Tanzania Yaongoza Unywaji wa Mataputapu

Tanzania Yaongoza Unywaji wa Mataputapu

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,425
Reaction score
3,300
uploadfromtaptalk1365227006957.jpg

Utafiti wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebainikwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu (mataputapu).

Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.Kwa mujibu wa utafiti huo,Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52,ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07.Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa pombe chafu.

Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.

Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Figo, Dk Francis Fulia aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo kwa sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama.

Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao."Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini,moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha," alisisitiza.

Dk Fulia pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo."Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo,inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi" alisema.Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya.

Katika miaka ya hivi karibuni,kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine.


Source: Mwananchi
 
Wasira na kinana ndio wanywaji wakubwa wa mataputapu....ccm wandaaji nguli wa mataputapu nchini.......MAISHA MAGUMU,NA VITISHO KWA KILA MTANZANIA.
 
Watu tumekwenda shule kwa ajili ya haya mataputapu ila sasa mama yangu kaacha kupika daa tumetoka mbali, haya yote yanaonyesha kiwango cha umasikini coz hii pombe sasa inauzwa lita 500/= sasa kwa nini unywe bia inayouzwa 2000/= wakati kwa ya kienyeji napata lita 4. Kwa hiyo hapa nawapa heko hawawatu wanatumia kanuni za uchumi
 
Kenya wameachwa wapi na ile kumi kumi yao iliyoua watu vile kipindi kile.........manina zake huyo aliyetoa hiyo takwimu.......
 
Sasa kumbe tunashika nafasi ya tano, inakuwaje unasema tunaongoza mkuu?? Mbona unajichanganya mwenyewe??
 
Kenya wameachwa wapi na ile kumi kumi yao iliyoua watu vile kipindi kile.........manina zake huyo aliyetoa hiyo takwimu.......
Ukiona hivyo ujue huko Kenya wanaokunywa pombe za kienyeji ni wachache, binafsi naona kuziita pombe hizo mataputapu ni tusi. Huyo Dr. aliyefanya utafiti namshangaa kujifanya haelewi chanzo cha msongo wa mawazo hapa kwetu. Tatizo ni umaskini maana wanywaji wa pombe hizo ukiwapelekea bia watafurahi. Pato lao haliwaruhusu kununua bia. Sababu kubwa ya kunywa pombe yoyote iwe ya kienyeji au kizungu si msongo wa mawazo wanywaji uchukulia pombe kama kiburudisho na hivyo uwaongezea furaha katika maisha.

Pamoja na hasara zake ikiwemo kusababisha magonjwa, kudhoofisha uchumi, kusababisha njaa, hajari nk bado jamii inaendelea kutengeneza na kunywa pombe. Binafsi naona tunachotakiwa kufanya ni kuimprove namna ya kuandaa pombe hizo ili tupunguze madhara kwa wanywaji. Ukiangalia vitu viletavyo madhara kwenye afya za watanzania ni vingi sana kikiwemo chakula tunachokula kutokana na mazingira kinavyozalishwa na kuandaliwa. Yapo mambo mengi sana tunakohitaji maboresho.

Mtu akielimika na kipato chake kikaongezeka anakuwa macho na anachokula pamoja na kunywa. Lakini kwa hizo Division zero za form IV na wale wanaomaliza darasa la saba bila kujua kusoma au kuandika kuna Elimu hapo? Wamarekani wana msemo wao usemao " You are what you eat" (eat= kula na kunywa). Slogan ya CCM wakati wa uchaguzi ilikuwa maisha bora kwa kila mtanzania labda niwaombe akina Nape watueleze huwa wana maana gani wanaposema maisha bora? Na watwambie ni hatua gani mtu wa kijijini au watanzania walio wengi waliyopiga kuhusu kuelekea maisha bora. Maana to honest maisha bora kwa walio wengi hakuna. Unywaji wa pombe uliokithiri pamoja na mambo mengine yasiyokubalika katika jamii ni kielelezo tosha kwamba hatuna maisha bora.
 
Sasa kumbe tunashika nafasi ya tano, inakuwaje unasema tunaongoza mkuu?? Mbona unajichanganya mwenyewe??

Kuongoza ni mpaka uwe namba 1? Badilika hata ukisikia shule kumi zinazoongoza unajua ni namba 1 zote? Iko kazi
 
Wazungu bwana, dadeki zao...hizo pombe babu zetu walizinywa tena wakishushia minofu ilichomwa ya nguruwe..wakaishi miaka mingi mno kuliko sisi tunaokunywa mibia yao hii iliyo jaa kansa!
 
Kuongoza ni mpaka uwe namba 1? Badilika hata ukisikia shule kumi zinazoongoza unajua ni namba 1 zote? Iko kazi


Mkuu nadhani hapo tunapishana tu kiswahili! Mtu ukisema shule imeongoza maana yake ni ya kwanza lakini ukitaka kuonyesha kuwa ni miongoni mwa shule zilizoongoza ni bora utumie kauli ya wingi badala ya umoja!! Title ya hii thread ingesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kunywa mataputapu Afrika nadhani inge-sound better!!
 
Hawa jamaa vipi??? Eti Makimaro aache kupika Mbegee... Unataka uchumi uyumbe!!!! Ili tuendelee kuwaomba 'unga' Hizi pombe (japo sizitumii) ni fahari yetu. Simemiss harufu ya mbege. Kweli tunapaswa kubadili mazingira, poa, je tunao uwezo?? Pombe zao ambazo ni 'salama' zimethibitika pasipo na shaka kuchangia shinikizo la damu, kisukari,.. Je kati ya hizo pombe zao 'sala' na zetu zipi zinamadhara makubwa kwa jamii?? Naona wanaamua kujibu mashambulizi.
Nimekumbuka nadharia moja ya ustawi (Theory of the Second Best ) jaribu kuipitia.
HAWA WAANDISHI WANAOKASHFU FAHARI YETU ILI HALI UCHUMI WA VIJIJINI (KWENYE WATU WENGI) UNATEGEMEA POMBE ASILIA WANAPASWA KUJITATHMINI.
Kwa hali tutajaletewa digitali ya pombe za kienyeji.
 
Kenya wameachwa wapi na ile kumi kumi yao iliyoua watu vile kipindi kile.........manina zake huyo aliyetoa hiyo takwimu.......
heheheheee,kenya wanaongoza kwa mambo muim tu,kama kupokea watalii wengi zaid ya nchi yeyote east afrika,kuzima sim za kichina,kufanya uchaguz wa digitali
 
Mataputapu!!! Sijui nini maana yake halisi, ila nadhani ni pombe za asili za watanzania. Tunaaminishwa na kuamini kila chetu ni cha kishenzi ndiyo maana tunachezea fedha za kigeni ambazo hatuna kuagiza hata vitu ambavyo tungeweza kutengeneza wenyewe. Kwa namna nijuavyo mimi duniani kote kuna aina mbili za teknologia ya kutengeneza pombe (Home made technology na commercial- viwandani). Commercial ni kwa ajili ya soko kubwa na kibiashara zaidi wakati homemade ni kwa ajili ya matumizi ya familia na kiasi kidogo kuuzwa kwa watu wa karibu, kwa wale wajuwao chemistry ya pombe ni kwamba homemade (mataputapu) mara nyingi ndiyo aina bora kabisa ya pombe kwani imetengenezwa kwa njia za asili pasipokuongeza kemikali ambazo ni hatari sana kwa afya ya binadamu. Mfano rahisi nenda katika chupa yoyote ya wine iliyotengenezwa katika viwanda vikubwa uangalie viambaupishi utaona kemikali nyingi ikiwamo sulphite, jaribu kugoogle side effect za hizo kemikali. Nawasiwasi na huyu mtaalamu wa Muhimbili kama kweli anaielewa vema chemistry ya pombe, swali hili alipaswa kuulizwa mfamasia au chemisists ambao wanaweredi wa nini kilichopo ndani ya chupa ya gongo vs kiroba (sprite), mbege vs bia.

Ni kweli kuna udhaifu katika pombe zinazotengenezwa nyumbani katika swala la usafi, na hii tunaisemea sana kwa sababu tuko karibu na hao watengenezaji, je nani anaelewa kwa uhakika usafi na usalaama wa malighafi za viwanda vya bia? Isijekuwa wanatumia mpaka sukari zilizoexpire kama zile za ARV. Watanzania tufungue macho, isije kuwa utafiti huu umelipiwa na viwanda hivyo kwani tunataarifa viwanda vikubwa vya bia hapa Tanzania vinatengeneza pombe za kienyeji na zimefikia hatua za kuzipaki kwenye madumu ya lita 20 na kuwasambazia akina mama wanaouza pombe za asili. Isije kuwa tunaonyeswa gololi tuache almasi zetu!!!!

Ningeomba pia wanajamvi mnisaidie pombe kama kibuku (TBL DSM), Zagamba (TBL MWANZA) na viroba viko kundi gani.
'
 
Does Uchafu means kwamba haijapimwa ?

Sababu gongo ni kama konyagi tofauti ni TBS tu..., hawa jamaa wasije wakawa wameweka pombe zetu za mnazi, rubisi, mbege na wanzuki kwenye hili fungu la pombe chafu 🙁
 
Kenya wameachwa wapi na ile kumi kumi yao iliyoua watu vile kipindi kile.........manina zake huyo aliyetoa hiyo takwimu.......


Na jana nliona citizen kuna watu watatu wamekufa kwa sababu ya pombe za kienyeji.
 
Wanaziita Mataputapu a.k.a mbogamboga,ukinywa unazuga na bia moja kutoa harufu mdomoni! Kule kwetu tulisomeshwa kwa hizi pombe mnazoita chafu!
 
Nadhani wangepewa semina watengenezaji wawe wanapika ktk mazingira ya usafi,japo c wote wengine ni wasafi.lakini hizo kejeli eti mataputapu,pombe chafu huyo ni mhuni na huo ni utumwa wa mawazo.asili ya mwafrika hiyo senzi
 
hilo gazeti likiwafikia wanywaji wa gongo,wanzuki,nk wanaweza kukumaliza
 
Back
Top Bottom