Tanzania yapata Mkopo wa Dola Mil 278 kutoka Benki ya Dunia

Ktk mfumo wa kibepari lazima awepo mnyonyaji na mnyonywaji. Tajiri na maskini. Hali tulio nayo ulimwengu wa tatu imetengenezwa na hao mabeberu ya dunia. Ukoloni mamboleo ndio unatamalaki sasa.


Jesus is Lord
Hata baada ya "Kujitawala" sisi wenyewe, bado tuendelee tu kulaumu mfumo? Haiwezekani tukasema sisi tunataka kufanya mambo tofauti kidogo tuonavyo inafaa sisi wenyewe?

Ninajua jibulako mkuu, usihangaike kunijibu hilo swali nililouliza hapo.

Ngoja nitumie muda kidogo kutumia hoja yako hii, nami kuweka ninachoamini juu ya hali yetu hii tuliyomo.

Binafsi ninaamini lawama hasa inaanzia kwetu sisi wenyewe na viongozi wetu wanaotuongoza katika awamu mbalimbali, na hasa hasa hizi awamu za miaka hii ya karibuni.

Tunashindwa hata kufanya mambo madogo madogo yaliyomo katika uwezo wetu, kubadili hali zetu, na badala yake tunasubiri mikopo kama hii, inayojadiliwa hapa.

Wananchi wengi wanaoishi ndani ya nchi yetu sasa hivi ni zao la uhuru wa nchi yetu, wengi wamesoma shule zilizoanzishwa na sisi wenyewe, lakini zikashindwa kuwapa uwezo wa kutumia akili ya kutumia nyezo zilizo katika uwezo wao kubadili mazingira yao. Hata vyoo vya mashimo, inakuwa ni tatizo kwetu, kweli?

Zahanati na vituo vya afya vimejengwa huko vijijini, lakini hatuna uwezo wa kuvifanya vifanye kazi kwa ufanisi. Hatujiulizi inakuwaje?

Kilimo chetu kwa sehemu kubwa ni kilekile alichotuachia mkoloni! Mkulima ambaye amesoma kwenye shule tulizoziendesha sisi wenyewe, hajabadilika, miaka sitini? Tunasubiri mikopo,kama hii, na inapopopatikana, hatujui inakopitia?
Hapo mwanzo, baada ya uhuru, tulisema kukosa watu wetu wenye elimu na utaalam katika mambo mbalimbali ilikuwa ni kikwazo kwetu.
Watu wakasomeshwa, tena kwa wingi na kwa gharama kubwa. Leo hii sidhani kuna eneo ambalo hatuna watu walilolisomea ndani ya nchi hii, lakini huoni kazi za hawa watu, sana sana itakulazimu uende ndani ya CCM, na utawakuta wamejazana huko, wakifanya yao yanayowafaa wao wenyewe, na siyo kunufaisha taifa.

Viongozi wetu sasa wameamua, kwamba sisi hatuwezi kuleta maendeleo katika nchi hii, kwa hiyo njia sahihi na bora iliyopo, ni kuagiza watu toka nje, waje watuletee maendeleo!

Hakuna kiongozi anayetaka kufanya kazi na wananchi hawa, kuwatia moyo na kuwahimiza wajiletee maendeleo ya kweli. Wananchi nao sasa wanawasikiliza viongozi wao, wakisubiri waletewe maendeleo, huku raslimali za nchi yao zikizolewa kama takataka!

Sasa acha tusubiri maendeleo, miaka sitini mingine inayofuata toka sasa! Sijui kama bado utakuwa upo kuyafaidi hayo maendeleo, au vipi mkuu 'BloodofJesus'?
 
Kuna wakati unatamani tuwakabidhi nchi watu wanaoweza kutuletea maendeleo. Sie abaki rais tu kama nembo lakini mambo ya uongozi, utawala na mipango ya maendeleo na utekelezaji wapewe watu wengine, sie tuwalipe kamisheni ya hiyo kazi.

Ukiangalia gharama zinatumika Kwa bunge, viongozi na kuendesha serikali ni mzigo Kwa wananchi na tija haipo kiviile.

Mikopo tutapewa lakini Mara nyingi inaishia kutafunwa na wachache huku deni la taifa likiongezeka.

Nnachokiona Kwa Sasa ninitahidi kustaafu na kuwaachia chochote wanangu. Kupata rais atakaeiletea maendeleo hii nchi na ikabadilika, ni zaidi ya miaka 30 ijayo.
 
Bora ya Samia mara 100000 kuliko yule sadist wenu aliyekuwa anakopa kimyakimya ...na kuhonga wapinzani wamuunge mkono
 
sasa tunaenda kushuhudia ujenzi wa bonde la msimbazi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa flyover pale jangwani
 
Mfumo wa elimu yetu umekaa hovyo, haumwandai mtanzania kujitegemea kimaarifa, asipoajiriwa amekwama. Na once anapoajiriwa anawaza kuiba tu yaani kujinufaisha kibinafsi. Mtu anaitwa msomi lakini ni kwa kukariri ideas za hao hao wazungu, najua unajua kuwa huwa tunasoma kufaulu mitihani.

Unaonaje unalima mazao malighafi ambayo huwezi kuitumia. Hadi uwaombe hao hao wazungu wanunue, wasiponunua umekwama. Na wananunua kwa bei wanayokupangia.

Una mali ndani ya ardhi yako madini na vito vya thamani huwezi kuchimba hadi uwaombe hao hao wazungu waje wachimbe!

Unalazimishwa uishi watakavyo ukijidai kujitenga nao wakikupiga "vikwazo" athari zake zinakuwa dhahiri. Kumbuka kilichowatokea nchi ya Zimbabwe kipindi kile cha Mugabe kwenye ishu ya wakulima wa kizungu nchini mwake.

Ukiona tunawakopa, ujue tokea karne nyingi walishajua kuwa tutafika muda ambao lazima tutawakopa tu. "the situation that we are experiencing now is a created one by those people over there"

Nakumbuka wimbo wa mtu mmoja unasema: "the world is not my home"


Jesus is Savior
 
Bora ya Samia mara 100000 kuliko yule sadist wenu aliyekuwa anakopa kimyakimya ...na kuhonga wapinzani wamuunge mkono

Kwanza kabisa jifunze kujikita kwenye hoja acha mambo ya kufikiria unachowaza wewe ndivyo kilivyo, hiyo kauli "sadist wenu" inaingiaje hapa? Unajua mie nipo upande upi?

Tukirudi kwenye hoja, hakuna unafuu wowote. Ndio maana nikasema tungekabidhi tu haya mambo nchi iendeshwe kama kampuni Kwa kuzingatia KPI, tungekua mbali sana.
 
Kukopa kwa mwafrika imekuwa sifa kutwa kutangaza kwenye magazeti

Wenzetu wanaandika maendeleo yao sisi tunajisifia kukopa halafu hatuoni hiyo mikopo imesaidia nini

Deni la Taifa linapaa ila watu bado wanauza maji kwa ndoo mpaka mikoani ambapo leo tungekuwa na mabomba ya maji kila kaya

Miaka ya 70 mitaani kulikuwa na maji ya bure kutoka idara ya maji
Hiyo mikopo wacha waibe tu
 
Wewe hapo kwako hata kisima cha laki 2 umechimba?
 
Wachimbaji gani hawana hamu hao?yaani umekaa nyuma ya keyboard unaanza kuharisha....tuna vijana wa hovyo Sana nchi hii
Mkuu, ukweli unauma, inabudi uuzoee!!

Kwenye machimbo huko kuna vilio, wanatimuliwa tuu huko ili waheshi miwa.... Waji milk she wao aisee, huyo mtu anaitwa Ro 1, mtamkoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…