Tanzania yaelekea kushindwa kutimiza Malengo ya Milenia MDG’s

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=2][/h]


TANZANIA inaelekea kushindwa kufikia Maendeleo ya Malengo ya Milenia (MDGs) ya kupunguza vifo vya akina mama wakati wa uzazi ifikapo mwaka 2015. Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Mtaalamu Mshauri wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Rose Mwaipopo.

Alisema hadi mwaka 2010, Tanzania ilikuwa imeshapunguza vifo vya akina mama hadi kufikia vifo 454 kwa kila akina mama 1,000.

“Katika Malengo ya Milenia, inatakiwa hadi kufikia mwaka 2015 vifo vya akina mama wakati wa uzazi viwe vimepungua hadi vifo 133 kati ya akina mama 1,000 lengo ambalo hadi sasa sio rahisi kulifikia.

“Sababu kubwa ya kutofikia lengo hilo ni kuwapo kwa akina mama ambao bado wanajifungulia kwa wakunga wa jadi badala ya kuhudumiwa hospitalini,” alisema Dk. Mwaipopo.

Alisema lengo ni kufikia asilimia 90 ya akina mama wanaopewa huduma za uzazi na wahudumu wa afya ifikapo mwaka 2015.

Alisema hadi mwaka 2010, asilimia 50.5 ya akina mama ndio waliokuwa wakihudumiwa na wahudumu wa afya wakati wa uzazi, hali ambayo haiwezekani kufikia Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2015.

Alitaja malengo mengine ambayo yanaelekea kutofanikiwa kuwa ni pamoja na suala la usalama endelevu wa mazingira, kupunguza na kuondoa ufukara na njaa ikiwamo kushindwa kupunguza idadi ya watoto wa umri wa miaka mitano waliodumaa.

Alisema malengo yanayoelekea kufanikiwa ni pamoja na kufanikisha elimu ya msingi, kuinua haki za kijinsia na kuwawezesha wanawake na kupunguza vifo vya watoto.

“Malengo mengine yanayoelekea kufanikiwa ni kupambana na Virusi Vya Ukimwi, malaria na maradhi mengine na kuendeleza ushirikiano wa kimataifa,” alisema Dk. Mwaipopo.

Alisema lengo la mkutano huo ni kusikiliza maoni ya wadau ikiwamo kuibua changamoto katika kufikia malengo hayo na kuzifikisha Ofisi ya Rais Tume ya Mipango kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa, Dk Rehema Nchimbi, aliwataka wadau hao wakati wakijadili malengo hayo wasizichukie changamoto zilizopo badala yake wapendekeze nini kifanyike.

“Kitu chochote kizuri kikiwa kinafanyika, lazima kuwapo na changamoto hivyo tuangalie nini kifanyike ili kukabiliana na changamoto hizo,” alisema Dk. Nchimbi.
 
Back
Top Bottom