Tanzania yatangaza kujitenga na Afrika Mashariki na Ulaya ili kuleta viwanda

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,959

Tanzania haitaweza kusaini mkataba wa EPA (economic partnership agreement) baina ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na jumuiya ya ulaya (EU) kwa kuwa utafungua fursa nyingi za kiuchumi na hivyo kugeuza Tanzania kuwa soko la bidhaa badala ya nchi ya viwanda
sababu nyingine pia ni kutokana na Uingereza kujitoa EU ambayo imeleta sintofahamu kubwa
 
Tanzex(from EPA)
Haya mambo yapo tangu 2002. Kuna haja ya kuwa na competent negotiation team. Ambayo inauwezo wa kuchunguza na kuangalia kwa undani faida na hasara kwa taifa na kwa wakati. Haya madeal ya kimataifa sio kitu kidogo.

Hapa suala sio Tanzania kuwa kigeugeu. Tukumbuke Serikali iliyopo inamipango tofauti wenda mingi itaathiliwa na makubaliano haya. Mipango hii imeanza kuwa ctive kuanzia mwezi huu.

Tunaelekea Tanzania ya Viwanda(kwa Mujibu wa wanasiasa). Na utafiti uliofanywa NIGERIA EPA ni sumu itakayoua na kudhoofisha viwanda, maana unaingia mktaba wa KUingiza vitu kutoka ulaya, Pili unaviondolea tarrif(Serikali hii inadiscourage importation kwa kuongeza tarif). Hapa tutakuwa tunajichanganya tukiingia kichwa kichwa.
Madhara ya awali na ya haraka ya EPA ni DE-INDUSTRIALIZATION kwa Tanzania, Pili itapelekea UPOTEVU WA MAPATO ya serikali kwa kiwango kikubwa.

Naunga mkono serikali hii mpya kutafakari sana na kuangalia je, hii EPA inacomply vipi na our local Developmental plan na Industrial revolution inayojadiliwa kila siku?

KUNA CHA KUJIFUNZA PIA KUTOKEA HAPA
1:Industrial Revolution: Why EPA Will Undermine Nigeria
2:http://www.actionaid.org/sites/file...plications_for_socio-economic_development.pdf
 
Shida yetu kubwa Tanzania ni kukosa msimamo.

Tunapeleka wawakilishi wetu kwenye meza za majadiliano in these high profile platforms ambapo wakifika huko wanashiriki mijadala na hatimaye kuunga mkono makubaliano. Cha kushangaza ni kwamba baadae tunayageuka makubaliano hayo au tunakuwa na kigugumizi cha utekelezaji.

Hii ni aibu kwa taifa. Au tunapeleka wawakilishi vilaza ambao wana-counter sign vitu wasivyojua???? Tunachekwa. Kwa wale tunaozunguuka zunguuka huko kwa wenzetu wanaelewa ninachoongea.

Kama nchi inabidi tuwe tuna tuma representatives ambao ni competent (sio kwa mjuano). Of course maslahi ya nchi yetu should be our priority lakini lazima tuweke wazi misimamo yetu mapema kabisa.
 
Impact yake ni short term ama otherwise? Kujitenga ni nia mojawapo, je utayari wa kujitosheleza kila nyanja pasipo wenzetu tunao? Ama ndo sasa tuneingia China moja kwa moja?

Impact yake kubwa ni kwamba Tanzania tunaonekana kama nchi ambayo haina maamuzi kamili. Sijui kama umefuatilia hii EPA inayoongelewa hapa. In short...negotiations za hii kitu zimefanyika kwa miaka...na sababu kubwa ya kuchukua miaka ni kwasababu Tanzania ilikua inaweka mapingamizi...kamati inakaa kutatua..mpaka Tanzania inaridhika. Iliendelea hivyo kwa muda mrefu mpaka mazungumzo yakakamilika. Na juzi juzi mawaziri walivyokutana..Tanzania iliconfirm kwamba ipo tayari kusign na wenzake. Tarehe ikachaguliwa kuwa tarehe 18 jul. Sasa leo ghafla katibu mkuu anaibuka na kusema aaaahhh....hatutasign.eti wanataka kupitia upya kujiridhisha.

Labda nieleweke vizuri...inawezekana tukawa na sababu nzuri za kusita kusign...lakini basi tuwe na kauli moja. Kama hatutaki tuseme hatutaki. Hii tabia ya ndimi mbili inatushushia sana heshima kwa wenzetu.
 
Shida yetu kubwa Tanzania ni kukosa msimamo.

Tunapeleka wawakilishi wetu kwenye meza za majadiliano in these high profile platforms ambapo wakifika huko wanashiriki mijadala na hatimaye kuunga mkono makubaliano. Cha kushangaza ni kwamba baadae tunayageuka makubaliano hayo au tunakuwa na kigugumizi cha utekelezaji.

Hii ni aibu kwa taifa. Au tunapeleka wawakilishi ****** ambao wana-counter sign vitu wasivyojua???? Tunachekwa. Kwa wale tunaozunguuka zunguuka huko kwa wenzetu wanaelewa ninachoongea.

Kama nchi inabidi tuwe tuna tuma representatives ambao ni competent (sio kwa mjuano). Of course maslahi ya nchi yetu should be our priority lakini lazima tuweke wazi misimamo yetu mapema kabisa.

