Tanzania ya leo na Mwenge wa uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ya leo na Mwenge wa uhuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jeff, Nov 8, 2011.

 1. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wana Jf,hiv kuna haja gani ya kuendeleza sherehe za kukimbiza mwenge mikoa yote hapa nchini tukitumia gharama kubwa,wakati kuna sekta muhimu zina bajeti finyu,sekta kadhaa za serikali hazijaajiri pesa hakuna,iweje pesa nyingi zitumike kwenye mbio za mwenge na wakati wananchi wana hal mbaya? Hili mnalionaje wanajf?
   
 2. l

  luckman JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Kwa bahati mbaya sana mi si muhumini wa utumiaji mbaya wa rasilimali za nchi, inawezekana lengo la mwalimu na timu yake lilikuwa sahihi soon after independence, ikiwa ni ishara kuwa sasa tuko huru!dhana na mantiki ya mwenge kwa miaka ya sitini na sabibi hadi themanini katikatika ilikuwa sawa lakini dhana ya sasa si dhana ya kuserve madhumuni ya mwenge!raiti tungekuwa na watu wenye uwezo wa kungamua mambo nadhani tungekaa chini, tukafanya kitu kinaitwa cost and benefit analyis then tukaja na jibu la kweli kama gharama tunayotumia kukimbiza mwenge nchi nzima ni sawa na faida tunayoipata.
  ,
  mwenge ulikutumika kuhimiza uzalendo, kuhimiza uwajibikaji, kueneza ujumbe juu ya athari za rushwa, lakini tunapokaa leo na kuhubiri mwenge mantiki yake ni nini make rushwa inaongezeka, ufisadi ndo wimbo na kanisa la matajiri kwa sasa wanaojiita wanasiasa ambao kipindi cha mwalimu ilikuwa ni ajabu kuona mwanasiasa ni tajiri, angalia uzalendo uko wapi?kila siku unashuka, angalia matumizi ya nchi yanakuwa makubwa kuliko mapato hadi tunakopa kulipa mishahara< mikataba ya nchi imekuwa siri kubwa hali wadau wa mikataba ni wananchi wenyewe!,
  ,.
  ubabe umeongezeka kodi zetu zinatumika na hakuna mtu anayeruhusiwa kuhoji, tumeona kwenye mtikisiko wa uchumi, ambao waziri wetu wa fedha bwa mkulo aliuhakikishia umma kuwa Tanzania hatutaathirika lakini kinachoendelea mi nadhani watanzania wanaweza kusema hata waliosoma political science wanalijua hili, ninachotaka kusema ni pale serikali ilitoa stimulus package kwa makampuni fulani ili yasifirisike lakini wabunge walipohoji serikali ilisema ni siri ingawa ni pesa za wanachi zilitumika!
  ,
  tunazo rekodi nyingi zinazoonesha kuwa hatuna haja ya kuendelea kuushikiria mwenge sema tungetafuta njia mbadala ya kufikisha ujumbe uliolengwa kusambazwa kwenye mbio za mwenge!kwani tuna wanafunzi wengi hawana madarasa ya kutosha, hamna walimu, hamna vitendea kazi, hamna madawati ya kutosha, hospitali nyingi na zahanati za serikali zimebaki na panadol, nadhani hii ni kukosa dira ya ukweli, tumekosa mtu wa kudefine njia sahihi ya nchi hii, tumebaki na wanafiki, wabinafsi, na mafisadi, waliona sifa za utawala 100% na kukosa sifa za uongozi 100%
  .
  tufike hatua tuamue wenyewe na tuseme kuwa tumechoka kuburuzwa na tumechoka na matumizi mamabya ya rasilimali za nchi hii!changa kimaendeleo ila kubwa kiumri.

  naomba niishie hapa.
   
 3. j

  jchakupewa Member

  #3
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  enzi za mwalimu mwenge ulikuwa sahihi. lakini kwa sasa unatumika kuibia fedha za walala hoi.
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni KAfara tupu humo!!
   
 5. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huu si mwenge wa uhuru bali mwenge wa udhuru. To hell with this torch. Ni ushenzi wa kawaida kwa sasa kuwasha kibatari mchana kweupe. Zama za mwenge ziliishapita. Kilichobaki ni zama za kibiriti kuwachoma mafisadi na watawala wababaishaji.
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mwenge ni uchawi na imani za kishirikina..sijawahi kushiriki na siwezi kushiriki..
   
 7. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  imekaa vizur sana,iangaliwe namna ingne ya kuenzi uhuru na sio kwa mtindo huo wa zamani kwenye dunia ya sasa
   
 8. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mi nadhani mwenge ungewekwa ndani ya nyumba ya makumbusho hapo DAR iwe moja ya kumbukumbu tuu tosha. Hii kuzungusha nchi nzima ni uwendawazimu maana ni ufujaji wa fedha za walipa kodi.
   
Loading...