Tanzania tusahau kuhusu maendeleo ya kweli kama haya yataendelea

mululu

JF-Expert Member
Nov 7, 2014
749
406
1. #Kwa kuendelea kuamini woooote wanaompongeza rais ndio wazalendo na wanalipenda taifa na woote wanaopinga mwenendo Wa serikali ni WAHAINI wasariti na hawalipendi taifa hivyo wasakwe popote walipo na kuuliwa.

Mm nikiamini kilimo ndicho kitatutoa haraka kimaendeleo anayeamini Utalii ndio suruhu isiwe sababu mm kumsaka huyo popote alipo na kumsweka ndani. Asikilizwe pengine pana ukweli juu ya anachoamini yeye. Jimbo au kata iliyoshikiliwa na Chama cha upinzani kuna mkakati wa KULIKOMBOA kwani limetekwa na nchi gani? Anayelitawala sio mtanzania?, daah

2.#Kwa kuendelea kuamini ni MTU pekee ndiye atatuongoza vzr na sio Taasisi imara!!

Tanzania liinji likubwa sana na pia idadi ya watu inaongezeka kwa kasi ni lazima tuhame badala ya kuachia kichwa na fikra za MTU mmoja kumanage eneo hili lote na idadi hii kubwa ya watu tujenge taasisi imara na huru zitatusaidia sanaaa. Hakuna aliyezaliwa MKAMILIFU kuweka mihimili ya serikali ya bunge na mahakama ilikuwa ni kwaajili ya kukamilisha mapungufu ya huyu mtu aitwaye prezdaaa, zikigeuka kuwa taasisi za kupongeza tu na sio kumuonesha wapi anafeli na apazibiti vp ni kumpoteza rais na nchi kwa ujumla

3. #Kwa kuendelea na siasa za sasa ambazo zimejaa mikakati ya ushindi badala ya mikakati ya kisera.

Mwaka huu ni uchaguz wa serikali za mitaa ukiwaulza wenye nia ya kugombea ni ngumu kumpata mwenye sera za nn atakifanyia kijj ila ni rahisi kumkuta amejaza mikakati n vp atashinda. Yaani piga hapa bonyeza pale mgodi wa kura unatema nashinda!! Ok sawa baada ya kushinda nn unaenda kuwatendea watu??

4.#Kwa kuendelea kukumbatia mfumo wa sasa wa elimu ya kikoloni kujibu mitihani kwa kiingereza huku mwanafunzi akivuta kumbukumbu kwa KISWAHILI.

Hakuna tena ubishi kiswahili kimeshajiunga kwenye jumuiya ya lugha za kimataifa, kuendelea kukionea aibu ni kujipoteza sisi wenyewe na tusipojiangalia majirani watatupokea jukumu la kukirea. Halafu kuendelea kumpima msomi kwamba ni anayezungumza kiingereza ni urongo na upotofu mkubwa.

5.#Kwa kuendelea kuamini mfumo wa sasa wa kilimo utachangia katika uchumi endelevu.

Kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kilimo na ufugaji kama sekta kuu ya uchumi ipo hatarini pengine kuliko zote. Pembejeo za kisasa, ruzuku maghara ya mikoa mabwawa na visima vya umwagiliaji masoko ya mazao na elimu ya haraka kwa wakulima juu ya mabadiliko ya tabia nchi na matumizi ya mbegu bora ndivyo pekee vingesaidia kuinua sekta.

Ahsanteni....
 
Maada kama hizi hutakuta watu.


Shida kubwa nchi yetu tuliikomboa kutoka kwa mkoloni mweupe, tukasahau kaobdoka yeye kaucha ukoloni utakaofanya na mkoloni mweusi
 
Back
Top Bottom