Tanzania siyo nchi ya uchumi wa kati (middle -income stutus) bali ni nchi ya uchumi wa kati wa chini (lower middle- income status)

Nadhani unatakiwa kujiridhisha katika madai yako kwanza mkuu.

Ukweli ni kwamba kwenye "uchumi wa kati" ndani yake kuna madaraja (categories) yaani uchumi wa kati wa chini na uchumi wa kati wa juu (lower middle na upper middle mtawalia)...
Hapa nimekuelewa vizuri. Kwa maana hiyo lower & upper middle countries zipo sawa na middle income countries kiuchumi?. Sasa kwa nini tusiambiwe uhalisia kwamba sisi ni lower middle income au ndo ile aliyepata one na aliyepata two wote wamefaulu. Kwamba Tz tupo sawa na Brazil kiuchumi.
 
Hapa nimekuelewa vizuri. Kwa maana hiyo lower & upper middle countries zipo sawa na middle income countries kiuchumi?. Sasa kwa nini tusiambiwe uhalisia kwamba sisi ni lower middle income au ndo ile aliyepata one na aliyepata two wote wamefaulu. Kwamba Tz tupo sawa na Brazil kiuchumi.

Tanzania tupo uchumi wa kati. Kuwa uchumi wa kati wa chini au wa kati wa juu bado ni uchumi wa kati.

Kama umeelewa hapa, ni jambo la kushukuru.

Kama unao uhakika kwamba kuna mtu alikwambia kwamba Tanzania ipo "uchumi wa kati wa juu" huyo alikudanganya. Ila sikumbuki Kama hii imewahi kuelezwa popote.

Lakini kama mtu alikwambia tu kwamba Tanzania ipo uchumi wa kati, hawezi kuwa alikuongopea.

Kusema uchumi wa Tanzania na Brazil unalingana, mmmh sijui umefikiria nini kuuliza hivi.
Ila nadhani mtu yeyote yule atakujibu kwamba uchumi wa Brazil ni mkubwa kuliko wa Tanzania.
 
Halafu for the records, benki ya dunia WORLD BANK ndio inalotoa hizo ranks.

Taasisi hiyo haioni haya wala haiogopi kuiweka Tanzania kwenye nchi masikini zaidi Duniani kama inastahili kuwapo hapo.

Kama Tanzania imewekwa kwenye nchi za uchumi wa kati, basi imestahili kwa mujibu wa vigezo vilivyopo.

Katika orodha hiyo kuna nchi zote na madaraja yake stahiki, kwahiyo nataka tuondoe hii dhana ya TUNADANGANYWA.

Unaweza uka "Google" tu na kuona, hivi vitu ni open access. Unaiona Tanzania ipo wapi kwenye "msimamo wa ligi", na sio Tanzania tu, utaiona Comoro, Shelisheli, Tunisia, Belarus, Ujerumani, Bolivia n.k kama utapenda kuzitazama.

Tanzania ipo uchumi wa kati.
Wa kati upi, wa kati wa chini.
Wa kati wa chini, ni wa kati ? NDIO.

Artificial intelligence

Screenshot_20220125-224252_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom