Tanzania: Together we can, "freedom is coming tomorrow "

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,680
Reaction score
58,686
Ipo siku inakuja ,inakuja ,inakuja....

Ikiwa leo ni siku ya sikukuu ya X- mass niwape tu ujasiri watanzani kuwa tumeona maisha tofauti mwaka huu 2016 lakini niwape moyo wapenda mabadiliko ya kweli wote ya kisiasa,kiuchumi,kijamii ipo siku inakuja ambayo tutaishi tofauti.

Utu,Uhuru na Haki vitajaa kiwango cha maji ya bahari zilizozunguka dunia na kujaa mioyoni mwenu.

1: Ipo siku inakuja masikini wenzangu wa Kagera ambapo pesa zenu mahafa hazitachangwa na zingine zikapotea bure.

2: Ipo siku inakuja masikini wenzangu wa wafanyakazi wa serikali hautapita mwaka mzima bila kupandishwa vyeo na kupandishwa madaraja.

3:Ipo siku inakuja wanachuo wa art's nao watathaminiwa katika jamii kama zamani hawataitwa vilaza na kunyimwa Ajira wakati ni watoto wa masikini.

4: Ipo siku inakuja watu kama Ben Saanane wakosoaji wa serikali hawatapotea tena bila kupatika kwa mwezi mzima wakati kuna serikali.

5: Ipo siku inakuja wapigania Uhuru wa habari kama Max hawatasumbuliwa na police tena tutakuwa tukiishi maisha bila hofu dhidi ya Uhuru wetu wa kukosoa na kusema ukweli.

6: Ipo siku inakuja wakina Lema na wengine waliopo gerezani kwa hila na figisu figisu za serikali watakuwa huru watakuwa nje na kufurahia Xmas na ndugu zao .

7: Ipo siku inakuja wahujumu uchumi ndio itakuwa priority number moja ya serikali kuwashugulikia ,Watu kama wakina Mulla wa meno ya tembo,Mafisadi kama Lugumi Singasinga wa IPTL hawatachezea tena kodi zetu maisha ya watanzania.

8: Ipo siku inakuja priority yetu itakuwa ni kutoa huduma muhimu na bora za jamii kama Maji,Umeme,Dawa hospital kutoa Ajira sio kujenga uwanja wa ndege Chato.

9 : Nasisitiza ipo siku inakuja watanzania hata wahamiaji haramu hawatauawa na kuwekwa kwenye mifuko na kuwekewa mawe na kutupwa kwenye maji ya Mto Ruvu ambayo wakazi wa dar wanakunywa kila siku.

10: Mwisho ipo siku inakuja ambapo waandishi wa habari hawatawekwa kizuizini kwa kuripoti njaa eneo husika,au kuripoti kero za maji eneo usika Wakati watanzania karibu asilimia 75% hawana maji safi na salama.

Nasisitiza ipo siku inakuja watu wote wa nchi hii watakuwa na furaha kwa pamoja na kupaza sauti zao kuongea ukweli na kuwaambia watawala kuwa hapana ni hapana na ndio ni ndio tena kupitia chombo chochote cha habari iwe radio,iwe TV.

Hapo ndipo watanzania wote kusini kasikazini magharibi,Mashariki tutakuwa tukiishi kwa furaha sio woga na hofu tutakuwa tukisherekea sikukuu kama hizi kwa tabasamu sio hasira.

Naomba Mungu aendelee kutupa nguvu na akili za kuongea ukweli na kutenda mengi yaliyo mema maana safari bado ni ndefu lakini ipo siku inakuja .

Mungu ibariki Tanzania wabariki na watu wake wanaofuata misingi yako.

"Merry Xmas to all Tanzanians " naipenda sana Tanzania

[HASHTAG]#togetherwecan[/HASHTAG].
 
Katika dunia ya sasa hayo yoote huwezi yapata labda mbinguni tu, anayoyafanya Mh Rais kwa sehemu kubwa duniani ndiyo yanayofanyika na watu wanafurahi na kuendelea na maisha.

Ukisubiri hayo uliyoorodhesha basi okoka utayapata kwenye paradiso lakini katika hii dunia inayotawaliwa na shetani ibilisi usitegemee kuipata haki kama upo paradiso.

Hata ashuke nabii gani bado hataweza kuturidhiasha matakwa yetu wanadamu kisawasawa malalamiko yatakuwepo tu.
 
Mimi huwa sikuelewi kama ambavyo simwelewi Popo...anaonekana ni ndege lakini pia huonekana kama ni mnyama (mamalia)...
 
nyie mna politicise vitu sana, japokuwa sifurahishwi na mambo mengi ila Tanzania sio nchi mbaya kihivyo mnavyodai
 
Katika dunia ya sasa hayo yoote huwezi yapata labda mbinguni tu, anayoyafanya Mh Rais kwa sehemu kubwa duniani ndiyo yanayofanyika na watu wanafurahi na kuendelea na maisha.

