Tunapongeza serikali kwa kurejesha umiliki wa TTCL mikononi mwa Watanzania, lakini tunailaumu kwani ni tamaa ya utajiri, waliokua nayo baadhi ya viongozi wa serikali kipindi kile ndio ilisababisha waibinafsishe TTCL, hakukuwa na haja hiyo.
Kama alivyowahi kusema hayati J K Nyerere, hana shida sera ya ubinafsishaji bali alitoa angalizo serikali iangalie yale mashirika yaliyoshindwa kujiendesha ndio yafanyiwe hiyo kitu mbaya. na yale yanayojiendesha na kodi yanalipa yaachwe.
Na hata ukiangalia huo ubinafsishsji wa TTCL ni wizi wa mchana kweupe tu ulifanyika, hao watu hawakuja na sent tano walikuja na brifcase ambazo walipewa viongozi wa umma baadhi yao , huku serikali ikiambulia patupu, ukitaka kuliona hilo jiulize inakuwaje aliye na hisa chache amiliki kila kitu?
Kama haitoshi ikaanzishwa celtel kwa mtaji toka TTCL wakitumia license ya TTCL, ikisikika ni kampuni tanzu .mara imekuwa ndio kila kitu na muamuzi wa maisha ta TTCL, haikutosha. Muda si muda ikamegwa na kuwa kampuni huru.
Nchi hii wacha wang'ang'anie madaraka maana zimwi likujualo halikuli likakwisha. Ingelikuwa China tumeshawasahau baadhi yao. Nampongeza sana rais Jakaya Kikwete kurekebisha kasoro hii iliyofanywa na waliomtangulia kwa faida ya Watanzania wote.