BIG Banned
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 262
- 71
Wale wataalam wa hii mambo, hebu tuelezeni kwanini Tanzania ipo SADC. Na kwanini nchi zingine za East Africa ( Kenya, Uganda.... etc) hazipo.
Sasa tunanufaika vipi na hiyo SADC!!Tulianza kuwa EAC ambayo historia yake ilianzia toka ukoloni,baadae ikaanzishwa rasmi 1967 na kuvunjika 1977.(nikipata muda inshallah,siku moja ntaweka jamvini historia ya EAC). SADC ilitokana na kile kilichoitwa Front Line States ktk harakati za kudai uhuru kusini mwa Afrika. Kiukweli kutoka moyoni mimi nadhani SADC ndio ndg zetu wa ukweli na tungenufaika sana na ushirikiano huo kuliko hawa jamaa zetu wa EAC wanaowaza rasilimali zetu hususan ardhi kila siku. Hebu fikiri,kwa nn nchi zote nne za EAC zinailaumu TZ kwa kukwamisha maamuzi ya EAC.
Wale wataalam wa hii mambo, hebu tuelezeni kwanini Tanzania ipo SADC. Na kwanini nchi zingine za East Africa ( Kenya, Uganda.... etc) hazipo.