Ukisubiri hayo uliyoorodhesha basi okoka utayapata kwenye paradiso lakini katika hii dunia inayotawaliwa na shetani ibilisi usitegemee kuipata haki kama upo paradiso.

Hata ashuke nabii gani bado hataweza kuturidhiasha matakwa yetu wanadamu kisawasawa malalamiko yatakuwepo tu.
Kwanini mkuu Lazima kuna siku tutapata anayeomba anapewa ,anayebisha anafunguliwa
 
Katika dunia ya sasa hayo yoote huwezi yapata labda mbinguni tu, anayoyafanya Mh Rais kwa sehemu kubwa duniani ndiyo yanayofanyika na watu wanafurahi na kuendelea na maisha.

Ukisubiri hayo uliyoorodhesha basi okoka utayapata kwenye paradiso lakini katika hii dunia inayotawaliwa na shetani ibilisi usitegemee kuipata haki kama upo paradiso.

Hata ashuke nabii gani bado hataweza kuturidhiasha matakwa yetu wanadamu kisawasawa malalamiko yatakuwepo tu.
Dawamahospitalini tuta patatu,Shetani haingii hapo.
 
Hakuna uhuru usio na mipaka.

Mkuu umekosea sio "Merry Xmas to all Tanzanian" ni Merry Kristmas to all Tanzanians.
 
nyie mna politicise vitu sana, japokuwa sifurahishwi na mambo mengi ila Tanzania sio nchi mbaya kihivyo mnavyodai
Hakuna ambaye anakataa lakini tukinyamaza ndio tunazidi kudidimia bora tupingee kidogo wengine stress zetu zinaishia kwenye kuongea sasa ukitaka tunyamaze maana yake tubameza sumu
 
1: Ipo siku inakuja masikini wenzangu wa Kagera ambapo pesa zenu mahafa hazitachangwa na zingine zikapotea bure.
Wewe nae wakati mwingne unakuwa na matatizo sana.....HIVI HIZI PESA ZA KAGERA mbona mnapenda kuishi kwa umbea sana bila ya kuwa na uthibitisho.....HAPA TUNATEGEMEA UJE NA USHAIDI YA KUWA HIZI PESA ZIMEENDA KWENYE MIFUKO YA WATU..........na si kubwabwaja as if hizi pesa zimeliwa na pia tunataka atleast kufikia sasa unakuja na ushahidi either wa video au wahusika juu ya hali yao ya MAISHA huko wa liko JE mapaka sasa hawajapokea msaada wowote au wanalala nje
Ipo siku inakuja watu kama Ben Saanane wakosoaji wa serikali hawatapotea tena bila kupatika kwa mwezi mzima wakati kuna serikali.
Hii mbona kila ipo WAZI mpaka sasa WAULIZWE CHADEMA kuhusu huyu KIJANA maana jinsi alivyokuwa akitumika kukikiingia KIFUA hiki CHAMA NAKUPOTEA KWAKE LEO HII NA uzito wanatoa CHADEMA juu ya utafutaji wa huyu kijana inatia SHAKA SANA...Tatzo unavyoandika ni as if SERIKALI INAHUSIKA NA KUPOTEA KWAKE....
Ipo siku inakuja wapigania Uhuru wa habari kama Max hawatasumbuliwa na police tena tutakuwa tukiishi maisha bila hofu dhidi ya Uhuru wetu wa kukosoa na kusema ukweli.
Na ulivyokuwa na AKILI NUSU...un afikiri hili linaweza timizwa kwa kutukana VIONGOZI MATUSI????atah kama angekuwa ni LOWASSA asingekubali huu UPUUZI......
Ipo siku inakuja wakina Lema na wengine waliopo gerezani kwa hila na figisu figisu za serikali watakuwa huru watakuwa nje na kufurahia Xmas na ndugu zao
Hivi ndio VIZAZI vya ajabu kweli...HIVI kwa akili yako unafikiri atah kama ingekuwa ni wewe UNGERUHUSU huu UPUUZI wa LEMA????walio wengi na hata waliomchagua wameishamuona ni MPUUZI na ndio maana hakuna atah movement yoyote wakazi wa ARUSHA wameionyesha kupinga LEMA kuwa GEREZANI ni wapuuzi wa wachache wenye CHUKI Na serikali hii ndio mnaolala humu kwenye mambo mema.....
 
