Tanzania tuwe na Tume huru ya Uchaguzi

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,980
Points
2,000

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,980 2,000
Imenishangaza mpaka sasa hasa wapinzani hawajadai tume huru ya uchaguzi. Hii haitakuwa nzuri kwa taifa tujiandae muhula wa pili kuwa mgumu kwa Magu. Kwanza kwasababu ya kutokuwa na tume huru jumuia za kimataifa zitatugomea kwenye mambo mengi. Pili pesa za watalii zitapungua kwa chaguzi za kenya na Tanzania kutisha wageni. Tatu CCM wataanza groups za kuwa Raisi ajaye. Vilevile kama kawaida Zanzibar kutaibiwa kura na kuleta majanga kule.
Hivyo kwa mnao ona mbali hasa CCM jueni tume huru itawasaidia kwa mengi.Bila hivyo mtawapa upinzani nguvu maana malalamiko yao kila mtu ataona wazi
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Messages
25,167
Points
2,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined May 27, 2014
25,167 2,000
Imenishangaza mpaka sasa hasa wapinzani hawajadai tume huru ya uchaguzi. Hii haitakuwa nzuri kwa taifa tujiandae muhula wa pili kuwa mgumu kwa Magu. Kwanza kwasababu ya kutokuwa na tume huru jumuia za kimataifa zitatugomea kwenye mambo mengi. Pili pesa za watalii zitapungua kwa chaguzi za kenya na Tanzania kutisha wageni. Tatu CCM wataanza groups za kuwa Raisi ajaye. Vilevile kama kawaida Zanzibar kutaibiwa kura na kuleta majanga kule.
Hivyo kwa mnao ona mbali hasa CCM jueni tume huru itawasaidia kwa mengi.Bila hivyo mtawapa upinzani nguvu maana malalamiko yao kila mtu ataona wazi
UKAWA walikimbia bunge la katiba na kutukosesha mengi mazuri!
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,865
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,865 2,000
Imenishangaza mpaka sasa hasa wapinzani hawajadai tume huru ya uchaguzi.
Hivyo kwa mnao ona mbali hasa CCM jueni tume huru itawasaidia kwa mengi.Bila hivyo mtawapa upinzani nguvu maana malalamiko yao kila mtu ataona wazi
Mkuu Kamundu, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Uchaguzi NEC ni tume huru, sema tuu sio Shirikishi.
Uhuru wa Tume ya Uchaguzi ni kama uhuru wa mahakama, uhuru wa Bunge, uhuru wa CAG, DPP, Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Tume ya Maadili etc.
P
 
Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,980
Points
2,000

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,980 2,000
Mkuu Kamundu, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Uchaguzi NEC ni tume huru, sema tuu sio Shirikishi.
Uhuru wa Tume ya Uchaguzi ni kama uhuru wa mahakama, uhuru wa Bunge, uhuru wa CAG, DPP, Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Tume ya Maadili etc.
P
Tumehuru nayosema ni vyama vyote vihusishwe maana tofauti na mahakama hii tume inashigjulikia siasa na huwezi kuweka siasa huru kama chama kimoja ndiyo kinateuwa viongozi. Mimi naona tupinguze maneno, kuoneana, na mengine mengi. Lakini kikubwa Magu aelewe bila hili muhula wa pili hautakuwa umetulia kutakuwa na majanga na ndama kila siku. Magu asipokuwa makini ataondoka na kutuachia dikteta kitu ambacho sijui kama watu wanajua hilo maana kama bunge litakuwa weak tunategemea nini na Nyerere alishasema.
 
Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
6,181
Points
2,000

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
6,181 2,000
Mkuu Kamundu, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Uchaguzi NEC ni tume huru, sema tuu sio Shirikishi.
Uhuru wa Tume ya Uchaguzi ni kama uhuru wa mahakama, uhuru wa Bunge, uhuru wa CAG, DPP, Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Tume ya Maadili etc.
P
Hata Musiba anaamini kuwa ni mwanaharakati huru-je ni kweli hiyo? Katiba inasema tuwajamaa-je ni kweli hiyo. Katiba ya Zanzibar inasema Tanzania ina nchi mbili-je ni kweli hiyo. Nina hakika kuna vigezo vya kuifanya tume iwe tume huru kimaandishi na pia kimatendo. Kwa matendo yao je una amini wao kweli ni tume huru? Hati kule Korogwe vyama vitano vya upinzani kwa masaa takribani matano vilishindwa kujua fomu za wagombea wao warudishe ofisi gani(Boma la Korogwe lina majengo makubwa mawili tu) halafu tume inayo ongozwa na JAJI na DOKITA (PhD) ina amini kuwa wapinzani walishindwa kurudisha fomu hivyo mgombea wa CCM kapita bila kupingwa. HATUNA TUME HURU kwa maandishi na kwa matendo.
Lakini la msingi ni kuwa na katiba inayozingatia kuwa Tanzania ni chi ya vyama vingi, na katiba hiyo idhibiti nguvu za raisi ambazo kama mwalimu alivyosema na kama tuonavyo sasa, inamruhusu raisi kuwa dictator. Na kwa Tanzania hii inatokana na UCHAMADOLA wa CCM na usingizi wa Kondoo wa Nyerere.
 
Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
6,181
Points
2,000

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
6,181 2,000
UKAWA walikimbia bunge la katiba na kutukosesha mengi mazuri!
Hata roho na dhamira yako itakuwa inakusita. Muulize JK alichofanya (kutusaliti) na pia msikilize Kabudu na Polepole wa enzi hizo. CCM Chamadola kilipata mchecheto kikaharibu mchakato. Kumuka yule mama (RIP) aliyesema serikali haipatikani kwa vikaratasi. Na kweli CCM wakamuibua Jecha tukaona kura zetu zikipoteza maana. Hati chaguzi ya raisi JMT iko sawa na ule wa Raisi wa SMZ unakasoro vituo karibu vyote Zanzibar. Hawa ni wa kupelekwa SHENZISTAN wakaishi huko.
 
yomboo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2015
Messages
5,993
Points
2,000

yomboo

JF-Expert Member
Joined May 9, 2015
5,993 2,000
Mkuu Kamundu, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Uchaguzi NEC ni tume huru, sema tuu sio Shirikishi.
Uhuru wa Tume ya Uchaguzi ni kama uhuru wa mahakama, uhuru wa Bunge, uhuru wa CAG, DPP, Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Tume ya Maadili etc.
P
Mzee wa 0
 
Mr Tyang

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2018
Messages
412
Points
500

Mr Tyang

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2018
412 500
Mkuu Kama unataka Tume huru.. Anza kuweka usawa kwenye familia yako kwanza Uache Mfumo dume Yani hata wewe uingie kwenye Zamu ya kupika na kuinama kupiga nyumba deki.

Kama Ukiona huwezi Fanya hivyo Basi jua hata hiyo Tume huru unayoidai haiwezi kupatikana.

Note; Nimeandika huu ujumbe kwa Lugha ya fasihi kwahiyo Kama wewe Ni kichwa nyumbu usihangaike hata kunielewa Ila kwa Great Thinker wanajua Nini Namaanisha.
"TUME HURU NI MUHIMU NA NDO SULUHISHO LA DEMOKRASIA YA KWELI."
 
Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
4,593
Points
2,000

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
4,593 2,000
Mkuu Kamundu, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Uchaguzi NEC ni tume huru, sema tuu sio Shirikishi.
Uhuru wa Tume ya Uchaguzi ni kama uhuru wa mahakama, uhuru wa Bunge, uhuru wa CAG, DPP, Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Tume ya Maadili etc.
P
Uwe unamuogopa na Mungu leo jumapili, hivi tume ya haki na madaraka ya bunge walikupa masharti gani naona toka uhojiwe umekuwa mtu wa kumpamba Zimwingara aonekane malaika.
 
