Tanzania tunayoitaka na 2015

tafakari kali

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
211
39
Imebaki miaka karibu miaka 2 na miezi 2 hv ili kifike kile kipindi cha kupiga kura na kuchagua chama kitakachotuongoza kwa kipindi cha miaka 5 baadae. nimesema kuchagua CHAMA kwa kuwa kwa mujibu wa katiba yetu hivi sasa hairuhusu kuwepo kwa mgombea binafsi hivyo kama hili alitokuwa na mabadiliko katika katiba ambayo sasa watanzania tunatarajia kuiunda basi ni hakika kuwa katika uchaguzi huo tunachagua chama ambacho kimsingi ndicho kitakochounda serikali.

SWALI. CHAMA GANI AMBACHO TUNAENDA KUKIPA MAMLAKA YA KUTUONGOZA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 5 BAADA YA 2015? Je, ni hiki hiki ambacho serikali yake imejaa wala rushwa ambao kimsingi hawana uchungu na nchi hii?
Je, ni chama cha hawa ambao wamenunua rada kwa bei ya juu na mwanasheria wao(A.CHENGE) alipitisha mkataba huo kwa maslahi yake binafsi? hawa hawa ambao mwana jamii wao mmoja alijipatia mapesa kibao na kuyaita vijisenti?
Ni chama hiki ambacho chaguzi zake za ndani zinanuka kwa rushwa? ni hiki ambacho watu wake wanasafirisha wanyama kama twiga kwenda nje ya nchi? hawa amabao watendaji wake wakiaribu wanaamishiwa kitengo kingine?
hawa ambao watoto wao wanapita bila kupingwa na wake zao? hawa ambao watoto zao wamejaza B.O.T na mizani?.
madudu yao yanatia hasira sana ni vigumu kuweza kuhesabu makosa yao ni mengi mno.

Napenda ikumbukwe kuwa kabla ya uhuru yani miaka ya 1950s uchumu wa Tanganyika( jina ambalo viongozi wanapata kigugumizi kulitaja) ulikuwa sawa na nchi kama CHINA,KOREA KUS/KAZ na INDIA lakini sasa hatua ubavu hata wa kuwakaribia. TATIZO NI CHAMA CHA CCM NA WATU WAKE.

HAPANA HATUWATAKI HAWA (CCM)hawa jamaa wa ccm hatuwaitaji,hatuwataki kuwaona na kuwasikia. TUNATAKA CHAMA AMBACHO KIMSINGI KINAELEWA MATATIZO YA WATANZANI KUWA SI UPEPO WA KISIASA KAMA WALIVYOZOEA KUSEMA,HATUTAKI WATU WA KUTOA MAJIBU MEPESI KWA ISSUE ZA MSINGI NA NZITO.
KWETU WATANZANIA CHAMA MBADALA NA CHAMA SAHIHI NI CHADEMA SI KWA SABABU WANAUPAKO WA KIMUNGU LA HASHA ILA KWA KUWA WANAONEKANA WANAO UWEZO UCHUNGU NA NIA YA DHATI YA KUTUTOA HAPA TULIPO NA KUTUPELEKA MBELE ZAIDI,NA PIA WATANZANIA TUNATAKA KUJENGA UTAMADUNI WA KUBADILISHA VIONGOZ KILA TUNAPOHISI KUWA HAWAFANYI KAMA TUNAVYOTARAJIA,HUU NDIO MTAZAMO WETU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom