa uhakika maeneo kama bunju mbweni bagamoyo kuna network inakuwa chenga. Kusambaa mikoani na vijijini. Wajipange sana tuone siku moja vodacom(T) inakuwa subsidiary kampuni ya TTCL na tunatoka na kwenda kuwekeza nje ya nchi.
 
Kale katangazo Kao ka T generation sijui kamepotelea wapi? Mimi naipenda Sana hii campun na nakumbuka kunakipindi nilikua moshi nikaenda HQ zao kuulizia line nikaambiwa hamna daah niliumia sanaaa
 
Aiseee TTCL ni nomaaaa Jana nmeijaribu, sikutegemea pale ilipodownload game la asphalt 8 (2GB) kwa dk.10
 
Watanzania wanependa vitu vyao sana ila viongozi wa serikali wanashindwa kuona hili swala. Ukitaka kuamini soma pages za TTCL za Facebook, au Instagram watu wanaulizia sana kama huduma imefika kwenye maeneo yao. Yaani roho inauma sana kuona kuona jinsi kampuni kama halotel wamekuja juzi tu hapa lakni wanawateja 2 million, Walijipanga kwelikweli walitangaza kama cheap network na mtandao uliosambaa zaidi vijijini wananchi walisaidia sana kuipa promo hii kampuni. TTCL kuna vijana wazuri sana wazalendo ambao ni wazuri sana w kwenye marketing naamini wapo tayari kujitolea kwa ajili ya nchii yao . Leo hii malamiko ya wateja wa TTCL ikiwemo na mimi upatikanaji wa vocha kwa urahisi, mtandao kutokuwa wa uhakika maeneo kama bunju mbweni bagamoyo kuna network inakuwa chenga. Kusambaa mikoani na vijijini. Wajipange sana tuone siku moja vodacom(T) inakuwa subsidiary kampuni ya TTCL na tunatoka na kwenda kuwekeza nje ya nchi.
Mkuu vocha si utumie M-PESA naona ndo njia rahisi na ya haraka
 
Kwanini tututmie platform ya kampuni nyingine? Kina washinda nini kuweka yao? Kumbuka hii ni kampuni kongwe kuliko zote za mawasiliano hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom