Tanzania, Taifa lenye nguvu kubwa duniani

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
TANZANIA, TAIFA LENYE NGUVU KUBWA DUNIANI

Leo 11:30hrs 20/09/2020

Tanzania ni nchi kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa na idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 60, Tanzania ingekuwa na code of unity, ingeweza kutawala dunia kwa ukubwa wake na maliasili iliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu,Tanzania ingeweza kulitawala bara la Afrika ambalo ndilo bara la pili kwa ukubwa duniani, ikitoka Asia.

Shule ya msingi tulitumia Atlas kujifunza jiografia ya nchi yetu na bara letu la Afrika,tumekua tukitumia Atlas kujua maeneo ya nchi yetu na rasilimali zake,kwa bahati mbaya kwenye Atlas nilikuwa naiona Tanzania ni ndogo sana hata bara la Afrika nililiona ni dogo kuliko nchi ya Urusi,nikaja pata elimu kidogo baadae ya kwamba ramani ya dunia nzima uwa inachorwa kwa kutumia 2 dimension of sphere lakini nilipoangalia zile kwenye atlas ilikuwa imechorwa kwa kutumia 2 dimension representation of sphere ambayo ni sawa na 3 dimensional ambapo kwenye kona za picha hiyo lazima upana uongezeke na kati kati kubaki kwa vipimo vya udogo.

Mzungu alipokuja Afrika na kuikuta historia ya Afrika tofauti na walivyotegemea,Mzungu alihakikisha anatengeneza inferiority complex kwa mwafrika kwa kumuaminisha ya kuwa bara la Afrika ni dogo sana kwa kupunguza ukubwa kwenye ramani, pia Alihakikisha vitabu vyote vilivyo andikwa Afrika kwenye Chuo Kikuu cha kwanza Duniani,Chuo Kikuu cha Timbuktu (University of Timbuktu) anaviteketeza na kuvificha,Afrika imefichwa historia yake ya ukweli kwa miaka 1000 nyuma,

Misri ina historia ya maendeleo Miaka 2500 kabla ya kuja kwa Yesu, enzi ya Musa na Joseph ( Yusufu) Wao tayari walisha piga hatua ya kimaendeleo ya kitechnolojia kabla ya Ulaya, Tanzania tukijiongeza tunaweza. Iran ni taifa la kupigiwa mfano, Kutokea Utawala wa Shaha ulipopinduliwa 1979 hadi leo ,Maajabu makubwa yametendeka pale,Wale Maayatolla na akina Mzee Ahmed Najjad wamefanya kazi kubwa mno kwa kipindi hicho kifupi na wameweza kuwa miongoni mwa Mataifa yenye nguvu kubwa duniani.

Iran hivi sasa wana Satellite kadhaa katika Orbit zikiitumikia technology ya Iran na wana uwezo wa kutengeneza makombora ya masafa marefu,Nege za kivita,Meli, Na Mafuta wanachimba wenyewe wale majamaa,Tazama Hat Drone wanatengeneza, na waliweza kuipopowa Drone ya USA ikatua salama kwenye mikono yao bila ya hata kuiharibu,hii ni Ushahidi wa technology waliyo nayo kwa sasa.

Hivi sasa detector ya kumjua mgonjwa wa corona kwa mbali kabla hajakufikia kwa umbali wa mita kadhaa,Pia tunaweza kujifunza kwa Madagascar,Wao waliwezaje kupata dawa na kuiendeleza kwa kiwango kile kwa muda mfupi hivi,na tayari ipo kwenye large scale production,hii ni hatua muafaka.

Tanzania tunapaswa kuwatazma watu kama hawa, siokushupalia wazungu watusaidie,bila wazungu hatuwezi kuishi, tutatengwa na dunia, lazima tutumie rasilimali zetu na tusimame kwa miguu yetu.

Nimepata bahati ya kuisoma barua ya Daktari David Livingstone,na maandiko mengine yaliyoandikwa na Jasusi Mbobezi Henry Morton Stanley aliyesafiri Kaskazini hadi Mashariki kumtafuta Dr David Livingstone, wote walitaja waliyokuwa wanayaona njiani. Dr Livingstone alipofika Tabora alikuta watu wa tabora wanawachukua watumwa wenzao walioachwa njiani na Mwarab kwa sababu ya kua dhaifu kutokana labda na njaa au maradhi na kwenda kuwauza tena kwa mzungu.

Morogoro ni sehemu pekee ambayo Henry Morton Stanley anaitaja kutoshiriki biashara ya utumwa, katika kitabu chake cha"How I found Dr Livingstone" Jasusi Henry Morton Stanley anamuelezea Chifu wa eneo la Morogoro, Kingo wa Kisebengo kama mtu tajiri sana, aliyekuwa na ngome kubwa sana ya ukuta wa mawe katikati ya Milima ya Uluguru, alimiliki jeshi kubwa lililokuwa na vazi la majani, Henry Morton Stanley anasema hakuwahi kuona jeshi katika uwanda wa Milima ya Uluguru.

Lakini baada ya kufika kwenye himaya ya Kingo wa Kisebengo aligundua alipishana askari wengi njiani waliokuwa wamejificha maporini wakifanana kabisa na majani ya miti ya porini,Kingo Kisebengo,pamoja na Chifu Msumi ambaye alimzaa Chifu Kingalungalu walipiga vita biashara ya Utumwa hata kumkamata Henry Stanley na baadae kumuachia na kumpa makazi maeneo ya kihonda ilipo Shule ya Kayenzi hivi sasa ili aweze kujenga na kuishi huku akiendelea kumtafuta Dr David Livingstone.

Kingo Kisebengo alitawala Kaskazini ya Milima ya Uluguru hadi pwani ya Afrika Mashariki na bara,Milima ya Uluguru ndio eneo ambalo kijiografia linatajwa kutia nanga kwa Safina ya Nuhu na kila kiumbe cha Leo duniani kiliteremkia katika Milima ya Uluguru.Kwenye kitabu cha "How I found Dr Livingstone" chapter 4 na 5 mbobezi Henry Morton Stanley anasema katikati ya Milima Uluguru kulikuwa na falme iliyojitegemea kwa kila kitu, Jamii hiyo ya kifalme ilizungukwa na ngome kubwa na ukuta mnene kuingia kwenye ngome hiyo,Mtawala wa eneo hilo aliitwa "King Kisebengo".

Nakubaliana na kila Mzalendo kuwa tungeendelea na taratibu, mila, desturi basi tungefanikiwa zaidi bila hata Elimu ya mzungu ambayo ni "Remembering" and not "thinking" hivi Leo watoto wetu wanafundishwa "when" instead of "why" hatuna tena elimu ya ugunduzi, hatuna tena common interest,common purpose wala common identity, kutokana na hayo sasa rasilimali zetu zinasombwa na wakubwa zetu ambao ni nchi za Ulaya na Marekani.

Emperialist came and conquered Afrika, Henry Morton Stanley is one of them,and Dr David Livingstone is also one of them, I gave you the example of a Roman, or Europe bible, the thing made African to be conservative and their minds became dogma, and dogmatism is the result of "remembering".The first President of South Africa, Pieter Willem Botha once said "This Pretoria is built by the White man brain", and again, He said "Black people don't have brain and Mental capacity"So there was no any chance of self believe among the African, thus led the whites to manipulate and maginate the African brains.

Elimu tunayoisoma ni bomu la kutega, watazame Nigeria, maprofesa wanauza mitumba kama machinga,watu wanakimbilia kwenye ajira ya Ubunge, Ubunge umekuwa ni ajira sio wito tena,tunategemea mbunge mmoja aiambie Serikali kuhusu suala hili, lakini wapi! hatuna mbunge mwenye uelewa mpana, hatuna mbunge mwenye sera mbadala, hatuna mbunge mwenye kuleta chachu ya Maendeleo, hili ni toleo la elimu yetu ambayo italeta wapokea rushwa na watoa rushwa na baadae kuleta kiongozi bomu, tutakuwa na kiongozi bomu na mwananchi asiye na sikio la kusikia dhana wala sera mbadala ya kuleta chachu ya Maendeleo, tunahitaji kiongozi na mwananchi mwenye 'will' ya kulitenda sawa sawa na wito wa Uzalendo uliomuita kwenye siasa.

Mila na utamaduni wetu uko wapi, mtoto wa kimasai aliishi miaka nenda huko nyuma akijifunza elimu ya kufuga ngombe na elimu ya uchungaji, leo kumchukua mtoto yule ukamsomesha elimu ya kuja kukaa ofisini ni kuiangamiza Tanzania na kuangamiza ufugaji wa kiasili, jambo muhimu la kujiuliza,ni kuwa vipi Taifa letu la Tanzania lilikuwepo miaka elfu kadhaa iliyopita na wazee wetu waliweza kuishi kwa kutumia Uongozi wa Machifu na ku survive? Na kuongoza dola zao kadhaa hadi ukoloni ulipokuja nao pia uliendelea kuheshimu machifu Lakini tulipo pewa uhuru tuliamua kuufuta mfumo wetu wa jadi na kuleta mfumo huu wa kijumla jumla.

Je, elimu ndio mwanzo wa kifeli!? Leo sisi kwetu elimu ni kwenda shule tuu, kusoma vitabu vya wazungu, kwa kizungu sisi wenyewe hatuandiki chochote kuhusu vitu vyetu na elimu zetu haziandikwi kabisa.Nchi zote zilizotoboa kimaendeleo duniani zinasomesha elimu kwa Lugha yao ya asili ,sisi tumelogwa? tumeng'ang'ania Kiingereza tu utafikiri ni lugha ya aliyetuumba?

Kuna waganga wa kijadi wengi tuu wanajua madawa ajabu ,hata sumu ya nyoka inatolewa kwa miti shamba,' tetanus ' inatolewa kwa chokaa, chango la uzazi linatibiwa kwa ndizi ya kuchoma, bawasiri inatibiwa kwa habasoda, Pumu(Athma) inatibiwa kwa mtanda kanga na chumvi, hata Madagascar iligundua dawa ya corona nk. hii ndio Afrika iliyopuuza vyake na kukimbilia vya wazungu na hatimae kuwa watumwa wa kielimu, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na kiulinzi pia.

Tukitaka kufanikiwa ni lazima tuanzie 'from the scratch' 'never too late' kimya kimya tunaweza kuibuka na kitu wazungu wakatushangaa,Nikitazama pale bungeni huwa nacheka sana nikiliona lile lidubwasha linaloitwa "siwa" linavyo bebwa na kusujudiwa,kile ni kinyamkela cha Muingereza kiko pale tunakiabidu kinyamkera cha muingereza halafu tunajiita sisi ni nchi huru? Ni muda sasa wa kuliondoa lile lidubwasha tuweke ngao ya Mkwawa na mkuki wake au tuweke Mwenge wa Uhuru,kama alama ya uzalendo na kuondosha kabisa fikra za kutawaliwa kimawazo.

Nimalizie kwa kukupa tafakuri jadidi ambayo itakurudisha Afrika na kukupa akili ya uvumbuzi ambayo iliishia Mwaka 1970,Ebu Fikiria miaka 7 msingi,miaka 6 high school,degree miaka 3 au 4 masters miaka 2 ,miaka 22 yooote unasoma halafu kuajiriwa lazima uwe na uzoefu wa miaka 5 ambayo wengi hawapati,Na kwa nini kuajiriwa,kwa sababu tuna akili ya kuremember na sio ya kufikiria ndio maana tunataka kuajiriwa,huu mfumo ni kuwapotezea watu muda na mwishowe ndio kina Tundu Lissu wanaishia kuwa vibaraka wa wazungu uko Ulaya.

Sasa turudi kwa mjasiriamali ambaye alijiajiri tangu amemaliza shule ya msingi Kama Msukuma Kasheku Mbunge wa CCM kule Geita, Sasa ni milionea anayeajiri wasomi hao na kuwapa amri, nadhani hii ndio ingepaswa kuwa elimu ya kiafrika na sio elimu ya mzungu ya darasani, Waafrika tungeweza kutengeneza mfumo wetu wa kielimu ya muda mfupi na kuwatoa watu kwenye umasikini. Sijui tunashindwa nini kuachana na elimu yenye mfumo wa Mzungu, Wenzetu Wachina waliweza japo mwanzoni waliyafanya kama hayaa lakini wao walifanya kwa utofauti kidogo. Waliwapeleka vijana wa kichina kusoma technical school kila mahali nchi za ulaya na Marekani,

Waliwastop wasiende high school maana ni kupoteza muda,waliwapeleka technical school ili wakajifunze ujuzi wa kutengeneza vitu mbali mbali. Angalia sasa wanatengeneza kila kitu cha dunia hii kiwe fake ama original wao wanafanya.

Wana viwanda mpaka kwenye sebule zao na hata kwenye kila nyumba ya chumba kimoja. Ni taifa lililokuwa chini saana lilionewa sana na wajapani leo wao ni namba mbili kama sio moja kwa uchumi duniani, hiyo ni nafasi iliyopaswa kuchukuliwa na Japan, tukiamua kuachana na wazungu inawezekana na ndicho anachofanya Rais John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Ooh, kumbe ni mwanakijani kwa mujibu wa hiyo avatar. Nimekuelewa, endelea
 
To some extent nakubaliana nawe. Elimu ya mzungu imelenga kutufanya watumwa wao, kwa sababu elimu hii haimwandai mwanafunzi kufikiri, bali kutoa alichokariri. Tazama debate za wasomi wakubwa hapa nchini, NI NADRA SANA MSOMI KUJA NA MTAZAMO WAKE, wengi wanaringia rejea za wasomi wa Ulaya na Marekani.

Sasa mwanadamu ameumbwa ayatawale mazingira yake. Huwezi kamwe kutumia mfumo wa Ulaya kuleta maendeleo Afrika. Badala yake utaigeuza Afrika kuwa mtumwa wa fikra za kimagharibi. Mambo haya husemwa kwa mfano:

Watanzania wengi wanapata shida sana kuongea Kiingereza hata kama ni wasomi. Unajua sababu ni nini? HUWEZI KUITAWALA LUGHA KAMA HUJAJIFUNZA KWANZA KUFIKIRI KWA LUGHA HIYO. Tunaongea Kiswahili kwa raha bila kusitasita kwa sababu tunafikiri kwa Kiswahili. Ndivyo ilivyo kwa lugha za asili. Lakini linapikuja suala la Kiingereza, wengi wetu tunafikiri sentensi Kiswahili kisha tunatafsiri kwenda Kiingereza, hapo ndipo tatizo lilipo.

Huwezi kuleta maendeleo ya familia yako kwa kufikiri kwa mipango ya familia nyingine. You have to be original. Huwezi kupata mafanikio ya kibiashara kama huna wazo original, wewe kazi yako ni kuiga tu. Taifa haliwezi kuendelea kwa kuigiza mfumo wa taifa jingine. Sasa elimu yetu imelenga kutengeneza ustaarabu wa Ulaya na Marekani kwenye taifa ambalo watu wake wala hawajui ustaarabu ni nini. Matokeo yake ni confusion. Magharibi walifika hapo walipo baada ya mchakato wa miaka mingi. Haikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua kama tunavyotaka kwetu iwe. China walifika hapo walipo baada ya kulipa gharama kubwa. Wote hawa walijitengenezea mifumo yao wenyewe kulingana na mazingira yao wakaisimamia. Kisha sisi tunatoa photocopy ya mifumo hiyo ili tuitumie hapa kwetu!!

Matokeo yake elimu yetu imekuwa ni utumwa. Profesa anajitapa hadharani kuwa darasa la saba hana cha kumshauri kwa sababu tu amekariri mawazo magharibi. Hapa ndipo tulipofikia.

Wakati ukisema Tanzania ni taifa tajiri zaidi Afrika, ukweli ni kuwa Mungu aligawa mali kila mahali kwa ajili ya kuwastawisha watu wake. Tatizo lilianza pale watu waliopo kwenye eneo husika walipokoma kufikiri na kuamini vya wengine ni bora zaidi kuliko vyao. Ndiposa kila taifa likataka liwe na mafuta, gesi, Tanzanite nk.

Wakongo wana msemo mmoja, kwamba wanaamini Mungu alipoumba nchi alianza kuzunguka na kapu kubwa sana lenye kila aina ya madini, akawa anagawa kwa kila nchi, hapa dhahabu, pale almasi, pengine rubi nk. Sasa alipofika DRC alikuwa amechoka sana. Hivyo akamwaga madini yote yaliyobaki kwenye kapu hilo, akarudi zake mbinguni. Ndio maana DRC kuna utajiri mkubwa wa kila aina ya madini. Swali je, nani ananufaika? Ndivyo ilivyo kwa Tanzania, Mungu katupa mali nyingi lakini tunachoweza kufanya ni kuzipeleka kwa wanaofikiri. Tumebanwa kwenye utumwa wa kimagharibi.

Kumbe bila ukombozi wa kifikra, haiwezekani kuendelea kamwe.
 
Weee Chagua CCM tunaenda kukamilisha hili jambo na tunaenda kupanda zaidi kiuchumi maana nguvu na nia tunazo zikisimamiwa na Chama cha Mapinduzi chini ya Jemedar Dkt Magufuli basi kila kitu kitakuwa sawaaa.
 
"Tundu Lissu wanaishia kuwa vibaraka wa wazungu uko Ulaya"..nimesoma uzi wako kufika hapa nikaacha mafi mafi tuu...Nyie ndio wasomi anaowasema Lissu mnakariri kwa ajili ya mitiani huku maarifa hamna..
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Siku nyingine huwa nawaeleza halafu hamfuati, niliwaambia mnichague mimi mkasema sawa, nikawaambia mnichagulie na mbunge wa CCM hamkunichagulia, nataka niwaeleze ukweli wala siwafichi asingekuwa Kapuya hii barabara nisingeijenga". Dkt.Magufuli
 
Pamoja na yote bado tumebaki watumwa wa kifikra na unaoangalia afrika tunatambaa hatuwezi kusimama na kutembea kulingana na hali halisi tunayoweza kusoma hama kujifunza.

Nadhalia ya kweli inayopatikana kwenye vitabu kwa sasa onakuwa ngumu kuingia kwenye uhalisia wa mwafrika mwenyewe kutokana na nguvu iliyotumika kutuondoa kwenye ile nature yetu ilishasagwa sagwa na kupeperushwa na upepo.

Ukiangalia leo tunapigana sisi kwa sisi, mmeru anapigana na muikizu kisa siasa, hapo hapo unataka asili ianze kutumika upya kitu ambacho hakiwezekani kwa sababu mfumo ulishaharibiwa kitambo.
 
hebu Nikuulize, kiswahili ni rahisi? Mbona hata hapa kwenye forum kuandika Kiswahili ni Shida? Kwa mfano neno “mabadiriko au mabadiliko “ lipi ni sawa? Msianze sababu za kijinga kuhalarisha weakness
 
Elimu ya mzungu unayosema ni ya "remembering" badala ya "thinking" ni hii iliyoleta magari, madawa, nguo, simu uliyotumia, ndege, redio,umeme wa stigler,SGR na vitu vingine kama hivyo?
 
hebu Nikuulize, kiswahili ni rahisi? Mbona hata hapa kwenye forum kuandika Kiswahili ni Shida? Kwa mfano neno “mabadiriko au mabadiliko “ lipi ni sawa? Msianze sababu za kijinga kuhalarisha weakness
Matusi hayajengi. Umedhihirisha ujinga wako kwa kushindwa kujadili mada husika na badala yake kujikita kwenye spelling error. Huko ni kukosa hoja na ndio ujinga wenyewe. Kwamba hata msingi wa hoja umeshindwa kuuona.
 
Back
Top Bottom