Tanzania Premier League 'TPL' Simba SC Vs Singida United, Uwanja wa Taifa Dar es salaam

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea tena leo Disemba 29, 2018 kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti. Gumzo ni Simba SC kuwakabili Singida United kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Simba SC, Mnyama, Lunyasi ambao ni mabingwa watetezi wataingia katika uwanja wa Taifa wakihitaji alama tatu muhimu katika mchezo wa leo. Je Singida United wataweza kuwaruhusu kuvurumishwa na Simba SC?

Kumbuka mechi ni kuanzia saa 1:00 usiku. Usikose Ukaambiwa
IMG_20181229_151601_537.jpeg
Kikosi cha Simba SC dhidi ya Singida United kinachoanza leo hiki hapa..Jeshi la Patrick Aussems
IMG_20181229_151910_569.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app

Kabumbu liko katikati ya uwanja kuashiria kuanza kwa mchezo huu wa TPL

Naaam Mpira Umeanza Uwanja wa Taifa

Simba SC 0-0 Singida United


05' Bocco anamjaribu Ally Mustafa kwa shuti la umbali lakini anakaa vema na kudaka bila wasiwasi

Wanachukua Singida Utd kujaribu kupeleka mashambulizi, lakini wanapoteza mpira

07' Anakwenda Bocco lakini golikipa anatokea na kuharibu ile mipango yake

10' Hakuna timu imeona lango la mwezake uwanja wa Taifa TPL

Simba SC 0-0 Singida United

Singida Utd wanajaribu kupanga mashambulizi lakini, beki za Simba zinakaa imara.

15' Mpira unachezwa kwa pande zote kwa zamu ijapokuwa hakuna bao

17' Gooooooooooaaal Gooooooaaal

John Bocco anaandika bao la kwanza kufuatia pasi safi ya Kichuya ndani ya 18 za uwanja

Simba SC 1-0 Singida Utd


Simba wanazidi kuzidisha mashambulizi kuelekea Singida Utd huku wakitawala katikati

23' Goo la la laaaaaaa, Kichuya anashindwa kumalizia mpira uliorudi kufuatia shuti la Bocco. ilikuwa hatari

29' Go laaa laaa..Cleoutus Chama anapiga shuti la umbali mrefu na kupanguliwa na golikipa Ally na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda

30' Simba SC 1-0 Singida United

La la la Habib Kiyombo anashindwa kumalizia mpira wa Krosi ilikuwa nafasi nzuri kusawazisha bao

34' Singida Utd kwa mara nyingine wanakosa bao, baada ya shuti kupanguliwa na Ally Mustafa

35' John Bocco anapiga kichwa. Lakini mpira unatoka nje na kuwa gooal Kick

40' Kipute cha TPL uwanja wa Taifa Simba bado anaongoza bao moja

Singida Utd wanatengeneza mashambulizi lakini safu yao haijaleta matunda kuweza kusawazisha

Bocco anakosa bao lingine la wazi kwa shuti lake kutoka nje na kuwa gooal Kick, ilikuwa hatari lango la Singida Utd

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Taifa

Naaaaaaaam kipindi cha kwanza kimekamilika ambapo Simba wanatoka uwanjani wakiwa mbele ya goli moja bila dhidi ya Singida Utd


Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Taifa katika TPL, hakuna mabadilko kwa sasa kwa pande zote

Simba SC 1-0 Singida United

49' Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal
Kichuya anaipatia Simba bao la pili ni pasi safi kutoka kwa Cleoutus Chota Chama

Simba SC 2-0 Singida Utd


Anakwenda kwa Obina upande wa Singida lakini wanashindwa kutulia eneo 18

55' Gooooooooooaaal kwa mara nyingine tena Shinza Ramadhan Kichuya anaandika bao la tatu..Kazi nzuri ya Cleoutus Chama 'Triple C'

Simba SC 3-0 Singida United


63' Simba wanakataliwa bao baada mpira kuingia wavuni. Mpira ulipigwa na Bocco

68' Anatoka Nicholas Cyan, anaingia Zana Coulibaly..Upande wa Simba

Kandanda safi linatandazwa hapa uwanja wa Taifa. Simba wanatakata

71' Simba SC 3-0 Singida Utd

Mpira unakwenda mbele ya lango Singida katikati uwanja Simba wanazidi kutawala mchezo

80' Singida wanacheza vizuri wakiwa na utulivu eneo kati

86' Okwi anakosa nafasi nzuri ya kuandika bao la nne hapa

Simba SC 3-0 Singida United

Kwa dakika hizi sidhani kama Singida wanaweza kufanya maajabu

90+3' Wakati wowote mpira utakuwa umemalizika

Naaaaaaaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa katika TPL ambapo Simba SC wanaibuka kwa ushindi mnono wa mabao matatu bila majibu dhidi ya Singida United, Shiza Kichuya akifunga mabao mawili na kusaidia moja.

Simba SC 3-0 Singida United

Asanteni..

Ghazwat..
 
Back
Top Bottom