Tanzania ya VIWANDA: Tuko wapi,tunaenda wapi na tutafikaje??

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,763
5,591
Tunatoka katika KILIMO KWANZA japo bado hatujafanikiwa sana, Tunaelekea TANZANIA YA VIWANDA.

Hii ni kitu ninayoiunga mkono 100%. Ni aibu kuimport nguo za mitumba,stick,maziwa ya unga, vyuma,Furniture, na bidhaa kibao huku tuna rasilimali watu,chuma (madini,), makaa ya mawe, mazao ya kilimo na vitu vingi ya kututoa huko.

Unadhani Rais JPM afanye nini ili Mapinduzi ya Viwanda Tanzania yawe halisi. Je unaona spidi hii iko sawa?Watu wamjiandaa kufungua viwanda hata vidogo?Je watu wako tayari kununua bidhaa za ndani? Miundo mbinu na masoko yanaandaliwa kwa kasi inayotakiwa?

unaweza ongeza thamani kwa taifa kwa kutoa suluisho au nini kifanyike ili mpando hii uwe halisi kwa kila mtanzania.
 
kwanza wawekezaji wa ndani pamoja na viwanda vilivyoanzishwa waangaliwe suala la operation cost ni kubwa kutokana na kodi kubwa ambayo wanatozwa ..pia serikali iwape motisha kwa wawekezaji wa ndani wanaotaka export nje ya nchi hasa taxes reduction ya atleast 30% kama wanavyofanya nchi jirani mfano kwa sasa dangote kawekeza kiwanda cha cement tanzania ila ukija suala ya bei ya cement ya dangote ni cheap compare na twiga cement reason ikiwa anapata punguzo toka serikali ya nigeria kwenye uwekezaji huo....
 
Frankly, Tanzania ya viwanda ni ngumu sana kwa mfumo huu.

Unapoongelea rasilimali watu ujue unaongelea skilled and unskilled labour.

Mfumo wa elimu ni mbovu (umekufa) hivyo skilled competent labour ni ngumu kupatikana sasa na pia huko mbeleni. Hii inaongeza gharama kwa kiwanda kuajiri skilled labour na kulipa bei kubwa (wachache waliopo ni ghali au waajiri nje ya nchi kwa gharama zaidi). Ni ndoto kuwaza viwanda kama kiwango cha elimu kinazidi kuporomoka.

Pili unskilled labour (vibarua) ni expensive. Nchi tunazoiga watu wanatumikishwa kwa ujira mdogo na tunaviona hivyo viwanda vyao tunavyotaka kuiga. Mfano, China, Indonesia, Vietnam etc. watu wanajiua kwa sababu ya kazi nyingi, ngumu, ujira mdogo na zero compliance to safety regulations. Huku, generally speaking, ni ngumu kupata vibarua wanaokubali mazingira hayo ya kazi.

Teknolojia pia ni tatizo. Teknolojia inaongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza gharama. Kwa sababu Serikali haijaweka kipaumbele katika R&D tunaona nchi haina ubunifu katika sekta ya teknolojia. Hivyo inabidi tu-import teknolojia na hii inaongeza gharama katika kiwanda pia.

Mikopo ya benki ipo katika riba kubwa inayomkimbiza mwekezaji. Mfano unataka kuagiza mashine kwa mkopo wa benki, utaona riba ni kubwa, pia kwa sababu mashine itahitaji repairs, spares nazo utaagiza nje kwa sababu hapa hamna. Hii inaongeza pia gharama.

Mfano mwingine ni gharama ya vitu kama umeme. Umeme pia ni tatizo. Gharama za umeme zipo juu. Unaweza ukaajiri watu kwa bei kubwa, ukanunua vifaa na mashine zako kwa bei kubwa na kwa mkopo na umeme usiwake kwa mwezi. Hiyo ni hasara!

Pia ili uwe na viwanda inabidi uwe na serikali rafiki na sekta binafsi na wakezaji (wa nje na ndani). Kwa miezi hii michache serikali imekua aggressive kiasi kwamba inatisha wawekezaji. Hapa hatujaongelea kodi kibao serikali hii inazotoza.

