Tanzania tuanzishe Coast Guard (Uokozi Majini)

Tanzania tuanzishe Coast Guard (Uokozi Majini)

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,494
uscg-crop.jpg

Nadhani kuna umuhimu wa kuanzisha kikosi maalumu cha uokozi Baharani ni kwenye maziwa makubwa kitakachiotwa Coast Guard ili kukiimarisha na kukifanya kiweze kufanya kazi saa 24 yaani usiku n mchana pale itakapotokea ajali yoyote ya majini.

Kwani kwa vikosi vyetu vya majini yaani Police Marine na Navy kwa JWTZ hivyo ukiangalia zaidi vipo kwa ajili ya ulinzi zaidi wa majini.

Ukienda nchi za wenzatu kama Norway kitengo cha uokozi kina boti ziendazo kasi,helcopter na ndege pia kiasi ambacho likitokea lolote eneo la majini wanafanya kazi saa 24 haijalishi kuna giza wala mwanga wa jua na kupeleka majeruhi popote pale ambako wanafikiri wanaweza kupata msaada kulingana na tatizo la majeruhi.

Kwa Tanzania hilo linawezekana kabisa kama vile KMKM kule Zanzibar ambavyo wanaweza kudhibiti magendo eneo kuu la bahari pia tunaweza pia kuweza kuanzisha kitengo cha uokozi.

Kila mmoja anakumbuka MV Bukoba walitoka wazamiaji toka Afrika ya Kusini kuja kuokoa majeruhi na maiti pia kuzitoa melini....Unakumbuka zile meli mbili zilizozama Zanzibara suala la uokozinlilikuwa changamoto sana ingawa kikosi cha JWTZ kilifanya kila linalowezekana kuhakikisha wanaokoa abiria na kutoa maiti lakini ni kwa juhudi za kizalendo zaidi.
 
This is very basic wazungu wanasema, sasa kama miaka 50 tunasheherekea uhuru suala dogo kabisa la kuwa na coast guards kwenye bahari, maziwa na mito yote tumeshindwa halafu watu wakiongea wanaitwa si wazalendo au wapinga maendeleo. Ulishaona hata diver mmoja pale mwenye gas kwenye lile tukio la uokoaji?, MV bukoba tumeiacha pale, Skaggit imepotelea baharini, MS Mtwara imepotelea baharini, Spice highlanders tumeizika baharini wakati ilitakiwa tuzitoe zikakae makumbusho kuvutia utalii na kama sehemu ya kumbukumbu pia..
 
Ngoja kwanza tununue wapinzani na madege ya kifahari, wananchi hamna issue
 
Yani unanunua mandege alafu huna hata boti ya kuokoa watu? kitengo cha maafa hakina pesa mpaka tungoje rambi rambi tuzipige? kweli baada ya miaka 50+ yauhuru bado tuko hapa?
 
This is very basic wazungu wanasema, sasa kama miaka 50 tunasheherekea uhuru suala dogo kabisa la kuwa na coast guards kwenye bahari, maziwa na mito yote tumeshindwa halafu watu wakiongea wanaitwa si wazalendo au wapinga maendeleo. Ulishaona hata diver mmoja pale mwenye gas kwenye lile tukio la uokoaji?, MV bukoba tumeiacha pale, Skaggit imepotelea baharini, MS Mtwara imepotelea baharini, Spice highlanders tumeizika baharini wakati ilitakiwa tuzitoe zikakae makumbusho kuvutia utalii na kama sehemu ya kumbukumbu pia..
Hivi unaufahamu jinsi sisiem inavyofurahi kumnunua mpinzani!??we acha tu!!! Yani tuacha kumnuna mpinzani na kurudia uchaguzi kisa eti Coastguard!!! Wewe unatakua mgonjwa
 
Ni kutafuta tu ulaji kwa majina ya kigeni, nini majukumu ya kikosi cha polisi maji,kikosi cha uokoaji na zimamoto na kikosi maji cha jeshi au hata idara ya maafa iliyo chini ya ofisi ya waziri mkuu? Hicho kikosi kingine labda kitolewe nje ya nchi kwa mkopo wa muda mrefu tulipe hilo deni hata kwa kulipa kodi ya kichwa!
 
VIKOSI VYA MAJESHI MAJINI KARIBU VYOTE VIKO KWA AJILI YA ULINZI
 
Hiyo ndege iliyonunuliwa haina mafundi Wala marubani. Ndio wapoTraining sasa hivi na ndege zipo kwenye packing lot yetu.
 
Hiyo ndege iliyonunuliwa haina mafundi Wala marubani. Ndio wapoTraining sasa hivi na ndege zipo kwenye packing lot yetu.
Boeing za zamani ATC zilikuwa zinaendeshwa na nani?
 
Ukifuatilia kwa umakini unaweza kukuta hicho kikosi kipo na watu wanapiga pesa kila mwisho wa mwezi
Asante sana ndugu yangu!
HICHO KIKOSI KIPO NA KINAFANYA KAZI NA WATU WA SA, hakikuanza leo, kiko muda mrefu tu walahi
Hivi kwa nini watu hawafanyi uchunguzi kabla ya kuanzisha uzi? TUIPENDE NCHI YETU KWA DHATI JAMANI HATUNA NYINGINE WALAHI!
Duh!
 
hakuna kikosi kama hicho tanzania wewe ukiona tu Navy JWTZ au Polisi marine basi unajua wako kuokoa ajali za majini
 
Back
Top Bottom