Tanzania ya viwanda ni lini itafufufua kiwanda cha general tyre?

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,721
515
Pamoja na hamasa zote hizi....Nauliza kulikoni juu ya kufunguliwa tena kilichokuwa kiwanda cha general tyre???
 
Tanzania ya viwanda itakuwa hii hata kiwanda cha kutengeneza baiskeli za mkulima hawawezi shenzi type
Jambo moja linanitatiza, kama viwanda havijengwi, hili ni tatizo la nani? Serikali, CCM au sisi wananchi? Juu ya kufufua viwanda vilivyokuwepo hilo sina shaka serikali inawajibika 100%. Je sisi wananchi hatuna wajibu wa kuanzisha hivyo viwanda vipya? Au watanzania tunamjomba huko ughaibuni atakayetujengea viwanda? Nafikiri watanzania tunashida mahali!
 
Nafikiri Mzee unatatizo, Serikali jukumu lake sio kufufua wala Kujenga viwanda vipya. Serikali inatakiwa itengeze Policy itayowavutia wawekezaji.

Wewe unafikiri Nchi za Europe Kama Ujerumani wanafunga viwanda vyao na kujenga China kwa sababu gani?

1. Wamepewa Garantee ya Mtaji wao.

2. Wanapata chip labour ukilinganisha na Europe

3. Wanapata Malighafi kwa bei rafiki

Sasa Serikali ilikuwa ikae iweke mikakati, kwa wajiulize kwa mazingira yapi tunaweza kuyaweka tukawapiku Wachina?

Tatizo la pili za Serikali zetu hawelewi ni Kitu gani kinapatikana Nchini, na Kitu gani tuagize nje.

Utakuta waziri anayejiita Mzalendo, anatia sahihi mkataba wa kujenga hicho kiwanda, lakini wafnyakazi wote wanatoka nje ya nchi na Serikali inaangalia tu
 
Inategemea upande mmoja upo sawa,lakini unaposema wanainchi wajenge viwanda unamaanisha nini kweli...
 
Nafikiri Mzee unatatizo, Serikali jukumu lake sio kufufua wala Kujenga viwanda vipya. Serikali inatakiwa itengeze Policy itayowavutia wawekezaji.

Wewe unafikiri Nchi za Europe Kama Ujerumani wanafunga viwanda vyao na kujenga China kwa sababu gani?

1. Wamepewa Garantee ya Mtaji wao.

2. Wanapata chip labour ukilinganisha na Europe

3. Wanapata Malighafi kwa bei rafiki

Sasa Serikali ilikuwa ikae iweke mikakati, kwa wajiulize kwa mazingira yapi tunaweza kuyaweka tukawapiku Wachina?

Tatizo la pili za Serikali zetu hawelewi ni Kitu gani kinapatikana Nchini, na Kitu gani tuagize nje.

Utakuta waziri anayejiita Mzalendo, anatia sahihi mkataba wa kujenga hicho kiwanda, lakini wafnyakazi wote wanatoka nje ya nchi na Serikali inaangalia tu
Mkuu Mtambwe, nimekuelewa vizuri sana, na ulichosema kuhusu serikali kuweka mazingira wezeshi na rafiki ni jambo la msingi kabisa na nakuunga mkona mia kwa mia.
Ni kutokana na muktadha huo ndiyo maana nilisema kuwa sisi wananchi nafasi yetu ni ipi, maana tunalaumu sana, lakini sisi tunafanya nini? Serikali ni watu wanaotoka miongoni mwetu, wengi wanapata mamlaka waliyonayo toka kwetu wenyewe, mfano wabunge wanaopitisha sheria na bujeti ya taifa tunawahoji hayo?
Ukweli ni kuwa mazingira ya uwekezaji wa viwanda kwa wazawa ni magumu mno lakini pia kukaa na kufikiri serikali itabadilisha mambo bila sisi wananchi kudai mabadiliko, tutasubiri sana! Tuache kulalamika, tuchukue hatua sasa, wanasiasa wana ajenda zao tofauti hawata tusaidia sana.
Kama nawewe unatamani kuwa sehemu ya mabadiliko tuungane, sisi tumeshaanza kuchukuwa hatua, tafadhali tutembelee hapa ESTA -TANZANITE CITY OF TECHNOLOGY & INNOVATION: MBEYA tusaidiane; imoja ni nguvu!
 
Jk jana alisha waambia,ilani wameitengeneza lakini viongozi makini wa ssm wamekaa na wameona kuna mambo ya ziada ,kwahiyo hayo mambo ya ilani sijui irani.

Baadae hiyo.
 
Mkuu Mtambwe, nimekuelewa vizuri sana, na ulichosema kuhusu serikali kuweka mazingira wezeshi na rafiki ni jambo la msingi kabisa na nakuunga mkona mia kwa mia.
Ni kutokana na muktadha huo ndiyo maana nilisema kuwa sisi wananchi nafasi yetu ni ipi, maana tunalaumu sana, lakini sisi tunafanya nini? Serikali ni watu wanaotoka miongoni mwetu, wengi wanapata mamlaka waliyonayo toka kwetu wenyewe, mfano wabunge wanaopitisha sheria na bujeti ya taifa tunawahoji hayo?
Ukweli ni kuwa mazingira ya uwekezaji wa viwanda kwa wazawa ni magumu mno lakini pia kukaa na kufikiri serikali itabadilisha mambo bila sisi wananchi kudai mabadiliko, tutasubiri sana! Tuache kulalamika, tuchukue hatua sasa, wanasiasa wana ajenda zao tofauti hawata tusaidia sana.
Kama nawewe unatamani kuwa sehemu ya mabadiliko tuungane, sisi tumeshaanza kuchukuwa hatua, tafadhali tutembelee hapa ESTA -TANZANITE CITY OF TECHNOLOGY & INNOVATION: MBEYA tusaidiane; imoja ni nguvu!
Sasa nafikiri umeingia pale hasa nilipokuwa napataka. Umesemwa viongozi wote tunawachagua wenyewe nakubaliana na wewe 100%. Lakini suala la msingi ni kujiuliza ni Kiongozi ambaye Baada ya Kumchagua anawajibika tena kwetu sisi? Jibu ni kwamba hakuna.
Kwa hio muarubaini wa Matatizo yetu ni Katiba mpya. Katiba ambayo wananchi watakuwa na Mamlaka ya kuwawajibisha viongozi wao wakati wowote watatakapoona wametoka nje ya mategemeo yao.
Katiba Ambayo tutakuwa na Taasisi imara na sio One man Show.
Katiba ambayo itakuwa dira haijalishi chama kipi kitashika hatamu za dola.
Katiba ambayo itatenganisha mihimili yote ya dola bila mmoja kumuingilia mwenzake
Kinyume chake tunaota ndoto za Alinacha tu
 
Back
Top Bottom