Tanzania tumekwama wapi maendeleo na kutawala Bora ?

Ikulumaliyawananch

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
339
533
Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 uchumi wa Tanzania ulikuwa sawa na uchumi Norway, South Korean, Singapore, Thailand na nchi nyingine nyingi katika mabara yote. Leo miaka 58 badaye nchi hizo zote zimeipita Tanzania kwa mbali sana.

Yani zimetoko kwenye nchi za ulimwengu watatu na kuingia kwenye nch za ulimwengu wa wa kwanza. Tanzania bado ipo palepale kwenye ulimwengu wa tatu, yana third world countries. Sasa chakujiuliza ni kwani nchi nyingine zimeweza kupiga hatuwa kubwa kiuchumi na kiutawala wakati Tanzania pamoja na rasilimali nyingi kuzidi nchi hizo imeshindwa kabisa kuendelea ndani ya miaka karibu 60?

Kwamtazamo wangu nafikiri kosa kubwa tulifanya na tunalo endelea kufanya ni aina ya viogozi tunao wapa madaraka kutuongoza, kosa la pili ni sisi wananchi kukubaliana na kuona umasikini na ujinga ni sehemu ya maisha ya kila mtu.

Maana nyingine watanzania sio wadadisi either kwa sababu ya kuathirika na propaganda za za watawala wanao tawala Tanzania tangu tupate uhuru. Au tamaduni zetu zina mambo mengi ya ujinga ambayo yanatuandaa kuwa wapumbavu tangu tukiwa wadogo, na kwasababu watawala wanafaidika na ujinga wetu hawataki kupampana na ujinga wetu. Na wanacho fanya nikuusifia ujinga na kufanya watanzania waamini kuwa ujinga ndio ujaja.

Tangu tupate uhuru tumekuwa maraisi ambao hawapendi kuhojiwa wala kuchalegiwa kwa mitazamo yao. maana yake tuna viogozi wanaofikiri wanajuwa kila kitu kuliko watu wote. Kutokana mtazamo huo wa watawala watanzania wote wamejikuta wameambukizwa mtazamo huo bila kujuwa ndio maana unakuta watu tunao waita wasome wanajitenga na watu tunao waita hawajasoma, unakuta mtu aliye soma mpaka chuo kikuu anataka kuwa karibu na watu wenye elimu kama yake. Aliye maliza form four anataka aliye ishia la saba amuogope.
 
KWANZA mkuu elimu akuna , PILI ufisadi uliopita viwango TATU viongozi wetu awana hofu ya mungu
 
Back
Top Bottom