chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,961
Impact yake ni short term ama otherwise? Kujitenga ni nia mojawapo, je utayari wa kujitosheleza kila nyanja pasipo wenzetu tunao? Ama ndo sasa tuneingia China moja kwa moja?
Shida yetu kubwa Tanzania ni kukosa msimamo.
Tunapeleka wawakilishi wetu kwenye meza za majadiliano in these high profile platforms ambapo wakifika huko wanashiriki mijadala na hatimaye kuunga mkono makubaliano. Cha kushangaza ni kwamba baadae tunayageuka makubaliano hayo au tunakuwa na kigugumizi cha utekelezaji.
Hii ni aibu kwa taifa. Au tunapeleka wawakilishi ****** ambao wana-counter sign vitu wasivyojua???? Tunachekwa. Kwa wale tunaozunguuka zunguuka huko kwa wenzetu wanaelewa ninachoongea.
Kama nchi inabidi tuwe tuna tuma representatives ambao ni competent (sio kwa mjuano). Of course maslahi ya nchi yetu should be our priority lakini lazima tuweke wazi misimamo yetu mapema kabisa.
Kujitenga!! hainiingii akilini.
Swadakta mkuu! Ndio hiki ninachosema hata mimi. Hatuna msimamo. Na ndio wenzetu wanapotuchoka. Wala hawana shida kwamba kuna vitu vingine hatukubaliani nao...shida yao ni kwamba leo tunakubali...kesho tunakataa..keshokutwa tunakubali. Sasa nchi kigeugeu namna hiyo unadeal nayo vipi?
Sawa, wasi deal na sisi, kwani lazima?nchi kigeugeu namna hiyo unadeal nayo vipi?
Sawa, wasi deal na sisi, kwani lazima?
Waendelee kivyao. Sisi hatutaki, tushaona ubaya wa kubanwa banwa kwenye ma treaty haya, tuna kongwa la Zanzibar limetunyiga koo tunashindwa kulifungua!
Hatua nzuri; ila tusifunge milango kabisa. Maana na sisi tutahitaji masoko kuuza bidhaa kwa hao tunaowafungia milango wasiingie kwetu. Isitoshe, tunahitaji ushindani na wenzetu waliondelea ili kujua namna ya kuboresha bidhaa na huduma zetu. Maana tuko nyuma kwa karibu kilakitu. Tumeishia kujisifia milima, wanyama, madini etc. Lakini vyote hivi vitahitaji ushirikiano na nchi nyingine, kwa namna moja au nyingine, kuleta maendeleo na kupunguza umaskini kwa Watanzania walio wengi. Kwa wingi wetu, na kwakuwa wengi wetu ni maskini, hatuwezi kuzalisha na kutumia wenyewe kwa kiwango cha kutuletea maendeleo bila "economic partnership".