DiasporaUSA

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Messages
20,239
Points
2,000

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2016
20,239 2,000
Imenishangaza mpaka sasa hasa wapinzani hawajadai tume huru ya uchaguzi. Hii haitakuwa nzuri kwa taifa tujiandae muhula wa pili kuwa mgumu kwa Magu. Kwanza kwasababu ya kutokuwa na tume huru jumuia za kimataifa zitatugomea kwenye mambo mengi. Pili pesa za watalii zitapungua kwa chaguzi za kenya na Tanzania kutisha wageni. Tatu CCM wataanza groups za kuwa Raisi ajaye. Vilevile kama kawaida Zanzibar kutaibiwa kura na kuleta majanga kule.
Hivyo kwa mnao ona mbali hasa CCM jueni tume huru itawasaidia kwa mengi.Bila hivyo mtawapa upinzani nguvu maana malalamiko yao kila mtu ataona wazi
Tukiwa na tume huru CCM itakufa kifo cha mende saa 1 asubuhi kwenye siku ya uchaguzi.
 
iMind

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Messages
2,108
Points
2,000

iMind

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2011
2,108 2,000
1. Tume huru imekuwa ikidaiwa hata kabla ya ukawa. Agenda moja wapo ya vyama vya upinzani siku zote tangu kuanzishwa kwake kumekuwa ni tume huru ya uchaguzi. Hivyo si kweli kusema kwamba wapinzani hawajawahi kudai.

2. Uhuru wa tume ni dhana tu. Hata tume ya sasa hivi ni huru vile vile. Ila kinacho kosekana ni dhamira na utashi wa uhuru na kutenda haki, miongoni mwa waliochaguliwa kuunda tume. Kwa kuzingatia tabia ya jamii yetu...ya kinafiki na kutanguliza matumbo mbele...sina uhakika hata kama wapinzani watashirikishwa kwenye tume, kuna jipya la maana laweza kutokea.

3. Tumekuwa hatuna tume jumuishi miaka yote lakini misaada imekuwa ikitoleaa kama kawaida. Misaada itaendelea kuwepo kama kawaida.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,587
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,587 2,000
Kenya wana hiyo mnayoita ,,Tume Huru” lkn Upinzani waligomea matokeo ya Uchaguzi walikataa kushindwa, tena wakaikataa ,,Tume Huru” ambayo walishiriki kuiunda, wakasema haiko huru.

Hivyo ,,Tume Huru” ni myth!
 
Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2009
Messages
3,493
Points
1,500

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2009
3,493 1,500
Mkuu Kamundu, kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Tume ya Uchaguzi NEC ni tume huru, sema tuu sio Shirikishi.
Uhuru wa Tume ya Uchaguzi ni kama uhuru wa mahakama, uhuru wa Bunge, uhuru wa CAG, DPP, Takukuru, Tume ya Haki za Binadamu, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Tume ya Maadili etc.
P
Kitu/vitu gani vinakufanya udhani na kuamini kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni tume huru kitaasisi, uoatakanaji wa wajumbe na wafanyakazi ???
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Messages
32,865
Points
2,000

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined Sep 22, 2008
32,865 2,000
Kitu/vitu gani vinakufanya udhani na kuamini kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni tume huru kitaasisi, uoatakanaji wa wajumbe na wafanyakazi ???
Sheria inayounda Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ni Tume huru, an independent institution ambayo haipaswi kuingiliwa na yeyote kama lilivyo Bunge, Mahakama, Ofisi ya CAG, Tume ya Haki za binaadam na Utawala Bora, ofisi ya DPP, Takukuru etc. Taasisi zote hizi watendaji wakuu wanateuliwa na rais.

Kama tumeikubali Mahakama kuwa iko huru, na NEC pia iko huru!.

Kitu nilichosema kuhusu NEC, kwa vile uchaguzi unahusisha vyama vingi, then NEC should be inclusive.

The electro process zina guarantee uchaguzi huru na wa haki. Ila our electoral law is a bad law na hili tumelizungumza sana humu.
P
 
Forum statistics

Threads 1,380,080
Members 525,684
Posts 33,764,899
Top