Tanzania tuitakayo itakuja lini?

dindaiphilly

Member
May 27, 2012
6
0
Imekuwa ni hamu na ndoto za muda mrefu kwa watanzania kuipata TANZANIA waitakayo.

Tanzania inayojali usawa,Tanzania ambayo watu wake wanapata huduma bora za afya, elimu, miundo mbinu bora, Barabara, reli, viwanja vya ndege na ustawi bora kwa watanzania wote, Viongozi bora wa kisiasa wanaojali maslahi ya watanzania wote.

Hakika haya yote yamekuwa ni kama ndoto isiyotimia miongoni mwa watanzania.

Kila siku ukiamka asubuhi swali linabaki TANZANIA TUITAKAYO ITAKUJA LINI? Wadau, members na wanaJF wote mliko mnasemaje juu ya hili? Unafikiri TANZANIA TUITAKAYO INAWEZEKANA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom