KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 35,744
- 86,370
Sote twafahamu msingi wa taifa hili toka hapo awali nisingependa sana kugusia mambo ya kale japo vya kale ni dhahabu lakini kwa muktadha wa mada hii nitaangazia mambo ya sasa..
Si jambo geni ama la ajabu kuona migomo na maandamano katika taifa lolote lile lakini sikuzote jamii ndio hushawishi waongozwe vipi.! Ndio na wala si ajabu maana kuongoza watu hutegemea wana elimu kiasi gani, utendaji, umoja na ustaarabu wao upo katika stage gani.
Kwa uchache tu na ufupi jamii yetu ipo katika stage ya uchangamano!, yani kuna kizazi kinachohitaji mabadiliko na kile ambacho hakihitaji!.
Hivi vizazi vyote vipo sahihi aidha kutokana na uzoefu wa maisha,matarajio na vilevile kuridhika ama kutoridhika!.
Ila moja ya kitu ambacho saikolojia ya binadamu huwa inaogopa ni mabadiliko. Kuubadilisha mfumo uliopo huwa inawapa tabu sana hususani watu wenye hulka ya hofu na uoga!.
Jamii hii ndio ileile iliyoona na kuishi mabadiliko toka enzi za awamu ya kwanza mpaka hivi sasa, na jamii nyingine ni imeona nakuishi awamu kadhaa hapo nyuma.
Mitazamo ya hizi jamii lazima itakinzana katika namna moja ama nyingine kutokana na vile mahitaji ya wakati huu yanahitaji nini na nani hayahitaji!.
Wapo wanaomini kilimo ni bora na wapo wanaomini usanii, ama uanamitindo ama kuwa mwana Mitandao ni bora zaidi!.
Hawa wote wapo sahihi maana wapo katika wakati sahihi na vyote vinaweza kupatikana kwa wakati sahihi!.
Shida ya haya yanakuja hapa: SIASA na Wanasiasa ndio wanaweza kuyafanya haya yakawa matunda matamu ama machungu!.
Bila kuremba muandiko, taifa hili limekosa wanasiasa wenye maono na wanaoogopa mabadiliko!, wanaogopa aidha kwa tamaa ama ileile hulka ya kibinadamu ya uoga wa mabadiliko lakini kwenye hili hata mtoto anaweza kung'amua uoga wao ni juu ya nini!.
Kwani nani yupo tayari kuliachia pande la keki liende kwa mwingine..?
Hii imekuwa ni ndoto kwa wanaharakati kuona uongozi ukigawa keki ya taifa ipasavyo lakini si malaika ama shetani ameweza kuruhusu hilo!.
Kiongozi mwenye maono anafahamika na hupimwa kwa matendo yake!, ila huu mzani uliolegalega bado hausomi vyema ila nimegundua tatizo lilipo na wapi pakutatua!.
Jamii imekosa sauti moja hii ni kutokana na mkanganyiko ya wanaofaidi na wasiofaidi, wanaoiba na wasioiba n.k
Hoja dhaifu za kukimbilia zinaonyesha ufupi ama uhafifu wa akili za watu fulani fulani!..
Hoja haiwezi kuwa Dini ama muungano au kabila maana wanufaika wa maendeleo nchi huwa ni ya wote pasipo kuangalia tofauti yoyote ile, ila kwasababu wanajua mkikimbiziwa huko mtaogopa na kuifyata mikia yenu kama mbwa koko basi hiyo ndio fimbo yakuichalaza!.
Nanyi nani aliwaambia kwa vurugu nakuharibu vitu vya watu wakusadikika ndio mtapata haki yenu..?
Hii ni akili finyu ila ni alama ya utambulisho inayoitwa "kuchoka!".
Japo hii vita haikupaswa kuwa hivi hapo awali ila sauti tu ya umoja inaweza kutosha na kubadili historia! Ni zwazwa pekee anaeweza kuiamini katiba ya nchi yakusadikika!, lakini vipi ndugu zangu ndio huwa inaombwa hivyo...?
Mengi mtasikia, mtaona na kuyaishi lakini mchezo unaoitwa siasa unatakiwa uwe na akili ya moja kwenda na mbili!, hesabu hupigwa na kuchezewa; hivi ni vipaji vya watu japo kwa sasa ni vipaji vilivyochacha!.
Hivyo basi, badiliko la kweli litakuja pale mtakapokuwa na sauti moja, vilevile kubadili mifumo katika njia sahihi lakini kama mtakuwa na sauti kila mtu anaongea lakwakwe hapo hakuna kusikilizana!, ni kutoana meno na manundu tu!.
Hata hivyo nanyi upande wapili mmeshakuwa wazee wapeni vijana nafasi wasimamie mambo!, ushamba wakukatiana umeme, internet na kuchukuana bila ridhaa hizo ni karne za zamani. Watu hivi sasa hawahitaji tu barabara bali barabara bora, sio tu umeme bali wa uhakika maisha yasasa umeme ni uchumi, sio tu internet bali ya uhakika.
Msiwe waoga wa mabadiliko.