Mkuu kwa nini ?
Mkuu kuna baadhi ya nyuzi zako nikizisoma unaonekana wazi we ni ""pro-ccm"", unasifia matamko ya kina pogba...lakini wakati mwingine unaleta uzi ambao kwa kweli unakutambulisha wazi kama..mtetezi wa watu, usiependa kuona watu wakipitia haya mateso wanayopitia, ukikemea wazi wale waliokwapua rambirambi za maafa.. (ref..huu uzi wako)..
 
You always impress me. Nami nasema ipo siku hata mawe yatapiga kelele kama watafanikiwa kutunyamazisha. Ipo siku wanaodhulumu haki watadhulumiwa hapa hapa duniani.
 
Freedom is coming, hivyo nyinyi watu ni nani anaewatuma kuandika huu ujinga?, hivi ni kweli tanzania hatuna uhuru, ata huo upuuzi umeandika kwa vile unao uhuru wa kuandika upuuzi, hacheni mambo ya ajabu, kuna nchi zinatamani maisha yetu lakini hawapati hiyo fursa , kila siku ni mapigano tu, wewe unalala unaamka unakula, sijui bado unakaa kwa baba hako,unaenda kupiga viroba unarudi hakuna ata aliekushika shati alafu unasema freedom is coming, pumbavu.
 
No. 7 mbona Lowasa hayumo????? Au ukiingia Cdm ndio unatakasika!!!????
 
Wewe nae wakati mwingne unakuwa na matatizo sana.....HIVI HIZI PESA ZA KAGERA mbona mnapenda kuishi kwa umbea sana bila ya kuwa na uthibitisho.....HAPA TUNATEGEMEA UJE NA USHAIDI YA KUWA HIZI PESA ZIMEENDA KWENYE MIFUKO YA WATU..........na si kubwabwaja as if hizi pesa zimeliwa na pia tunataka atleast kufikia sasa unakuja na ushahidi either wa video au wahusika juu ya hali yao ya MAISHA huko wa liko JE mapaka sasa hawajapokea msaada wowote au wanalala nje

Hii mbona kila ipo WAZI mpaka sasa WAULIZWE CHADEMA kuhusu huyu KIJANA maana jinsi alivyokuwa akitumika kukikiingia KIFUA hiki CHAMA NAKUPOTEA KWAKE LEO HII NA uzito wanatoa CHADEMA juu ya utafutaji wa huyu kijana inatia SHAKA SANA...Tatzo unavyoandika ni as if SERIKALI INAHUSIKA NA KUPOTEA KWAKE....

Na ulivyokuwa na AKILI NUSU...un afikiri hili linaweza timizwa kwa kutukana VIONGOZI MATUSI????atah kama angekuwa ni LOWASSA asingekubali huu UPUUZI......

Hivi ndio VIZAZI vya ajabu kweli...HIVI kwa akili yako unafikiri atah kama ingekuwa ni wewe UNGERUHUSU huu UPUUZI wa LEMA????walio wengi na hata waliomchagua wameishamuona ni MPUUZI na ndio maana hakuna atah movement yoyote wakazi wa ARUSHA wameionyesha kupinga LEMA kuwa GEREZANI ni wapuuzi wa wachache wenye CHUKI Na serikali hii ndio mnaolala humu kwenye mambo mema.....
Hivi swali Dogo tu zilikusanywa kiasi gani? Na zilitangazwa kiasi gani kama ujui utakuwa ni moja ya wakwapuaji
 
Mkuu kuna baadhi ya nyuzi zako nikizisoma unaonekana wazi we ni ""pro-ccm"", unasifia matamko ya kina pogba...lakini wakati mwingine unaleta uzi ambao kwa kweli unakutambulisha wazi kama..mtetezi wa watu, usiependa kuona watu wakipitia haya mateso wanayopitia, ukikemea wazi wale waliokwapua rambirambi za maafa.. (ref..huu uzi wako)..
Mimi tatizo sitetei vyama natetea "watu"
 
Freedom is coming, hivyo nyinyi watu ni nani anaewatuma kuandika huu ujinga?, hivi ni kweli tanzania hatuna uhuru, ata huo upuuzi umeandika kwa vile unao uhuru wa kuandika upuuzi, hacheni mambo ya ajabu, kuna nchi zinatamani maisha yetu lakini hawapati hiyo fursa , kila siku ni mapigano tu, wewe unalala unaamka unakula, sijui bado unakaa kwa baba hako,unaenda kupiga viroba unarudi hakuna ata aliekushika shati alafu unasema freedom is coming, pumbavu.
Wewe acha useme nilicho andika hapo kama kuna jambo la uongo.....

Hata hizo nchi walianza hivi wakaenda uko.....
 
Iko siku meza itapinduliwa hekaluni na hapo ndipo furaha na Uhuru wa kweli utapatina. Wokovu wa taifa na watu wake waliokataa tamaa
Ipo siku inakuja ,inakuja ,inakuja....i

Back
Top Bottom