Tanzania yajiandaa kupokea ndege tano ilizozinunua hivi karibuni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
1645618747212.png

Siku chache baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha bungeni taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2021/2022 ilieleza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania limepata hasara jumuishi ya Sh152.96 bilioni tangu mwaka 2015/16.

Leo Jumatano, Februari 23, 2022 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), Dk Ally Possi alitembelea ofisi za ATCL zilizopo jijini Dar es Salaam na kuweka wazi kuwa athari za ugonjwa wa Uviko-19 ni chanzo cha hasara ya Sh60.24bilioni katika shirika hilo.

Akijibu swali mbele ya wanahabari leo wakati wa ziara yake ofisi za ATCL, Dk Possi amesema;

“Hasara ile imetengenezwa na sababu nyingi, kama utakumbuka ugonjwa wa Uviko ulikuwa umeathiri sekta ya usafirishaji wa anga sio kwetu tu ila mashirika mengi ya ndege duniani tukiwamo sisi pia,”amesema.

Hata hivyo amesema kumekuwa na juhudi za kukabiliana na hasara hiyo ikiwemo kuboresha viwanja vya ndege nchini huku Serikali ikijiandaa kupokea ndege nyingine tano ilizonunua ili kukuza mapato

Kwa mujibu wa ATCL, kwa sasa ina jumla ya vituo 15 vya safari ndani ya nchi na vituo vinane nje huku ikiingia ushirikiano wa huduma za usafiri na mashirika ya ndege ya Rwanda, Qatar, Ethiopia.

Kuhusu fursa ya usafirishaji wa bidhaa za ndani katika masoko ya nje, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Ladislaus Matindi amesema tayari wameshaanza kuifuatilia fursa hiyo kwa masoko ya India na Marekani.

MWANANCHI
 
Safii sana, hasara ndo mwalimu na tatajufunza kupitia changamoto. Cha ajabu sijasikia kama ndege ya mizigo (cargo plane) ni kati ya hizo ndege mpya maana njia pekee ya kupeleka bidha njee ni sisi kuwa na ndege yetu ya mizigo
 
Hivi kuna umuhimu gani kuwa na ndege nyingi ambazo gharama zake za safari haziendani na hali ya mtanzania wa kawaida?

Shilika linashindwa nini kujifunza Kwa fast-jet ambae alikuwa mshindani wake na akafanikiwa kuwa na wateja wakutosha kabla ya Jiwe kuiua?

Na wataendelea kupata hasara zaidi kama wasipobadili namna ya uendeshaji wa shilika.
Ndege nyingi ni ngapi ndugu
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Hivi kuna umuhimu gani kuwa na ndege nyingi ambazo gharama zake za safari haziendani na hali ya mtanzania wa kawaida?

Shilika linashindwa nini kujifunza Kwa fast-jet ambae alikuwa mshindani wake na akafanikiwa kuwa na wateja wakutosha kabla ya Jiwe kuiua?

Na wataendelea kupata hasara zaidi kama wasipobadili namna ya uendeshaji wa shilika.
Usafiri wa anga ni anasa kwa mtanzania wa kawaida
 
Kama nusu tu ya pesa hizo zingewekezwa kwenye kilimo cha mazao mkakati kama vile Alizeti, Ufuta na Michikichi katika baadhi ya wilaya hapa nchini tukishirikisha vijana kama wabia wakuu nafikiri leo tusingekuwa tunahaha kununua dumu la mafuta ya kupikia ya lita tano kwa Tshs. 40,000 na tungeweza ku- export mafuta hayo kwa majirani zetu kuingiza fedha za kigeni.
 
Wewe unawaza hivyo wenzako wanapiga pesa ndefu sn kwenye manunuzi
 
Kama nusu tu ya pesa hizo zingewekezwa kwenye kilimo cha mazao mkakati kama vile Alizeti, Ufuta na Michikichi katika baadhi ya wilaya hapa nchini tukishirikisha vijana kama wabia wakuu nafikiri leo tusingekuwa tunahaha kununua dumu la mafuta ya kupikia ya lita tano kwa Tshs. 40,000 na tungeweza ku- export mafuta hayo kwa majirani zetu kuingiza fedha za kigeni.
Bwashee kupanga ni kuchagua!
 