Hivyo kuendesha nchi kwa viwanda ni mfumo. Ni sera endelevu na huwezi kukurupuka na kuanza tu. Ni kuwa na sera bora katika elimu, ubunifu, sayansi na teknolojia, miundombinu n.k
 
uko sawa kabisa mkuu.
Ijulikane kuanzisha kiwanda sio kazi rahisi. katika stage ya kuanza na stage ya kujitanua (expansion) ndipo serikali inapaswa pia kuwa na msaada wa karibu kwa kutoa unafuu kwa wazawa.
 
Kwanza tukiangalia sera ya viwanda vidogo na kati iko vizuri sana shida ni utekelezaji wake umekua shida.
Tuanze na SIDO imepewa mandate ya kusaidia wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati viweze kufanya primary and secondary processing. Mafunzo wanatoa kisha wanatekelezwa kwa maana mwenye wazo hasaidiwi vya kutosha kufikia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda hivyo.
Wakati huo huo SIDO wamekuwa wakitoa mikopo kwa wajasiriamali hao kwa riba kubwa lakini core busiiness ya shirika sio kutoa mikopo bali kusaidia viwanda vidogo na kati na kama ni mikopo ilibidi itolewe kwa wajasiriamali wenye mawazo yanayotekelezeka.
Nini kifanyike rais magufuli alifumue shirika la umma sido lirudi kwenye core business yake, waanzishe viwanda vidogo, kukuza viwanda vido ili viwe vya kati na vya kati viwe vikubwa. Sido iondokane na mambo mengine yote badala yake kusaidia SMEs tu.

Ukuaji wa viwanda vidogo ndio msingi wa kukua kwa viwanda vya kati na vikubwa.

Sehemu ya kwanza inayoweza kufanya transfomation ya uchumi wa tanzania ni agro processing. Angalia tu muhogo technolojia ya kusindika haizidi 3million lakini bado watu wengi hawajaingia. Shida kubwa mitaji na pale inapopatikana riba kubwa.
 
Sera ya matokeo makubwa sasa(BRN) ILIMSHINDA MTANGULIZI WA JPM... KAMA INGEFAA JPM ANGEIHUISHA UPYA ILI IENDANE SAMBAMBA NA MFUMO WA VIWANDA... EMBU ANGALIA MALAYSIA TULIPOCOPY HIYO BRN WAO WAKO WAPI KIUCHUMI...WAKO MBALI ZAIDI YETU..SHIDA MOJA TZ SIASA NYINGI, KUBEBANA KWINGI NK
 
Kuhusu suala la skilled labour kama ilivyosemwa na msemaji hapo juu sio kweli kwamba hakuna skilled labour, wapo wengi sana.

Kuna fani chache sana oil, gas and mineral processing ndio wapo wachache the rest of the skills wapo, fanya research yako vizuri utaona.

Ila suala la mitaji na umeme nakubalina nawe 100% isipokuwa ningemshauri Mh.Rais badala ya kutoa 800billion kwenye vijiji (50m @) ni vyema ukatoa seed capital kuwezesha viwanda vidogo 6400 ambavyo vitaajiri wafanyakazi walau 10 kila kimoja lakini viwe ni import substitution, primary processing ya agro products for export mfano korosho, madini,nk
 
Frankly, Tanzania ya viwanda ni ngumu sana kwa mfumo huu.

Unapoongelea rasilimali watu ujue unaongelea skilled and unskilled labour.

Mfumo wa elimu ni mbovu (umekufa) hivyo skilled competent labour ni ngumu kupatikana sasa na pia huko mbeleni. Hii inaongeza gharama kwa kiwanda kuajiri skilled labour na kulipa bei kubwa (wachache waliopo ni ghali au waajiri nje ya nchi kwa gharama zaidi). Ni ndoto kuwaza viwanda kama kiwango cha elimu kinazidi kuporomoka.

Pili unskilled labour (vibarua) ni expensive. Nchi tunazoiga watu wanatumikishwa kwa ujira mdogo na tunaviona hivyo viwanda vyao tunavyotaka kuiga. Mfano, China, Indonesia, Vietnam etc. watu wanajiua kwa sababu ya kazi nyingi, ngumu, ujira mdogo na zero compliance to safety regulations. Huku, generally speaking, ni ngumu kupata vibarua wanaokubali mazingira hayo ya kazi.

Teknolojia pia ni tatizo. Teknolojia inaongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza gharama. Kwa sababu Serikali haijaweka kipaumbele katika R&D tunaona nchi haina ubunifu katika sekta ya teknolojia. Hivyo inabidi tu-import teknolojia na hii inaongeza gharama katika kiwanda pia.

Mikopo ya benki ipo katika riba kubwa inayomkimbiza mwekezaji. Mfano unataka kuagiza mashine kwa mkopo wa benki, utaona riba ni kubwa, pia kwa sababu mashine itahitaji repairs, spares nazo utaagiza nje kwa sababu hapa hamna. Hii inaongeza pia gharama.

Mfano mwingine ni gharama ya vitu kama umeme. Umeme pia ni tatizo. Gharama za umeme zipo juu. Unaweza ukaajiri watu kwa bei kubwa, ukanunua vifaa na mashine zako kwa bei kubwa na kwa mkopo na umeme usiwake kwa mwezi. Hiyo ni hasara!

Pia ili uwe na viwanda inabidi uwe na serikali rafiki na sekta binafsi na wakezaji (wa nje na ndani). Kwa miezi hii michache serikali imekua aggressive kiasi kwamba inatisha wawekezaji. Hapa hatujaongelea kodi kibao serikali hii inazotoza.

Hivyo kuendesha nchi kwa viwanda ni mfumo. Ni sera endelevu na huwezi kukurupuka na kuanza tu. Ni kuwa na sera bora katika elimu, ubunifu, sayansi na teknolojia, miundombinu n.k

skilled labour sio tatizo. Nchi hii inautaratibu mzuri usiofuatwa na kuwa audited au monitored. Tuna watu wengi wenye fani nyingi na uwezo mkubwa wasio na kazi ila hawajiamini na wengi tumechagua uzembe. Nchi kama singapole kutokana na shida hii, waziri wa kazi pamoja na wataalamu wao kuwepo, wanampango wa MAN POWER IMPORTATION. Unaingiza watu nchini waliohakikiwa uwezo wao, wanafanya kazi sehmu nyingi na hawa waswahili graduates, Skills and competency importation. Tatizo tulilo nalo Karibu 90% wanaojiita maexpert ni weupe,wasiojua vitu, wanaingia kiujanjaujanja, wachoyo wa maharifa, hakuna wakuwafuatilia uwezo na competency zao, wanaficha maalifa kutengeneza dependency na kutunza ajira zao. Dunia ina mamilioni ya watu wenye uwezo na nia ya kusaidia nchi masikini lakini tunajikuta tunaandaa ajira kwa wasio na ajira ulaya na asia badala ya watu wenye uwezo.

Mimi naamini watanzania wengi tuna uwezo mkubwa sana uliojificha katikati ya HOFU YA KUTHUBUTU, Kutoamini uwezo wetu, kukatishwa tamaa na watawala wanaojilimbikizia fursa na kujipendelea wao kwa kila kitu,kuamini kuwa bila mzungu hakiwezekani kitu,
Dawa ya hii kitu au ugonjwa ni ndogo sana, maana ni tatizo la kisaikolojia tu sio UWEZO. Napendekeza kuwe na halambee au vuguvugu kubwa nchi nzima mijini na vijijini, makanisani, misikitini, popote pale watu wajue. Huwezi kuwa na nchi ya viwanda bila kuwa na watu wanaoviona viwanda vichwani mwao. inaanzia akilini kwanza.

mfano:
Singapole hii kazi ilifanywa na Lee Kuan Yew kuanzia 1965, na Huyu akabadili taswira ya uchumi wa asia yote
China Deng Xioping 1978, baada ya kubadili Philosophy za kimasikini nchi nzima
Ulaya Magharibi na Marekani: Mapinduzi ya Viwanda Yalitanguliwa na Mapinduzi ya FIKRA (The age of enlightenment)
 
Sera ya matokeo makubwa sasa(BRN) ILIMSHINDA MTANGULIZI WA JPM... KAMA INGEFAA JPM ANGEIHUISHA UPYA ILI IENDANE SAMBAMBA NA MFUMO WA VIWANDA... EMBU ANGALIA MALAYSIA TULIPOCOPY HIYO BRN WAO WAKO WAPI KIUCHUMI...WAKO MBALI ZAIDI YETU..SHIDA MOJA TZ SIASA NYINGI, KUBEBANA KWINGI NK
nakubaliana na wewe. Tatizo letu sio sera ila wanaotekeleza hizo sera. Yawezekana JK alikuwa na maono mazuri ila wanayobeba hayo maono ni wezi,wafitini,mafisadi, wenye nia mbili na wabinafsi. Ili kuwapata hawa hakuna haja ya kutafuta maraika ni kufanya kinachofanyka sasa. Tunatumbua huku tunaplan na kuimpliment. Lakini taifa lazima liwe na Progression plan ya kuandaa kizazi adilifu kuliVusha katika stage mbalimbali linalopitia.
 
Kwanza tukiangalia sera ya viwanda vidogo na kati iko vizuri sana shida ni utekelezaji wake umekua shida.
Tuanze na SIDO imepewa mandate ya kusaidia wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati viweze kufanya primary and secondary processing. Mafunzo wanatoa kisha wanatekelezwa kwa maana mwenye wazo hasaidiwi vya kutosha kufikia uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda hivyo.
Wakati huo huo SIDO wamekuwa wakitoa mikopo kwa wajasiriamali hao kwa riba kubwa lakini core busiiness ya shirika sio kutoa mikopo bali kusaidia viwanda vidogo na kati na kama ni mikopo ilibidi itolewe kwa wajasiriamali wenye mawazo yanayotekelezeka.
Nini kifanyike rais magufuli alifumue shirika la umma sido lirudi kwenye core business yake, waanzishe viwanda vidogo, kukuza viwanda vido ili viwe vya kati na vya kati viwe vikubwa. Sido iondokane na mambo mengine yote badala yake kusaidia SMEs tu.

Ukuaji wa viwanda vidogo ndio msingi wa kukua kwa viwanda vya kati na vikubwa.

Sehemu ya kwanza inayoweza kufanya transfomation ya uchumi wa tanzania ni agro processing. Angalia tu muhogo technolojia ya kusindika haizidi 3million lakini bado watu wengi hawajaingia. Shida kubwa mitaji na pale inapopatikana riba kubwa.

Ianzishwe Industrial Derivery Unit (IDU), Itakayosimamia projects zote za startups na viwanda vya wazalendo na kutoa immediate assist in terms of marketing, linking to specific ministry, managing changes, linking government and owners, na kufanya nationa promotion ya hii kitu.
Watafutwe watu visionary Kuongoza vitu hivi nyeti, watakao endesha projects hizi kwa specific Time,cost,scope quality na guided by procedures.Sio lazima awe mtanzania, Duniani wako watu wengi ambao ni solution ya matatizo yetu. kama tunania ya Speed na Accuracy.

Viongozi wote kwenye ngazi za maamuzi (wenyeviti wa vijiji,mameya, wakuu wa mikoa,wilaya, mawzili etc) lazima wawe na angalau elimu ya Technology, Management na Entrepreneuship. Sio lazima ya chuo Serikali iandae special TAilored short courses au itafute consultants hawa watu waoshwe bongo ziendane na kule nchi inakoelekea. Haiwezekani kuongoza watu wako ukiwa Shallow au uninformed kuhusu kitu unachotaka waproduce mwisho wa siku.
 
Siaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasa. Tangu wameshika hatamu wameshindwa kupiga maarufuku hata toothpick na pamba za masikio kuagizwa kutoka nnje ,wakat pamba twalima wenyewe na miti ya kutengenezea toothpick tunayo.
 
Ilipaswa kuwa na faida kubwa sana nchi hii kuongozwa na chama kimoja kama China,Singapore etc, badala yake pamekuwa hakuna leadership na continuity ya progressive plan. Nyerere aliondoka na yake, mwinyi, mkapa,jk. Tunawaheshimu kwa kulisimamia taifa ila pia nao walikuwa na mapungufu yao. Sasa jpm anapaswa kuweka basement ya uhakika kama sio walewale.

Mfano: kipande kidogo tu cha gogo, kunitoa maelfu na malaki ya stick.
Angalia hapa chini mchakato mzima
 
Tunatoka katika KILIMO KWANZA japo bado hatujafanikiwa sana, Tunaelekea TANZANIA YA VIWANDA.

Hii ni kitu ninayoiunga mkono 100%. Ni aibu kuimport nguo za mitumba,stick,maziwa ya unga, vyuma,Furniture, na bidhaa kibao huku tuna rasilimali watu,chuma (madini,), makaa ya mawe, mazao ya kilimo na vitu vingi ya kututoa huko.

Unadhani Rais JPM afanye nini ili Mapinduzi ya Viwanda Tanzania yawe halisi. Je unaona spidi hii iko sawa?Watu wamjiandaa kufungua viwanda hata vidogo?Je watu wako tayari kununua bidhaa za ndani? Miundo mbinu na masoko yanaandaliwa kwa kasi inayotakiwa?

unaweza ongeza dhamani kwa taifa kwa kutoa suluisho au nini kifanyike ili mpando hii uwe halisi kwa kila mtanzania.
Tatizo tulilonalo ni kukubali kuongozwa na wanasiasa. Nawaambia ukweli. Hatutatoka hapa tulipo kama hatutampata mtu ambaye yeye hafikilii siasa bali anafikiria nchi na maendeleo kwa ujumla. Yaani mtu ambaye kichwa chake hakitasema huyu ni ccm wala huyu ni chadema. Bali atajari uzoefu na ujuzi wa huyo mtu kumuweka kwenye sekta inayofaa. Yaani tumpate mtu ambaye yeye yupo tayar kukitoa sadaka chama chake cha siasa kwa sababu ya nchi hii. Na awe na maono sio mbwembwe wala ulaghai. Na pili awe tayari kushaurika. Hayo mambo mengine mnayoyasema ni simple tukimpata mtu wa hivi
 
Ilipaswa kuwa na faida kubwa sana nchi hii kuongozwa na chama kimoja kama China,Singapore etc, badala yake pamekuwa hakuna leadership na continuity ya progressive plan. Nyerere aliondoka na yake, mwinyi, mkapa,jk. Tunawaheshimu kwa kulisimamia taifa ila pia nao walikuwa na mapungufu yao. Sasa jpm anapaswa kuweka basement ya uhakika kama sio walewale.
Yani wangetumia hayo mabilioni wanayoyakusanya Sasa kwan nguvu kununulia haya mashine hizi tukaliteka soko LA east Africa ingekuwa poa sana

Mfano: kipande kidogo tu cha gogo, kunitoa maelfu na malaki ya stick.
Angalia hapa chini mchakato mzima
 
Tatizo tulilonalo ni kukubali kuongozwa na wanasiasa. Nawaambia ukweli. Hatutatoka hapa tulipo kama hatutampata mtu ambaye yeye hafikilii siasa bali anafikiria nchi na maendeleo kwa ujumla. Yaani mtu ambaye kichwa chake hakitasema huyu ni ccm wala huyu ni chadema. Bali atajari uzoefu na ujuzi wa huyo mtu kumuweka kwenye sekta inayofaa. Yaani tumpate mtu ambaye yeye yupo tayar kukitoa sadaka chama chake cha siasa kwa sababu ya nchi hii. Na awe na maono sio mbwembwe wala ulaghai. Na pili awe tayari kushaurika. Hayo mambo mengine mnayoyasema ni simple tukimpata mtu wa hivi
Uko vizuri
 
serikali ilibinafsisha baadhi ya viwanda na kujitoa ktk kuendesha viwanda kwa kuwaachia sekta binafsi.

tz ya viwanda itawezekana ikiwa serikali itataifisha baadhi ya viwanda na kurudi ktk umiliki wa serikali... lkn kikwazo ni usimamizi na ufisadi.
 
Unaweza pitia bamboo toothpick machine. Hii kwa mwenye uwezo unaimport alibaba. Na ni cheap.Mali ghafi ni Mianzi
Changamoto pia itakuwa gharama za uzalishaji kulinganisha na bei rahisi kbs ya hizi za kichina zilizofurika masokoni. Serikali bado inanafasi kubwa ya kumlea kwenye kiwanda mzawa mchanganyiko kwa kucontrol import na kuhakikishwa vitu tunavyoweza kutengeneza vinakuwa discouraged kwa hata kwa kuviongezea kodi
 
Attachments

  • 543431799_214.jpg
    543431799_214.jpg
    60.3 KB · Views: 92
Hapa tukutane watu wote wenye mawazo ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo
1:Wanafunzi wa Veta
2:Wanafunzi wa vyuo vya ufundi stadi
na wadau mbali mbali tupeane mawazo ya kuanzisha viwanda
 
Back
Top Bottom