Tanzania tunamuhitaji Rais wa aina gani 2025? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania tunamuhitaji Rais wa aina gani 2025?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by FisadiKuu, Feb 22, 2018.

 1. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,483
  Likes Received: 6,833
  Trophy Points: 280
  Habarini za Asubuhi wanabodi..

  Uzi huu niuandika baada ya kusikiliza kupindi cha Straight Talk Afrika cha Shaka. Jana walikuwa wanaongelea siasa za Afrika Kusini na Cyril Ramaphosa. Binafsi sikuwa namjua Cyril vizuri mpaka alipokwaa madaraka kutoka kwa Zuma. Hapo ndipo nilishawishika kutafuta na kuusoma wasifu wake. Ukiacha mengine mengi, he is a purely businessman.

  Tanzania tuna mipango na matazamio mengi mbeleni, tunaitaka Tanzania ya viwanda na ifikapo 2025 tunatazamiwa kuwa nchi yenye uchumi wa kati (Second world country).

  Binafsi siamini kama hawa walioko madarakani sasahivi watatufikisha kwenye hata moja kati ya hayo mawili. Kufika huko hatuhitaji kauli za kibabe, sera zisizoeleweka za kuwakandamiza wawekezaji, kujifungia ndani tukiwasubiri mpaka wao waje.

  Serikali yetu ya sasa labda inafanya mazuri kwenye baadhi ya mambo ambayo kiukweli ni machache na yanahesabika. Serikali ya sasa imejaa wanataaluma ambao kiukweli hawana background yeyote kiuongozi hasahasa kibiashara zaidi ya kuwa wakufunzi tu.

  Mambo mengi yanakwama, viwanda tulivyohaidiwa hatuvioni vinavyofunguliwa vingi kama sio vyote vilikuwa initiated wakati wa Kikwete, wakati huo ilikuwa rahisi kushawishi wawekezaji sababu purchasing power ilikuwepo, hali ya fedha kwenye mzunguko ilikuwa nzuri. Ila sasa, ni wenyewe tu ndio wanajua wanachofanya.

  Tukirudi kwenye mada kuu, Je, kwa hapa tulipo na huu mkwamo tunaoupitia bila shaka kwanza tunahitaji Rais msomi lakini pia Rais ambaye amebobea kwenye masuala ya kibiashara.

  Hapa haraka lilinijia jina la ALI MAFURUKI. Kwa kiasi kikubwa naona Mtanzania huyu anaweza kutupeleka kule tunakotaka kwenda. Huyu amekulia kwenye buashara na anajua biashara haitaki ubabe, biashara yeyote duniani inataka NEGOTIATIONS, biashara haitaki two faced people. Kwamba leo tunaongea hiki alafu kesho tunageuka.

  Kwa mtizamo wako; nani unaona atafaa kuwa mrithi wa JPM?
   
 2. kiumbe kipya

  kiumbe kipya JF-Expert Member

  #21
  Feb 22, 2018
  Joined: Sep 30, 2016
  Messages: 2,468
  Likes Received: 1,071
  Trophy Points: 280
  Mkuu 2025 kwani 2020 hamna uchaguzi au??au ushatupa ushindi tiari??
   
 3. real G

  real G JF-Expert Member

  #22
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 7, 2013
  Messages: 5,261
  Likes Received: 5,103
  Trophy Points: 280
  Ali Mafuruki ana uzoefu gani kwenye siasa mpaka sasa? maana kuwa rais sio kujua biashara tu.. huyo Cyril ni mfanyabiashara lakini alikuwa kwenye siasa tangia kitambo sana
   
 4. kasolobela

  kasolobela Senior Member

  #23
  Feb 22, 2018
  Joined: Mar 25, 2017
  Messages: 101
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Mbona unaongelea 2025 wakati Kuna Uchaguzi 2020???
   
 5. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #24
  Feb 22, 2018
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,516
  Likes Received: 46,591
  Trophy Points: 280
  Tunaitaji Rais anaejielewa, ukali apeleke kwenye familia yake.
   
 6. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #25
  Feb 22, 2018
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,516
  Likes Received: 46,591
  Trophy Points: 280
  Umuunge mkono mtu asiekua na vision?
   
 7. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #26
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,483
  Likes Received: 6,833
  Trophy Points: 280
  Kipi kikubwa alichokifanya? Au tumpe muda?

  Binafsi ninampongeza kwenye miundombinu pekee.. Mpaka 2025 nadhani tutakuwa na barabara nzuri za rami kila kijiji.. Lakini kwa mengine mengi anafeli, hatuwezi kufikia nchi ya uchumi wa kati kwa idadi ya barabara tu.. Kuna mengi ya kufanya
   
 8. FisadiKuu

  FisadiKuu JF-Expert Member

  #27
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 19, 2015
  Messages: 5,483
  Likes Received: 6,833
  Trophy Points: 280
  Mkuu achana na story za vijiweni.. hata JK alishutumiwa kutaka kujiongezea muda. Hilo haliwezekani nchini kwetu
   
 9. dem boy

  dem boy JF-Expert Member

  #28
  Feb 22, 2018
  Joined: Nov 4, 2016
  Messages: 2,548
  Likes Received: 3,145
  Trophy Points: 280
  Tangu lini kijana wa kitanzani akawa na utamaduni wa kujadili mambo kama haya vijiweni??
  Hakuna kijiwe chenye upeo wa kujua na kupambanua hayo mambo siku hizi ,vijiwe vyote siku hizi vimejaa story za Diamond na Zari,Kusaga na Ruge,Gigy money na mimba,shilole na Uchebe,Okwi na Boko na story zingine zinazohusu ugumu wa maisha

  ....just jaribu kusoma vitabu then soma system ya uongozi ya huu utawala utagundua hilo jambo haliepukiki ndugu,watz wengi hawaamini hilo kama linaweza tokea ni kwasababu tu wana vichwa vigumu kuusoma mchezo..
   
 10. Titicomb

  Titicomb JF-Expert Member

  #29
  Feb 22, 2018
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 3,923
  Likes Received: 3,814
  Trophy Points: 280
  Unaongea usichokijua.
  Kuna kampuni nazijua hazikufanya ukaguzi wa hesabu(Auditing) kwa zaidi ya miaka miwili kinyume na sheria zinavyotaka.

  Na zilikuwa hazipeleki hesabu za marejesho ya kodi ya ongezeko la thamani au VAT. ( I mean they did not file VAT returns) na kuzituma TRA.

  Zilikuwa zinasuasua kulipa Corporate Tax za limited companies.

  Kilichokuwa kinafanyika ni kuwapoza tu wafanyakazi wa TRA kitu kidogo kama milioni 3 au 4 kwa kuchelewesha au kutowachukulua kabisa hatua kutikana na kidi wanazodaiwa zinazoanzia milioni 150.

  Jiulize hapo serikali inapoteza 150M kwa ajili ya mtumishi wake anavuta 5M na kisha analipwa stahiki zake kibao zinazofikia 4M au zaidi ni faida hiyo kwa taifa?

  Hizo 145M anazobakiwa nazo mfanyabiashara ndio ulikuwa unaona vurugu huku mitaani na maendeleo kwa taifa kama miundombinu na madawa au elimu bora hakuna kwa hao masikini(walaji) ambao wametozwa kodi.

  Bank kama CRDB zilikuwa jeuri hazikopeshi watu wa chini. Zinakopesha taasisi kubwa na matajiri ili maafisa wa bank wanaowezesha mkopo upite wapate 10% yao. Mwisho wa siku mikopo halipiki kwa wakati na kupelekea majanga kama ya bank ya wanawake.
  Ilikuwa deal kutajatisha fedha za serikali. Sasa waone CRDB wapo kwenye list yenye hali tete wakati hawa walisifiwa sana. Lakini NMB iliyokumbatia wanyonge hadi sasa hawajayumba sana labda pesa za mikopo ya waliotumbuliwa vyeti feki ndio zitawasumbua kidogo.

  Ule mfumo Kikwetwe ulikuwa unatajirisha wachache na kuifilisi nchi. Ni uchumi bandia ulikuwa unafaida kwa nchi za magharibi na China waliojipenyeza kwetu.

  Mkuu hayo madudu machache nasema kitu nilichokishuhudia kwenye corporate business companies. Na bado nipo nashuhudia huku mitaani wanavyoshindwa sasa kujiendesha na kudhibiti nidhamu yao ya matumizi huku wakilipa madeni ya nyuma.

  Hali mbaya ya sasa kifedha huku mtaani sio kosa la Magufuli bali ni la watangulizi wake na yeye anapojaribu kutuepusha yasitukute ya Cyprus, Ugiriki na kwingineko tunamrushia lawama za bure.
   
 11. p

  pilipili kichaa JF-Expert Member

  #30
  Feb 22, 2018
  Joined: Sep 3, 2013
  Messages: 7,574
  Likes Received: 2,953
  Trophy Points: 280
  Mwenye hekima na busara
  Mwenye hofu ya Mungu
  Asiekuwa na upendeleo na mkabila
  asiwe mtu wa visasi.
   
 12. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #31
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 687
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Mi naamini kila mtu huwa na Malengo yake, kwa wiki, mwezi na mwaka. Na katika hayo malengo yake kuna yenye kipaumbele zaidi.
  Ili tuweze kuwa na uchumi wa viwanda nilazima tuwe na nishati ya umeme ya uhakika ( rejea hotuba ya Obama ubungo) nadhani unajua nini kinaendelea kuhusu hili la umeme, kuna mradi unaitwa Rufiji Hydro Power Plant (RHPP).

  Miundo mbinu kama ulivyosifia hapo juu nadhani sina haja ya kulizungumzia hilo.

  Naomba tuwe na subira na kumwamini, kuna mambo mazuri naamini atafanya na yataacha alama kwenye jamii ya kitanzania ambayo kizazi kijacho kitajivunia mara baada ya sisi (kucheck out.)

  Dhana ya upinzani siyo kukosoa kila jambo ambalo serikali inafanya au kusonya mbele ya camera HAPANA.

  Kwa navyofahamu upinzani ni kuipa serikali changamoto kwa hoja zilizoshiba, kuishauri serikali kwenye maamuzi yake ndani ya bunge na si kuitisha maandamano yasiyokuwa na tija kwa umma.

  Ukiwa Mtanzania jisikie furaha na kujisifu kwenye kadamnasi kuwa na rais jembe na mpambanaji kama JPM.
   
 13. taekwondo

  taekwondo Member

  #32
  Feb 22, 2018
  Joined: Oct 6, 2016
  Messages: 35
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  kila nikikaa na kufikiria kuwa kuna namna ya mkulu kudumu kwenye kiti,mwili unakufa ganzi kabisa,kiukweli graduates tulioanza maisha enzi za huu utawala,tunakwama saana.
   
 14. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #33
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 687
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Mtu asiyekuwa na vision ni marehemu tu, ila binadamu yeyeto ana vision. Watanzania sijui tunakula vyakula gani siku hizi mpaka tunasahau haraka kiasi hiki!

  Ndugu rejea ufunguzi wa kampeini za ccm pale jangwani 2015, nenda YouTube tizama na sikiliza.
   
 15. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #34
  Feb 22, 2018
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,516
  Likes Received: 46,591
  Trophy Points: 280
  Zile ni porojo zisizokua na mbele wala nyuma, hauwezi kusikiliza maneno ya mtu anaeomba kura ukayatilia maanani.
   
 16. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #35
  Feb 22, 2018
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 687
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Porojo ambazo huwa hazitiliwi maanani ni zile zitolewazo mtu akiwa juu ya kifua.

  Awamu hii ya tano ina dhamira ya kweli na wakwamishaji nadhani unaona wanachofanywa. Tuunge juhudi za mhe Rais na sikubeza kila kitu.
   
 17. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #36
  Feb 22, 2018
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 21,516
  Likes Received: 46,591
  Trophy Points: 280
  Nimuunge kwa lipi la maana alikofanya mpaka sasa?
   
 18. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #37
  Feb 23, 2018
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 280
  Wewe umeuona mchezo unaoendelea na umeuelewa vizuri. Huu utaratibu wa kuwanunua wabunge wa upinzani unanionyesha kuna lengo kubwa kabisa mbele. Hii ni njama kubwa dhidi ya watanzania, wanatafuta mbili ya tatu ya wabunge wa bara ili wabadilishe katiba na kuweka kipengele cha kubadilisha mhula wa utawala. Kama rais atatusamehe, ataongezea kipindi kiwe miaka 7 kama Mhe. Juma Nkamia alivyotaka. Na watataka hiki kipindi cha miaka mitano kisihesabike. Kama hili litafaulu inawezekana utawala wa sasa kutawala miaka 19, hadi 20134.
   
 19. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #38
  Feb 23, 2018
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 280
  Kiongozi wa Taifa tunayemtaka antakiwa kuwa na uwezo mkubwa kabisa kwa nyanja mbalimbali, sio biashara tu, sio ukali tu, sio uaminifu tu. Mambo mengi, yanahitajika, lakini jambo kubwa kabisa anatakiwa mtiifu kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 20. peculiar my best

  peculiar my best JF-Expert Member

  #39
  Feb 23, 2018
  Joined: Apr 5, 2015
  Messages: 810
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 80
  1.Rais ambayo atakubali kupitishwa kwa Katiba mpya.
  2.ambaye askari wa jeshi lake hawatapiga risasi ya plastiki juu hewani ikarudi chini ikakata kona ikaingia kwenye gari na kuua mtu.
  3.ambaye Atafanya matajiri waishi kama malaika na masikini wawe matajiri
  4.ambaye ataifanya kuwa nchi ya uchunguzi umekamilika kutoka katika nchi ya uchunguzi bado unaendelea.
  5.atayekubali kukosolewa kama kikwete, ukimsema sana anakuita ikulu.
  6.atakaye pandisha thamani ya sarafu yetu kama mkapa
  7.atayeruhusu watu kufanya siasa na biashara kisheria kama mwinyi
  8.atakayepambana na madawa ya kulevya kama magufuli.
   
 21. Pierreeppah

  Pierreeppah JF-Expert Member

  #40
  Feb 23, 2018
  Joined: Feb 2, 2014
  Messages: 1,488
  Likes Received: 1,645
  Trophy Points: 280
  Mwenye utu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...