Tanzania yafungwa 5-1.......

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,428
2,281
Twiga Stars yamkuna Roger Miller

TIMU ya soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’, jana iliwasili jijini Dar es Salaam kutoka Cameroon ambako licha ya kunyukwa mabao 2-1, imeacha gumzo kutokana na kiwango cha kuvutia, hata kumduwaza nguli wa soka wan chi hiyo, Roger Miller.
Timu hiyo iliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 3:30 asubuhi na kupokewa na viongozi waandamizi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakiongozwa na Katibu Mkuu, Fredrick Mwakalebela, Salum Madadi na Dany Msangi.

Akizungumza mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa, alisema vijana wake walicheza kufa au kupona hata kuacha gumzo, kubwa kwa mashabiki wa soka nchini humo.

Alisema, kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake, wengi hawaamini kama timu hiyo ndiyo ilifungwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya Februari 23.

Mkwasa alisema, ingawa wachezaji wote walicheza vema, lakini kivutio kikubwa alikuwa ni Fatma Mustapha, aliye mdogo kuliko wote katika timu hiyo.

Kocha huyo aliyewahi kucheza na kufundisha timu mbalimbali, ikiwamo Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars, alisema Fatma ndiye aliyesababisha bao pekee la Twiga, ambalo lilifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ kabla ya Cameroon kusawazisha na kuongeza jingine.

“Mchezaji huyu mdogo kuliko wote katika timu, tulikuwa tukiogopa hata kumpanga, lakini Cameroon kaonyesha uwezo mkubwa na kuwa gumzo, hata wadau kutushauri vipaji hivi viendelezwe,” alisema Mkwasa.

Mkwasa alisema, baada ya mpira kumalizika, wadau mbalimbali wa soka akiwamo mkongwe Miller, walionyesha kuvutiwa na vipaji vilivyoko Twiga na kushauri timu hiyo iendelezwe zaidi kwani baada ya miaka mitatu watatisha.

Naye Mkuu wa msafara, Elizaberth Kalinga, aliipongeza TFF na Watanzania kwa ujumla kwa misaada na dua zao ambazo zimefanikisha kwenda na kurejea salama katika safari hiyo.

Aidha, Kalinga ameishauri TFF kutafuta wafadhili wa kudumu wa timu hiyo ili waiendeleze kwa manufaa ya baadaye, badala ya TFF kuendelea na mtindo wa kutembeza bakuli, kwani Twiga itakuja kuitoa kimasomaso Tanzania muda si mrefu kama itaendelezwa.

Naye Katibu Mkuu wa TFF, Mwakalebela aliwapongeza wachezaji kwa kwenda kupigana kufa au kupona na kuwa Watanzania kwa ujumla wameridhishwa na matokeo hayo kutokana na historia ya soka la Cameroon ukilinganisha na Tanzania.

Alisema, katika kuiendeleza timu hiyo, TFF iko katika taratibu za mwisho za kusaini mkataba na taasisi moja isiyo ya kiserikali (NGO’s), ambayo itakuwa ikiitumia timu hiyo kama mabalozi wao.

Mwakalebela alisema, katika mpango huo ambao unatarajiwa kuanza Mei mwaka huu, timu hiyo itakuwa ikifanya ziara mikoa 17 kwa kucheza mechi za kirafiki, ambako pamoja na mambo mengine, pia kuhamasisha mechezo huo kwa wanawake.

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa kalenda ya TFF, Agosti mwaka huu, wataendesha mashindano makubwa ya kitaifa kwa wanawake, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera kutaka iwepo ligi ya kitaifa kwa wanawake.

Naye Nahodha wa Twiga Stars, Sofia Mwasikili ‘Singo’, aliiomba TFF, kutoifanyia mabadiliko timu hiyo bali iendelezwe na kuwa katika mechi walizoshiriki wameweza kupata uzoefu wa kutosha.

Kambi ya timu hiyo ilitarajiwa kuvunjwa jana, ambako wachezaji wa Dar es Salaam watarejea makwao huku wa mikoani kama wakiwapo watafanyiwa utaratibu wa usafiri kurejea kwao.

Twiga Stars iliondoshwa katika kinyang’anyiro hicho cha kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa wanawake, baada ya kulala kwa jumla ya mabao 5-1.
 
Back
Top Bottom