Tanzania yapata Mkopo wa Sh. Trilioni 3.3 toka Standard Chartered Bank kwa ajili ujenzi reli ya SGR

Mi sijui sijaelewa,huu si mkopo ambao tutaulipa kwa pesa zetu za ndani au ni msaada?
 
Tabutupu,
Hii ngoma nzito sana kwa CCM Mpya. Wamejitwisha mzigo mzito sana kwa kukosa mikakati na maarifa kama ulivyoainisha na sasa wanatapatapa.
 
Nafikiri kati ya reli ya tazara au kati iliwakamua sana wachina hadi leo ukikutana na mchina ughaibuni ukamwambia unatoka Tanzania anashtuka. Ni kama tunaelekea huko maana ujenzi wa reli si jambo la mchezo mchezo....
 
Haha, huu sio mkopo kama ule unokopa kununua furniture dukani. Interest rate is manageable and fixed, tuna miaka 20 kulipa huu mkopo. Na nani atakukopesha kama hana uhakika na hali yako ya kiuchumi? Banks are not that reckless.
YOU DON'T ABOUT ANYTHING
 
Wakati wa uzinduzi wa reli hii, rais Magufuli alisema hii reli ya kisasa inajengwa kwa fedha za ndani.
Hivi wewe kwa akili yako ukienda benki ya biashara kuchukua mkopo au bank over draft (wenye riba ya kibiashara) kwa ajili ya kujenga nyumba yako au kiwanda chako, hizo pesa utakazochukua zitakuwa ni za kwako au ni za nani? Unataka kusema hizo fedha zinakuwa bado ni za hiyo benki?

Matajiri wote duniani hukopa benki za biashara kama hiyo Standard Bank, na kurejesha mikopo hiyo ndani ya muda mfupi plus riba ya kibiashara. Matajiri hawakopi World Bank ambao pamoja na kuwa na riba ndogo lakini masharti yao ni balaa tupu la kutaka kukutawala na kukufanya ufanye cho chote wanachokitaka hususani mpiganae tigo!!

Hizo ni pesa zetu za ndani kwani huo mkopo tutawalipa kwa fedha zetu za ndani. Na wenyewe hao waliotukopesha wamejiridhisha kuwa sisi ni matajiri na kwamba mkopo wao huo plus interest utalipwa bila shida yo yote. Na ndiyo maana wanafurahia sana kumpata mkopaji tajiri kama sisi wa trillion 3.3!
 
Haha, huu sio mkopo kama ule unokopa kununua furniture dukani. Interest rate is manageable and fixed, tuna miaka 20 kulipa huu mkopo. Na nani atakukopesha kama hana uhakika na hali yako ya kiuchumi? Banks are not that reckless.

..mkopo wowote hauna guarantee ya 100% kwamba muombaji ataweza kuulipa.

..benki inachukua risk. Na wanaokopa wanachukua risk.

..kwa maoni yangu wanaofurahia mkopo wana hoja. Na wasiofurahia huu mkopo pia wana hoja.

..ETHIOPIA ambao wamemaliza kujenga SGR kwa MKOPO toka kwa WACHINA mwaka jana waliomba kuongezewa muda wa kulipa.

..kwa kifupi tunatakiwa tuchukue tahadhari zote kuhakikisha kwamba tunarejesha mkopo.
 
Nyinyi inawasaidia kitu gani mnavyo jibaraguza kuwa mnaijenga kwa fedha zenu za ndani?

In God we Trust
Sisi watanzania hatuna shida pesa za ndan au nje....labda wewe mkimbizi ambaye ikikamilika ndo utatanguliza ngoko zako huko
 
Tanzania haijawahi kuwa na pesa ya ndani ya kuweza kujengea miradi kama hiyo.
Kwa nini uongo nao uwe mjadala mkubwa hivi?
 
Naantombe Mushi,
Hiyo Benki ni wasimamizi wa mkopo huo tu basi; wakopeshaji ni kundi la kampuni/nchi 17, zikiwemo Denmark na Sweden.
Ndio ni mkopo wa kibiashara, na riba yake 'of course' ni kubwa. Mkopo unalipwa kwa muda wa miaka 20.

Hiyo dola bilioni moja na ushee kwa muda huo sio mbaya kama mkopo utatumika kufanyia kazi uliokusudiwa kuifanya.

Wewe unadhani kuna asiyetaka mkopo wa nafuu?..., asiyejua ugumu wa kuipata mikopo hiyo ndie atakuwa amepungukiwa kichwani.

Hata hii ya kibiashara, usidhani inatolewa tu ovyoovyo pamoja na kuwa na riba kubwa. Kuna waliokataa kutoa mkopo huo.

Kwa hiyo usidhani wewe ndio mwenye maarifa zaidi kuwashinda hao waliopata huu mkopo.
 
Return Of Undertaker,
Hawa Denmark na Sweden wanatupa misaada ya bilioni 100 halafu wanatukopesha trillion 3 kwa riba ya 50%,..daah.., Ifike mahali tuwahurumie watoto na wajukuu zetu kwa hii mizigo tunayowabebesha, ni mizito sana..!
 
Hatukuelewi una mana gan ni kwamba huamini kama hivyo vimefanyika kwa hela yetu ya ndan au vp

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani, kuandika kwa haraka bila kuipitia tena kuona ikoje.

Nia yangu ilikuwa ni kusema nchi ikikopa sio kama inalimbikiza madeni na hayalipwi. Madeni ya zamani yanalipwa na mapya yanakopwa kwa maendeleo ya nchi. Cha msingi nikuona fedha zikipatika ziwe za nje au ndani zinatumikaje nini.
 
JokaKuu, Hata hizo risk zina levels, high, mid and low. Kuna risk zingine mabenki wanaweza kumeza na kuna zingine ambao wanasema hapana kutokana na trend ya ulimwenguni wa kibiashara. Hata Tanzania pia kama nchi inapima kile unachoweza kumeza na kile ambacho haiwezi.

Kwanini tulisimama Bagamoyo port, au Mtwara gas?, those where $40 billion projects which you don't just shy away. Lakini inabidi kujiuliza maswali kabla ya kurukia mambo, how much risk can we take.
 
Jamani kwani SGR si tunatumia hela zetu za ndani? Mbona tinaenda tena kukopa? Hatujaambiwa zitalipwaje hizo fedha.
 
Back
Top Bottom