Swadakta mkuu! Ndio hiki ninachosema hata mimi. Hatuna msimamo. Na ndio wenzetu wanapotuchoka. Wala hawana shida kwamba kuna vitu vingine hatukubaliani nao...shida yao ni kwamba leo tunakubali...kesho tunakataa..keshokutwa tunakubali. Sasa nchi kigeugeu namna hiyo unadeal nayo vipi?
 
Kwa mtazamo wa uda ukosawa ila kwakutumia mtazamo wa mwendokasi
1: maisha yangekua simple
2: sisi tungekua dampo kwa kawaida hamna bidhaa yenye gharama dampo.
Basi twende tu na UDA yaviwanda
 
Swadakta mkuu! Ndio hiki ninachosema hata mimi. Hatuna msimamo. Na ndio wenzetu wanapotuchoka. Wala hawana shida kwamba kuna vitu vingine hatukubaliani nao...shida yao ni kwamba leo tunakubali...kesho tunakataa..keshokutwa tunakubali. Sasa nchi kigeugeu namna hiyo unadeal nayo vipi?

Uko sahihi kabisa mkuu
 
nchi kigeugeu namna hiyo unadeal nayo vipi?
Sawa, wasi deal na sisi, kwani lazima?

Waendelee kivyao. Sisi hatutaki, tushaona ubaya wa kubanwa banwa kwenye ma treaty haya, tuna kongwa la Zanzibar limetunyiga koo tunashindwa kulifungua!

Waendee na sisi kwa yale tunayokubali, kama UK alivyokataa kuua pound yake na kuingia Schengen Visa. Wakiona tunakataa mengi au tunazingua kwenye umoja, vote us out!
 
Hatua nzuri; ila tusifunge milango kabisa. Maana na sisi tutahitaji masoko kuuza bidhaa kwa hao tunaowafungia milango wasiingie kwetu. Isitoshe, tunahitaji ushindani na wenzetu waliondelea ili kujua namna ya kuboresha bidhaa na huduma zetu. Maana tuko nyuma kwa karibu kilakitu. Tumeishia kujisifia milima, wanyama, madini etc. Lakini vyote hivi vitahitaji ushirikiano na nchi nyingine, kwa namna moja au nyingine, kuleta maendeleo na kupunguza umaskini kwa Watanzania walio wengi. Kwa wingi wetu, na kwakuwa wengi wetu ni maskini, hatuwezi kuzalisha na kutumia wenyewe kwa kiwango cha kutuletea maendeleo bila "economic partnership".
 
Sawa, wasi deal na sisi, kwani lazima?

Waendelee kivyao. Sisi hatutaki, tushaona ubaya wa kubanwa banwa kwenye ma treaty haya, tuna kongwa la Zanzibar limetunyiga koo tunashindwa kulifungua!

Ewaaahh...kama ndio matakwa yetu kama nchi..basi tukae pembeni tuwaache wenzetu waendelee. Tatizo letu tumengangania kubaki kwenye EAC....na moja wapo ya kanuni za EAC ni kwamba mikataba kama hii EPA inayotakiwa kuingiwa na jumuiya ya ulaya, ni lazma iingie jumuiya nzima..sio nchi moja moja. Sasa hii geugeu yetu inawaathiri wanachama wengine...hususan kenya ambao wanafanya biashara kubwa sana na EU. Kwahiyo kama tunaona "tunabanwa"...basi tutoke wenzetu watuelewe hivyo.
 
Hatua nzuri; ila tusifunge milango kabisa. Maana na sisi tutahitaji masoko kuuza bidhaa kwa hao tunaowafungia milango wasiingie kwetu. Isitoshe, tunahitaji ushindani na wenzetu waliondelea ili kujua namna ya kuboresha bidhaa na huduma zetu. Maana tuko nyuma kwa karibu kilakitu. Tumeishia kujisifia milima, wanyama, madini etc. Lakini vyote hivi vitahitaji ushirikiano na nchi nyingine, kwa namna moja au nyingine, kuleta maendeleo na kupunguza umaskini kwa Watanzania walio wengi. Kwa wingi wetu, na kwakuwa wengi wetu ni maskini, hatuwezi kuzalisha na kutumia wenyewe kwa kiwango cha kutuletea maendeleo bila "economic partnership".

Na ndio hapo mimi nashindwa kumuelewa mkapa (ambaye ndio mpinzani mkuu wa hii EPA). Ukikataa kushirikiana na wenzako..hizo bidhaa utakazozalisha utaziuzia wapi? Ila watu wakuelewa hii si wengi. Ndio maana nikasema badala ya kuvunja heshma yetu kwa hii "mguu ndani mguu nje"...bora tutoke kwanza. Hivyo viwanda vikija tukianza kuwa na bidhaa nyingi na tunapata shida kuuza...wenyewe tutaufyata na kwenda kuitafuta hiyo EPA ambayo tunaikataa sasa.
 
wakuu,

nathani ni jana tu niliandika kuhusu wa waafrica kujitoa kwenye mashirikisho ambayo hayana maaana kwa waafrica Zaidi ya unyonyaji.
Ila niwakumbushe au kusema nitoe tahathari kuwa,kushirikiana na nchi nyingine ndani ya Africa ni kitu muhimu sana.
siamini kuwa,waafrica tunatakiwa kutengana Zaidi ya kuzidi kushirkiana,kiuchumi,ulinzi na mambo mengine mengi.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom