Tanzania Top Model kufanyika Jumamosi 7/12/2013

Tanzania Top Model kufanyika Jumamosi 7/12/2013

Joined
Dec 1, 2012
Posts
42
Reaction score
22
Shindano la Tanzania Top Model litafanyika kwa mara ya kwanza nchini siku ya Jumamosi 7/12/2013 katika ukumbi wa Mwalimu JK Nyerere ulioko Jijini Dar es salaam katka barabara ya Shaaban Robert inayoanzia kwenye viwanja vya Gymkhana na kuishia kwenye lango kuu la Ikulu ya Dar es salaam.

Wanamitindo 15 kutoka katika sehemu mbali mbali nchini ambao wameweka kambi yao katika Hotel ya Giraffe Ocean View watachuana katika kinyang'anyiro hicho kitakacho toa mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Top Model of the World mwakani.

Sambamba na shindano hili, atapatikana pia Princess of Tanzania atakaye patikana baada ya kupata kura nyingi zinazoendelea kupigwa mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom