Tanzania yenye AMANI na UPENDO!

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Ujumbe wa matumaini kwa baadae yetu. Kizazi chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi sana kama Taifa. Tumerithi taifa ambalo
limegawanyika na lisilokuwa na malengo ya pamoja wala maono. Kiwango cha uzalendo wa watu wetu kimeshuka mno katika hali
ya kuogopesha na kunifanya nijiulize ni wapi tunaelekea. Taifa hili linahitaji uongozi na dira. Linahitaji atayeleta upya uzalendo na kuamsha roho ya kulitumikia Taifa hili kwa watu wote.

Watu wa Taifa hili lazima wahisi utaifa wao ndani ya roho zao na wawe tayari kulitumikia. Sisi ni watu wamoja. Majaliwa yetu ni mamoja kama Taifa. Naamini kama tukiji organize kwa pamoja kukabiliana na matatizo yanayotukabili kama Taifa bila ya ubinfasi tutafika. Ni lazima tujue ni wapi tunataka kwenda kama Taifa. Ni nini azma yetu na malengo yetu. Taifa hili halijazaliwa kusudi liwe
ombaomba, tuna nafasi ya kukua kama tukilipenda na kulitumikia Taifa hili.

Tunapozungumzia mabadiliko ni pamoja na kulipenda Taifa hili, kupenda Raia wenzako kwa moyo wote na kuwa Tayari kuwatumikia. Ukweli ni kwamba hatujawa Taifa kusudi tunyonyane au kundi moja likandamize kundi jingine. Tumekuwa Taifa ili tufikie kilelele
fulani cha mafanikio na ndio hasa itakayo kuwa sababu ya furaha yetu kama Taifa. Mafanikio yetu ya pamoja iwe ndio furaha yetu. Lazima tukumbuke tunawajibu kwa vizazi vijavyo, ni sisi tunaotengeneza baadae ya vizazi vyetu. Lazima tuvipende vizazi vyetu ambavyo havijazaliwa kwa kuwatengenezea mazingira bora kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kupendana kama raia wa Taifa hili.

Tumaini hili lazima lizame katika mioyo yetu. Lazima tujue tunapotaka kwetu kama Taifa. Ukweli ni kwamba , hatutaweza kulijenga Taifa hili pasipo kulipenda kwanza. Ni lazima tulipende kwanza ndipo tutakapo litumikia kwa mioyo yetu yote. Tujenge Taifa ambalo
Raia wanaheshimiana kwa dhati na kushirikiana katika ujenzi wa Taifa lao na viongozi wakitenda Haki na kuwajibika. Hili ndilo
Taifa ninalo lihitaji . Ambalo wanawake na wanaume wanashirikiana na kuheshiamiana katika ujenzi wa Taifa lao, ambalo wazazi wanawajibika kwa pamoja katika malezi ya watoto.

Hatujawa Taifa kusudi kila mmoja ajiangalie mwenyewe, tunawajibu kwa kila mmoja wetu.. Tunachohitaji ni Taifa hili kusonga mbele kwa nguvu ya umoja wetu. Sisi ni Watanzania na nilazima tuungane pamoja ili tupambane na matatizo yanayotukabili sasa hivi, ili
tupambane na uovu unaolikabili Taifa hili. Tuna changamoto za rushwa, uzembe na kutokuwajibika kwa watu waliopewa dhamana.
Wakati wa kutawalaiwa kama waafrika na kama watu weusi ni lazima uishe, kwa kuamua sasa na kwa dhati kuwa wamoja na kutia juhudi katika kujikomboa. Nina amini kwa dhati kabisa tunauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama mataifa mengine. Ni jitihada zetu na kujitolea kwetu na dhamira yetu isiyofifia ya kuleta mabadiliko. Ya kuona maisha ya mwafrika na mtanzania yakibadilika.

Natumaini siku moja kuona WANAUME KWA WANAWAKE WAKIJITOLEA KWA DHATI KULITUMIKIA TAIFA HILI. Mabadiliko haya lazima yaje na yaonekane. Kwa juhudi za pamoja ni lazima tutashinda kama tumedhamiria kwa pamoja kukusanya nguvu zetu na uwezo
wetu wa kiakili. Watanzania tuna uwezo wa kuwa Taifa kubwa. Nafikiri tofauti kuhusu Taifa hili. Naliona katika macho ya uwezekano. Taifa hili linauwezo wa kuwa kitu chochote linachotaka ni juhudi zetu na umoja wetu na jitihada zetu zisi zisizofifia. Katika kizazi chetu leo hii tuna viongozi wanaogawa watu na kuondoa umoja wetu ambao ni nguvu yetu ya kuleta maendeleo.

Uchu na ubinafsi umetamalaki. Wajibu wetu wa dhati kwa kila mmoja wetu ni kuliona Taifa hili likisonga mbele ni kuona Taifa hili likisonga mbele na kuliletea heshima yake.. Vijana wa Taifa hili ambao tunaishi sasa tunawajibu huu, majaliwa ya taifa hili anatutegemea sisi ni lazima tuwe Taifa lenye malengo. Ni lazima tuwe taifa lenye ushawishi na nguvu. Ni lazima vijana tujikusanye tufanye mapinduzi haya kwa faida ya Taifa na heshima yetu na vizazi vyetu vingi vijavyo.. Hili ni lazima tulidhamirie. We must have a
fighting spirit. The spirit of those who conquer and not conquered. Ili tuwahadidhie watoto wetu jitihada zetu na mafanikio yetu tuliyo
 
Dhulma imekithiri mno na ndio sababu kubwa ya matokeo haya.Na kuweka sawa inakuwa na gharama kubwa sana kwasababu hakuna atakae kubali kosa lake.Ni sawa na maji masafi yamwagike na kuyazoa inakuwa ngumu kupata yaliyo masafi.Ubinafsi unasababisha wengine kuwa masikini huku wengine wanalia shida.Na badala yake vijidudu vya chuki vinazaliwa na kuangamiza kizazi chetu.
 
Napiga Goti kuwaomba watanzania wote kwa siku ya leo wasimame imara kila mmoja wetu kwa Imani yake na wale wasio na Imani.

Tuepuke mijadara ya kidini na ile inayochochea uhasama, tutumie silaha yetu moja ya Upendo.


Nakuomba wewe unayesoma uzi huu, Kujifanya Mjinga siku ikapita kwa maslahi ya Amani yetu. Tuwe wavumilivu. Tusichoke kuvumiliana mapungufu tuliyo nayo. Tukumbuke kila jambo lina faida na hasara.

Heri Uwe falla mwenye raha kuliko Shupavu mwenye taabu.
 
Taifa letu ni kama familia au ukoo, wenye baba, mama, watoto na jamaa wengine. Familia hii na ukoo huu, hukaa pamoja katika raha na huzuni. Hufurahia mafanikio ya familia na huhuzunika pamoja pale familia inapopata shida au tatizo. Aghalabu, vi vigumu kuona mwanafamilia mmoja, tuseme baba au mjomba kutaka kujipatia faida pekee yake ili hali wanafamilia wengine wakipata shida na njaa.

Hii ndio familia kwa maoni yangu ilikuwa hivyo nyakati za utawala wa awamu ya kwanza.
 
Back
Top Bottom