Ni hatua nzuri maana shirika letu lilikuwa halina ndege.. angalau sasa tunatembea kifua mbele. Ni wajibu wa ATCL sasa kuhakikisha kuwa ndege hizi zinakuwa na nauli nafuu ili watanzania wengi zaidi wapande ndege.
 
Kuna watu watakuja kulalamika! Ujumbe wangu kwao tafuteni hela mkapande ndege acheni makasiriko!
"Watu wa Bongo mbona hamna utu moyoni
Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara
Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara
Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao"

wewe utakuwa umekula umevimbiwa
 
Kwahiyo wewe anasa uioni.au bongo hii kwa uchumi gani tulionao hadi tuwe na midege mingi kiasi hicho.Hizo ela zingeweza kufanya mambo mengine yakawaida ambayo tunaangaika nayo leo kwa pesa za mkopo wa riba.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Nambie ni hasara zipi zimepatisha hizo ndege..?
Serikali yako imeamua itumie njia ya manunuzi ya ndege sasa hapa tutabishana na wameshafanya!.
 
Safii sana, hasara ndo mwalimu na tatajufunza kupitia changamoto. Cha ajabu sijasikia kama ndege ya mizigo (cargo plane) ni kati ya hizo ndege mpya maana njia pekee ya kupeleka bidha njee ni sisi kuwa na ndege yetu ya mizigo
Wanasubiri zifike mengine watajua badae
 
Siku chache baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha bungeni taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2021/2022 ilieleza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania limepata hasara jumuishi ya Sh152.96 bilioni tangu mwaka 2015/16.

Leo Jumatano, Februari 23, 2022 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Uchukuzi), Dk Ally Possi alitembelea ofisi za ATCL zilizopo jijini Dar es Salaam na kuweka wazi kuwa athari za ugonjwa wa Uviko-19 ni chanzo cha hasara ya Sh60.24bilioni katika shirika hilo.

Akijibu swali mbele ya wanahabari leo wakati wa ziara yake ofisi za ATCL, Dk Possi amesema;

“Hasara ile imetengenezwa na sababu nyingi, kama utakumbuka ugonjwa wa Uviko ulikuwa umeathiri sekta ya usafirishaji wa anga sio kwetu tu ila mashirika mengi ya ndege duniani tukiwamo sisi pia,”amesema.

Hata hivyo amesema kumekuwa na juhudi za kukabiliana na hasara hiyo ikiwemo kuboresha viwanja vya ndege nchini huku Serikali ikijiandaa kupokea ndege nyingine tano ilizonunua ili kukuza mapato

Kwa mujibu wa ATCL, kwa sasa ina jumla ya vituo 15 vya safari ndani ya nchi na vituo vinane nje huku ikiingia ushirikiano wa huduma za usafiri na mashirika ya ndege ya Rwanda, Qatar, Ethiopia.

Kuhusu fursa ya usafirishaji wa bidhaa za ndani katika masoko ya nje, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Ladislaus Matindi amesema tayari wameshaanza kuifuatilia fursa hiyo kwa masoko ya India na Marekani.

MWANANCHI
upuuzi mtupu, zinasaidia nn ili maisha ni magumu?
 
Kama nusu tu ya pesa hizo zingewekezwa kwenye kilimo cha mazao mkakati kama vile Alizeti, Ufuta na Michikichi katika baadhi ya wilaya hapa nchini tukishirikisha vijana kama wabia wakuu nafikiri leo tusingekuwa tunahaha kununua dumu la mafuta ya kupikia ya lita tano kwa Tshs. 40,000 na tungeweza ku- export mafuta hayo kwa majirani zetu kuingiza fedha za kigeni.
Au tuwekeza kwenye tikitiki maji😁😁😁
 
Back
Top Bottom