Tanzania vs Marekani: Transition of Power

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Nasi inapaswa tujisifu.
Kwa miaka 55 sasa tumekuwa na smooth transition of power ambapo marais wetu kwa Amani kabisa wamekuwa wakirithishana madaraka.
hatujawahi kuwa na Rais mng'ang'ania madaraka na hili ni jambo la mfano wa kuigwa!
tuombe Mungu utamaduni huu uendelee kudumu daima milele!
ktk hili tuwapongeze wanasiasa wote walioshinda na kushindwa urais kwa kukubali kwao matokeo na kuendelea kuheshimu katiba ya Jamhuri ya Muungano!
Hakuna western media itakayotusifia, so inabidi tujisifu wenyewe!
Mungu ibariki Tanzania....
Mungu ibariki Africa!
 
Huwezi kusikia kauli za kibaguzi kama hizo US, ndio maana huwezi kufananisha TZ na US kwenye kupokezana madaraka ni sawa na Mbingu na Ardhi. Sisi bado tupo miaka 10000BC.


Ubaguzi upi hapo unaouengelea? Kwani siyo ukweli kwamba Wachaga ndiyo wanaoichukua CCM kuliko jamii yoyote ile JMTZ?
 
Wacha uongo wewe.Rais wa Nzanzibar alishindwa .lakini ameng'ang'ania maraka.Na huku bara Ccm ilishindwa lakini wamenga'ang'ania madaraka.Unajidanganya mwenyewe na mandondocha wenzio wa ccm.
 
Sawa. Kuna data zinazoonyesha hiyo % ya chukizo? na nikwanini kuna chukizo?


Matokeo ya Uchaguzi ndiyo data pekee, chadema imeshinda kwa kiasi Kikubwa uchagani tu, wkt CCM Tanzania nzima, hata Dar yenyewe mahali ambapo chadema imepata kura nyingi ni pale ambapo wenyeji wengi wa KLM wanaishi kama Kimara na Kibamba!!
 
Samahanii Mleta Mada...
Lakini Usifananishe Marekani na mambo ya kijinga..

Ujinga hufananishwa na ujinga mwingine uliopiga hatua chache...
 
Matokeo ya Uchaguzi ndiyo data pekee, chadema imeshinda kwa kiasi Kikubwa uchagani tu, wkt CCM Tanzania nzima, hata Dar yenyewe mahali ambapo chadema imepata kura nyingi ni pale ambapo wenyeji wengi wa KLM wanaishi kama Kimara na Kibamba!!
Hatari sana, kwahiyo wabunge wote na madiwani wa chadema wamechaguliwa/wameshinda kwa nguvu ya wachaga?
 
Hivi inawezekana nchi iliyoanza mambo ya democracy miaka ya 1800 kulinganisha nchi iliyoanza democracy 1992???? lakini ni wajibu wa aliyeshindwa kumuunga mkono aliyeshinda huku kwetu mtu akishindwa kitu atakacho sema uchaguzi si huru au nimeibiwa huko ndo kupongezana kwa viongozi wa Africa
 
Bila unafiki,hakuna mtanzania yeyote hapa nchini ama nje ya nchi anayeichukia CCM kama mimi.Hata akiwa ndg yang ni mwana ccm,kwa vile naichukia ccm hata yeye pia nitamchukia,Hata kama atagua siwezi mpa huduma maana yeye nahisi atakuwa na maisha bora kama ccm inavyo jitanabaisha.
Ukiangalia Marekani kila Rais anayetoka madarakani lazima awe amechoka mwili na wengi huonekana kuzeeka,hii ni tofauti na hapa kwetu ambapo wa kwetu huonekana kunawili na kuwa kama vijana
 
Hatari sana, kwahiyo wabunge wote na madiwani wa chadema wamechaguliwa/wameshinda kwa nguvu ya wachaga?


Kwa kiasi fulani naweza kusema ndiyo, kwani Wabunge wa Upinzani wengi wameshinda Mijini na huko ndiko watu wa KLM walikojaa, angalia Kimara na Kibamba huko kashinda Mnyika, ngoja nikuulize unafikiri ilikuwa ni bahati mbaya Mnyika kwenda kugombea Kimara na Kibamba badala ya Ubungo?
 
Sasa ccm udikteta wao wakubadilisha MTU tu ila chama kile kile ulitaka wagomee madarakani ili iweje?
 
Back
Top Bottom