Tanzania ya Magufuli Itakuwa ya Viwanda

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,192
1,972
Mpaka sasa hatujaona Kiwanda chochote kikianza kujengwa! Tunamwomba Mkubwa wetu aanze sasa juhudi za kujenga/kufufua Viwanda ili angalau tujiepushe kuwa Soko la Bidhaa toka nchi jirani, especially Kenya! Otherwise ahadi hii isije ikawa ni JIPU mwaka 2020!
 
Dunia ya sasa viwanda havijengwi Na serikali viwanda vinajengwa Na wawekezaji serikali inajenga viwanda vidogo.Serikali iboreshe mazingira ya kuwekaza ili wawekezaji wakubwa waje.
 
Hahahahahahahah mkuu jamaa anataka viwanda vinjengwe in six month makubwa hayo!but si mwijage kasema general tyre tayari inanza teh teh !!!
 
Nataka JPM aweke mpango mkakati wake w serikali....kujena viwanda na kuviendesha! Asije akajikuta anarudi kule kule! Aje na mpango wake aseme wapi na wapi atajenga na kama itakuwa serikali pekeyake au PPP! Zile ngonjera zake z jukwaani ndio tunataka ziw kweli! Pia ana mambo mengi aliahidi.....tunasubiri! Reli, Ndege, Viwanda na Meli! Asiwe kama Mfalme njozi alitoa ahadi hadi wapambe wakawa wanaona aibu! Kigoma kuwa dubai...sijui kwa maana gani ya biashara au majumba na maisha!!
 
!
!
Ingekuwa sio kosa ningesema ile ni ahadi ya bwege kwa wananchi vichaa. Selikali ya viwanda ni ndoto za mwendawazimu. Long live selikali ya viwanda vya majipu
 
Badala ya viwanda wamekuja wa Oman kupanda nyasi nchini kwetu wakalishe mifugo yako huko Oman, ardhi ikiisha rutuba ndio mitarudishwa kwa wananchi wapande mazao, viwanda watakuja wakati ng'ombe wao wameshiba wanataka kugeuzwa kitoweo watasindika nyama irudi oman kuliwa kwa ajira ya elfu 80 kwa mtanzania.
 
Huwezi kuzungumzia viwanda wakati kilimo kiko taabani. kilimo kiimarike tupate raw materials huko, ndiyo tufikirie viwanda tena vidogo na vya kati..
 
Huwezi kufikiria kujenga uchumi imara bila kujenga misingi ya maadili kwenye serikali , image ya nchi kwa mataifa ya nje na washirika ili wajue hawaji kuvuna tu ....ndio maana JPM hacheki na mtu kwasasa na ataumiza wengi hadi umma utapojua enzi za porojo na kuuza rasilimali za nchi imekwisha ....then akianza mikakati itakuwa na watekelezaji wenye adabu na hata washirika watakuja kwa adabu.....tunapojadili haya tusiwe wasahaulifu nchi yetu ilifikia hatua gani ....na mjue kuvunja hiyo mifumo si rahisi ....lakini walau in short term anaweza kupata pakuanzia .....huwezi kuiona pepo bila kufa kwanza ....tumpe muda tuache siasa ...
 
Mpaka sasa hatujaona Kiwanda chochote kikianza kujengwa! Tunamwomba Mkubwa wetu aanze sasa juhudi za kujenga/kufufua Viwanda ili angalau tujiepushe kuwa Soko la Bidhaa toka nchi jirani, especially Kenya! Otherwise ahadi hii isije ikawa ni JIPU mwaka 2020!
Mpeni muda Rais wenu its too early jamani
 
Pia tu subiri bajeti yake kwanza Maana huwezi kuona matokeo kwa muda wa miezi mitano tu aliyokaa madalakani hata kama angekuwa Malaika haiwezekan! Tumpe muda kwanza.
 
Mpaka sasa hatujaona Kiwanda chochote kikianza kujengwa! Tunamwomba Mkubwa wetu aanze sasa juhudi za kujenga/kufufua Viwanda ili angalau tujiepushe kuwa Soko la Bidhaa toka nchi jirani, especially Kenya! Otherwise ahadi hii isije ikawa ni JIPU mwaka 2020!
Heri ununulie mchina lakini si mkenya.ndoo maana rais wenu anatabia zenu za chuki zidi ya Kenya.
 
Haya ni maneno ya Raisi Magufuli kwenye hafla ya wazalishaji bora Viwandani!

"Nataka Nchi ya Viwanda halafu pawepo mtu anakwamisha ataondoka, nimezunguka nchi nzima nasema nataka nchi ya viwanda sikuwa kichaa,, - JPM
 
Back
Top Bottom