Tanzania yapinga ripoti ya UN ya Tume ya Haki za Binadamu

uhalisa gani anaoutaka huyu jamaa, hivi Azory kasharudi? Ben Karudi, waliommiminia risasi Lissu washapatikana? nani alizuia mikutano ya hadhara kwa miaka 5 ? nk

UN si wa kuchezea chezea, wameandika wakiwa na ushahidi tosha!! Kwa ujumla wake haya yote yanaweza kugeuka muda wowote yakawa ni mashitaka.
 
Mambo ni mazuri kweli kweli huku, inaonyesha wanatuonea gere jinsi tunavyotenda haki bin haki
Democrasia sawa lakini tunakatishwa tamaa hao UN Democrasia wanaoileta huko Libya, Syria, Iraq na kwingineko. Waliwambia wananchi wa nchi hizo kwamba marais wao walikuwa madikiteta wakaweka wasio madikiteta badly enough situation is worse.
 
Badala ya kujibu hoja kwa hoja, yeye anatoa habari za uchaguzi huu !! ambao hata nao kuna dosari kibao hasa za haya mapingamizi yasiyo na mantiki ya vyama vya upinzani pamoja na usawa kwenye media coverage wakati wa kampeni.

CCM mmejiweka wenyewe kwenye kilengeo cha UN. Awamu zote nne zilizopita walikuwa makini sana kwenye hili suala la Haki za Binadamu, sasa mmeshayakanyaga.
 
Bwashee wewe uko UN?!
 
Hivi wale vijana wawili wa Singida waliowekwa jela kwa kuonewa, waziri anaona ni haki kweli?
 
Hana hoja
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kisiasa nchini haina uhalisia kwa kuwa mazingira ya kisiasa yako vizuri.

Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ilitoa taarifa juu ya Haki za Binadamu na kuonesha wasiwasi wake juu ya hali ya Tanzania.

Profesa Kabudi amesema kuwa tathmini iliyotolewa hailingani na uhalisia wa hali ilivyo Tanzania kwa kuwa vyama vinaruhusiwa kufanya siasa kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi.

Aidha, amesema changamoto ya haki za binadamu zipo katika nchi zote, zinazonyoosha vidole na zinazonyoshewa vidole, na Tanzania inahakikisha haki za binadamu zinalindwa.

source Millard ayo
 
Huyu Prof kuna wakati alsema hadharani kuwa aliokotwa jalalani nashindwa kujua alikuwa na maana gani.
Nilitegemea ajibu kulingana na matukio yaliyotolewe mifano na siyo mambo ya kampeni za uchaguzi wa sasa
 
Hiyo demokrasia ingekuwa inaminywa hata huyu Lissu asingekuwa anaropokaropoka upuuzi kama anavyofanya sasa hivi.
upuuzi kama upi mkuu? ebu cite hata upuuzi mmmoja halafu wewe utoe maelezo ya kujibu upuuzi wa Lisu kwa maelezo yaliyo sahihi sanasana mtaishia kuongea kijumlajumla bila kutoa majibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…