Tanzania tunamuhitaji Rais wa aina gani 2025? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunamuhitaji Rais wa aina gani 2025?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by FisadiKuu, Feb 22, 2018.

 1. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Habarini za Asubuhi wanabodi..

  Uzi huu niuandika baada ya kusikiliza kupindi cha Straight Talk Afrika cha Shaka. Jana walikuwa wanaongelea siasa za Afrika Kusini na Cyril Ramaphosa. Binafsi sikuwa namjua Cyril vizuri mpaka alipokwaa madaraka kutoka kwa Zuma. Hapo ndipo nilishawishika kutafuta na kuusoma wasifu wake. Ukiacha mengine mengi, he is a purely businessman.

  Tanzania tuna mipango na matazamio mengi mbeleni, tunaitaka Tanzania ya viwanda na ifikapo 2025 tunatazamiwa kuwa nchi yenye uchumi wa kati (Second world country).

  Binafsi siamini kama hawa walioko madarakani sasahivi watatufikisha kwenye hata moja kati ya hayo mawili. Kufika huko hatuhitaji kauli za kibabe, sera zisizoeleweka za kuwakandamiza wawekezaji, kujifungia ndani tukiwasubiri mpaka wao waje.

  Serikali yetu ya sasa labda inafanya mazuri kwenye baadhi ya mambo ambayo kiukweli ni machache na yanahesabika. Serikali ya sasa imejaa wanataaluma ambao kiukweli hawana background yeyote kiuongozi hasahasa kibiashara zaidi ya kuwa wakufunzi tu.

  Mambo mengi yanakwama, viwanda tulivyohaidiwa hatuvioni vinavyofunguliwa vingi kama sio vyote vilikuwa initiated wakati wa Kikwete, wakati huo ilikuwa rahisi kushawishi wawekezaji sababu purchasing power ilikuwepo, hali ya fedha kwenye mzunguko ilikuwa nzuri. Ila sasa, ni wenyewe tu ndio wanajua wanachofanya.

  Tukirudi kwenye mada kuu, Je, kwa hapa tulipo na huu mkwamo tunaoupitia bila shaka kwanza tunahitaji Rais msomi lakini pia Rais ambaye amebobea kwenye masuala ya kibiashara.

  Hapa haraka lilinijia jina la ALI MAFURUKI. Kwa kiasi kikubwa naona Mtanzania huyu anaweza kutupeleka kule tunakotaka kwenda. Huyu amekulia kwenye buashara na anajua biashara haitaki ubabe, biashara yeyote duniani inataka NEGOTIATIONS, biashara haitaki two faced people. Kwamba leo tunaongea hiki alafu kesho tunageuka.

  Kwa mtizamo wako; nani unaona atafaa kuwa mrithi wa JPM?
   
 2. GENTAMYCINE

  GENTAMYCINE JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2018
  Joined: Jul 13, 2013
  Messages: 27,704
  Likes Received: 31,875
  Trophy Points: 280
  Ambaye atakuwa ' Mkali ' zaidi ya ulivyo ' Upole ' wa sasa wa Rais na Amiri Jeshi Dr. Magufuli.
   
 3. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Unaweza ukapanga 2025, ikifika unakuta jamaa anajiingezea muda.
   
 4. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2018
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,659
  Likes Received: 4,228
  Trophy Points: 280
  Rais yeyote ajaye ni mbaya kuliko JPM Kama ambavyo watangaluzi wake walivyokua wabaya kulinganisha na watangaluzi wao.

  Kutokuridhika ni hulka ya mwanadamu.
   
 5. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Hilo pekee ndio hataweza..
   
 6. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Hatujadili mihemko na hearsay.. Tujadili content mkuu. Ni rais gani atatufaa tunapoitafuta Tanzania ya viwanda na nchi ya kupato cha kati?

  Kipato cha kati hakiletwi kwa kelele, tunahitaji biashara zishamiri. Sasa kama tunaua biashara, makusanyo ya kodi ni hadithi tunawezaje kufika huko?
   
 7. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  Kuna wapiga debe wake wapo, wanalipiga kwa mbali
   
 8. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2018
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,659
  Likes Received: 4,228
  Trophy Points: 280
  Hata Malaika ashuke kuwa Rais bado atakua mbaya kuliko JPM. It's that simple
   
 9. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Anaweza fanikisha vingi ila hilo hataweza
   
 10. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2018
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  kwann uongelee 2025 wakati uchaguz ni 2020??
  so huyu amepita bila kupingwa???

  lakn nauliza haya huku nikijua akiwa hai hakuna wa kumtoa hata wampe kula watu wawiliatasema wenipa wote!!
   
 11. forumyangu

  forumyangu JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2018
  Joined: Dec 25, 2016
  Messages: 1,718
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  Kwanza lazima utambuwe watanzania wengi ni vigeugeu just remember Kabla ya uchaguzi wengi wa watu walipendekeza/walipendelea tupate rais mkali na mwenye msimamo thabiti lakini leo wanakengeuka.
  Back to the topic~Tanzania inahitaji rais mwenye msimamo kama jpm lakini awe na mtizamo mbali na jpm.Kuwa na rais mfanyabiashara sio case sana lakini kama hana uzalendo ni kazi bure/debe tupu.
  Kwa tulipofikia sasa tunahitaji rais ambaye ni mwana falsafa.
   
 12. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Kwenye ukuaji wowote lazima uwe na tamaa ya kila jambo. Kama nchi bado tunakuwa, tulimuhitaji mkali tukasema hata akiwa dikteta potelea mbali. Sasa tumeona, na nadhani hilo halitajirudia kamwe..
   
 13. Lyamber

  Lyamber JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2018
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,846
  Likes Received: 3,946
  Trophy Points: 280
  Raisi design ya Kikwete au kama vipi kikwete ahamie Chadema agombee uprezidaa tuu
   
 14. KORBOTO

  KORBOTO JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 14, 2014
  Messages: 1,560
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Huyu Tuliye naye hatufiki naye 2020
   
 15. C

  CWR2016 JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2018
  Joined: Dec 14, 2017
  Messages: 1,618
  Likes Received: 2,618
  Trophy Points: 280
  Hivi unajielewa wewe?!!!. Unazungumzia 2025 wkt tunampiga chini 2020. Acha kutujaribu kisaikolojia. Koma kutuletea mawazo ya kututeka...
   
 16. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2018
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,326
  Likes Received: 2,195
  Trophy Points: 280
  Awe nusu kama kikwete na nusu kama magufuli
   
 17. Professor kipuyuyu

  Professor kipuyuyu Member

  #17
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 11, 2018
  Messages: 18
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 5
  Asiwe Mtoa Roho na akubali ye ni binadamu anakosea
   
 18. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 687
  Likes Received: 383
  Trophy Points: 80

  Salama!
  Watanzania waulize hawapendi nini, hapo utapata majibu hata page 30 lakini ukiwauliza wanapenda nini hautakaa upate majibu yaliyosahihi.

  Ni kama wewe mwandishi ulivyosema hapo kwamba tumejifungia ndani kusubiri wawekezaji waje badala ya kuwafwata huko waliko. Miaka mitano nyuma ninyi wenyewe mlikuwa mnalalamika hapa kwamba rais kikwete anasafiri sana mara oh hatulii nyumbani mpaka kumbatiza majina ya ajabu mzee yule.

  Leo hii tunakiongozi ambaye anafanya mnayoyataka ninyi watanzania lakini bado mnalalama kwamba rais anajifungia ndani hatafuti wawekezaji. Ndugu ukiwa na mali yako unaiuza mteja hawezi kukupangia bei na majira ya kuiuza hiyo mali. kama utaruhusu mteja apange bei na majira ya kununua hiyo mali yako basi andika umeumia na maumivu yake hautayaona leo ila baadae sana.

  Maendeleo tuliokuwa tunayalilia kila siku yana gharama yake mkuu, maendeleo hayaji kama ghafla bin vuu. Ili tufikie hayo maendeleo ni lazima tutoke jasho, tule sana mboga za majani, tushone viraka vya kutosha ili kufikia dhumuni kuu ambalo ni maendeleo. Viwanda vingi sana vinajengwa mkoa wa pwani hasa bagamoyo na kwingineko, tembea uone nchi inavyobadirika. Huwezi kuona mabadiriko ya nchi ukiwa umekaa sehemu moja, waulize ambao wako pembezoni mwa nchi watakwambia Tanzania wanaionaje?.

  Hii purchasing power unayoizungumzia hapa mkuu ni ipi? ni purchasing power kwa serikali au kwa raia? kama ni kwa raia , ndiyo raia tulikuwa na pesa nyingi sana mikononi ambazo hazikuwa zetu, tulikuwa na pesa chafu kwenye mzunguko na ndiyo maana tulikuwa tunaishi maisha ya "ibiza" ndani ya Tanzania.

  Huyu rais tuliye naye anania na dhamira ya kweli na taifa hili tumuunge mkono na siyo kumbeza. Maendeleo ni gharama na ili ufike ni sharti ulipie

  Shukrani!
   
 19. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #19
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,494
  Likes Received: 6,846
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo pesa chafu imeondoka? Kama imeondoka na serikali inalijua hilo imepima impact yake? Wamefanya nini kuongeza mzunguko wa pesa mtaani? Hiyo pesa chafu ilikuwa pia inafanya biashara na serikali inapata kodi yake. Baada ya kuiondoa biashara ikoje? Wananchi wanakopesheka? Mabenki yamestahimili hicho kishindo?

  Mwenye nia ya dhati anaua, anakandamiza wengine? Asikilizi ushauri, ana pesa za kununua wapinzani na kurudia chaguzi ila za kuwalipa wastaafu hana? Huyo ndiye mwenye nia ya dhati?

  Viwanda unavyoongelea vya Pwani vilianza kujengwa tangia awamu ya JK. Yeye kaleta kiwanda gani cha maana?
   
 20. dem boy

  dem boy JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 4, 2016
  Messages: 2,548
  Likes Received: 3,145
  Trophy Points: 280
  Kwanza sio 2025 ni 2027,pili kuna kila dalili mzee baba akabakia ulingoni hiyo 2027 kuelekea 2034

  Ni vyema mkafikiria mtakabiliana vp na hii hali kama hamtakubaliana nayo na hivi ndo mambo yalivyo wala msijaribu kutumia njia nyepesi ya kutatua tatizo kwa ku assume ya kwamba halipo....
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...