Tanzania,taifa ambalo jinai ni chai ya asubuhi,bora uwe na pesa.

Truth guy.

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
396
195
Taifa hili limefika mahali ambako mtu anatenda kosa na bado sheria inapindishwa,fikiria kuna kundi kubwa la watu limeibuka kukopesha pesa za riba bila ya kuwa na kibali maalumu cha BOT,na halilipi kodi ya serikali na linanyanyasa watu litakavyo maana linakula na police,mtindo huu upo wilaya ya kahama kwa sana,ukichukua laki moja ukachelewa kulipa kidogo tu unaongezewa riba kwa asilimia mia,ukikwama kulipa unakamatwa na police na kufunguliwa kesi ya wizi wa kuaminiwa,ilhali ulikopa,taifa lenye serikali,rais,usalama wa taifa,lakini nchi inaenda kama hatuna serikali,mama mmoja alikopa sh laki 5,akachelewa kulipa kwa wk 2,akapandishiwa ikawa milioni moja,akapeleka laki 8 akagomewa,siku zikazidi kwenda,ndani ya miezi mitatu akawa anadaiwa sh mil 3 kutoka laki 5,sasa kaporwa kijumba chake na hapa pa kuishi,taifa gani hili jamani?
 
Back
Top Bottom