Tanzania ya Samia: Documentary Yaleta Mzozo

Tanzania ya Samia: Documentary Yaleta Mzozo

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Kesho, Agosti 27, macho ya Watanzania yatageukia ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambako kutafanyika uzinduzi wa “documentary” maalum iitwayo Tanzania ya Samia. Kazi ambayo imetangazwa rasmi na mtangazaji wa Clouds FM, Meena Ally, ambaye pia ni miongoni mwa waliopata nafasi ya kushiriki katika utayarishaji wa filamu hiyo.
1756227908512.jpg

Kwa mujibu wa Meena, Tanzania ya Samia inalenga kuonyesha mandhari na maendeleo ya Tanzania, hususan jijini Dar es Salaam. “Hii ilikuwa nafasi ya kipekee kwangu kujifunza, kushiriki, na kuona upekee wa nchi yetu kwa mtazamo tofauti,” alisema akizungumza na wanahabari. Aliongeza pia kuwa shukrani zake kubwa zimemwendea msanii na mchekeshaji maarufu, Idris Sultan, kwa kumpa fursa ya kuwa sehemu ya timu ya utengenezaji.
images (52).jpeg

Nimesikiliza wimbo wa Rostam leo nimebaki kucheka na kuona bado tuna safari ndefu sana, kila mtu anakuwa chawa ili kulinda mkate na ugali usije kuwa mgumu. Hivi karibu usishangae Meena akawa Mkuu wa Wilaya fulani kwa hili ambalo amelionesha. Lamba miguu ili upate nafasi ya kulamba asali.
 
Back
Top Bottom