Tanzania opposition laments its ‘naivety’ over president as repression intensifies

Tanzania opposition laments its ‘naivety’ over president as repression intensifies

8 Desemba 2024

DOKUMENTARI : WAZIMU UNAOLETWA NA MADARAKA

Kurunzi kumulika : Utawala na dola zinavyopofusha uono wa kiongozi aliye madarakani


View: https://m.youtube.com/watch?v=Qj6lSxAbxEY

Hii ni hadithi ya mtu mwenye nyuso mbili. Daktari Bashar ambaye ni mwoga, ambaye kwa muda mrefu ameshawishi nchi za Magharibi na kuahidi kuipeleka nchi yake kuelekea kwenye demokrasia zaidi.

Na Bwana Assad mbaya, dikteta, ambaye anapigana na watu wake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na mamia ya maelfu ya wahasiriwa.

Bwana Assad wa kutisha, dikteta ambaye anapigana na watu wake. Magenge ya kiMafia. Na ma-godfathers wake, machawa kuchonga sifa zake, na pia mabilioni yake katika fedha chafu.

Bashar El-Assad alipokea Syria kama urithi kutoka kwa babake, Hafez El-Assad. Yeye ndiye aliyejenga udikteta huu wa chuma ambao umeshikilia nchi kwa karibu miaka 50. Filamu pia inachunguza uhusiano wa shauku unaounganisha Ufaransa na Syria. Viongozi wakuu wa kisiasa wa Ufaransa, mawaziri na wanadiplomasia wa zamani, wanatuweka nyuma ya pazia la uhusiano huu wenye misukosuko.

Uhusiano ambao hadithi ya Bashar El-Assad inaashiria kikamilifu. Marais wa Ufaransa Jacques Chirac na kisha Nicolas Sarkozy hapo awali walimwona kama mshirika wa thamani na wakamtengenezea zulia jekundu. Kabla ya kujuta kwa uchungu. Dokumentari Iliyoongozwa na Christophe Widemann
 
Makala ya Kimataifa by Carlos Mureithi wa:
Gazeti tajwa kimataifa la The Guardian

09 December 2024

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa karibu, akitabasamu akiwa amevalia hijabu ya zambarau.


Upinzani Tanzania walalamikia ‘ujinga’ wao dhidi ya kumuamini rais na kauli mbiu yake ya 4R huku ukandamizaji ukizidi​

Mauaji ya hivi majuzi na kukamatwa kwa wakosoaji wa serikali yanaonesha kufikia tamati kwa mbinu ya mageuzi ya 4R chini ya Samia Suluhu Hassan, wasema wapinzani wa kisiasa


Wakati Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani kama rais wa Tanzania mwaka 2021, wengi katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki walipongeza kile walichotarajia kuwa ni pambazuko jipya baada ya kiongozi huyo wa kimabavu. utawala kandamizi wa mtangulizi wake John Pombe Joseph Magufuli.


Dalili zilikuwa chanya katika miaka yake michache ya kwanza madarakani: Rais Hassan alikomesha marufuku ya magazeti na mikutano ya kisiasa, na sheria ambayo iliwazuia wasichana wajawazito na kina mama wachanga kutokwenda shule, sera zote ambazo Magufuli alikuwa ameidhinisha.

Lakini viongozi wa upinzani wanasema mauaji ya hivi majuzi ya viongozi, msururu wa kutoweka, na kutiwa mbaroni kwa wakosoaji wa serikali na kupigwa marufuku kwa mikusanyiko ya upinzani kunapendekeza kumalizika kwa mtazamo wa mageuzi.


Mwishoni mwa Novemba 2024 chama cha upinzani cha Chadema kilisema wanachama wake watatu waliuawa katika matukio yanayohusishwa na chaguzi za ndani, ambazo chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi kilishinda kwa kishindo cha asilimia 99.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema kwenye mtandao wa X kwamba mgombea mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania, Dar es Salaam, alipokuwa akijaribu kuzuia kura “feki na batili” kuwasilishwa kwenye kituo cha kupigia kura.
Tundu Lissu karibu, amevaa miwani, akitabasamu.

Picha maktaba: Tundu Lissu. Tundu Lissu amesema matarajio ya chama chake cha upinzani Chadema kuhusu uhuru wa kisiasa chini ya Rais Samia Hassan 'yalikuwa kama ndoto ya kiwendawazimu, uendawazimu usio na chembe ya uhalisia '. Picha: Virginia Mayo/AP

Chadema imesema mgombea mwingine aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake Mikese katikati mwa Tanzania na kwamba ofisa wa chama hicho aliuawa kwa kushambuliwa kwa panga nyumbani kwake Tunduma karibu na mpaka na Zambia.

Jumatatu Disemba 2, 2024 chama cha upinzani cha ACT Wazalendo kilisema kiongozi huyo wa tawi la vijana maarufu kama Ngome ya Vijana amepatikana akiwa hai ufukweni mwa bahari ya Hindi maeneo ya makaazi ya vigogo wa serikali, matajiri na mabalozi eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam akiwa na majeraha mabaya baada ya kutekwa nyara. Chama hicho kilidai kuwa Abdul Nondo "alitekwa nyara" Jumapili asubuhi na watu ambao waliamini kuwa walikuwa maajenti wa usalama wa serikali. Polisi walisema uchunguzi unaendelea kubaini waliohusika.


Vifo hivyo vinafuatia kuuawa Septemba mosi 2024 kwa mjumbe wa sekretarieti ya Chadema ambaye alitekwa ndani ya basi la abiria kisha kuburuzwa kutoka katika chombo hicho cha usafiri wa kwenda mikoani, asubuhi siku inayofuata alikutwa amepigwa na kumwagiwa tindikali usoni. Hakuna ushahidi kuwa rais Hassan amehusika katika vifo hivyo ambavyo vimekemewa na serikali.


Katika mahojiano na gazeti tajwa kubwa la Uingereza The Guardian , Tundu Lissu, kiongozi mwingine wa Chadema, alisema, kwa manufaa ya mtazamo wa nyuma, matarajio ya chama chake kuhusu uhuru wa kisiasa chini ya Hassan “ni kama ya ndoto ya kiwendawazimu , ndoto isiyoweza kutekelezeka”.


Lissu, makamu mwenyekiti wa chama hicho CHADEMA , alishika nafasi ya pili dhidi ya Magufuli katika uchaguzi wa urais wa 2020 na anatarajiwa kujitosa tena kugombea kiti cha urais wa Jamhuri katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani 2025. Kama ilivyotokea kwa mwenyekiti Freeman Mbowe, Lissu naye amekamatwa mara mbili katika miezi michache iliyopita.
Polisi wenye silaha, wengine wamevaa helmeti, mitaani

Picha : Polisi wa Tanzania wakizuia maandamano ya upinzani, yaliyopigwa marufuku kufanyika jijini Dar es Salaam mwezi Septemba 2024. Picha: Anthony Siame/EPA

Lissu alisema upinzani ulikuwa "wajinga" kwa kufikiria rais Hassan angeleta mabadiliko na walipaswa kumshinikiza zaidi kufanya mageuzi ya kina ya kikatiba, kisheria na kitaasisi.

Alisema: “ Samia Hassan alirithi mfumo dola wa serikali ambayo iliundwa na Magufuli na ambayo ilihusika na ukandamizaji ambao tulipitia kwa miaka sita. Tungewezaje kufikiria kwamba, kutokana na zigo lote hili la mfumo dola kandamizi , huyu Samia Hassan angekuwa mpenda mageuzi?”


Mwanaharakati mpigania demokrasia, haki za binadamu na kupambana na rushwa, Tundu Lissu alipigwa risasi 16 katika jaribio la mauaji mwaka 2017 ambalo lilimlazimu kuishi uhamishoni nchini Ubelgiji kwa miaka mitano. Hakuna aliyeshitakiwa kwa jaribio la kutaka kumuua Lissu. Mnamo Septemba 2024, mfanyakazi wa zamani wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo aliiambia mahakama ya London kwamba kampuni hiyo iliipatia serikali ya Tanzania data za simu za Lissu wiki kadhaa kabla ya kupigwa risasi.


Samia Hassan, ambaye alikuwa makamu wa rais chini ya Magufuli na kumrithi baada ya kifo chake, alifanya baadhi ya hatua za maridhiano na upinzani uliozimwa miezi kadhaa baada ya kushika wadhifa huo, na kufuta mashtaka ya ugaidi dhidi ya Freeman Mbowe na kumwachia huru baada ya kukaa kizuizini kwa miezi kadhaa, na kukutana na Lissu huko Brussels.Ubelji , ambapo alikuwa uhamishoni. Hatua hizi za mapicha picha na wapinzani zilimpa rais Samia Hassan kupata uungwaji mkono kisiasa wa ndani na kimataifa.


Hata hivyo, matukio ya miezi michache iliyopita yamezusha hofu ya kurudi kwa kutovumiliana. "Samia Hassan amefanya ugandamizaji kwa tabasamu kama alichokifanya Magufuli kwa mbwembwe," alisema Lissu. "Magufuli alifanya hivyo kwa furaha . Hakuwa na silika kujifanya. Ila Samia Hassan anafanya mambo yale yale, lakini anayafanya kwa tabasamu lile la mama mwenye huruma.”

Miongoni mwa waliopotea ni Deusdedith Soka, kiongozi wa vijana wa Chadema (30) ambaye alitoweka mwezi Agosti baada ya kuitisha maandamano ya kupinga utekaji nyara.

Mjomba wake Didas Soka alisema siku ambayo Deusdedith alitoweka, mtu aliyejitambulisha kuwa ni askari polisi alimpigia simu kumtaka aende kituo cha polisi.


Didas Soka kusema: “Deus alikuwa akipigania mageuzi ya katiba kwa ajili ya nchi bora na mifumo bora ya utawala. Tunawezaje kuwa na imani ikiwa ametoweka wakati wa kupigania hilo?” Baadhi ya waliotoweka wameibuka wakiwa hai, mfano Edgar Mwakabela almaarufu kama Sastiva , mwanaharakati mwenye umri wa miaka 27 aliyetekwa nyara mwezi Juni na kupatikana akiwa ametelekezwa siku nne baadaye katika hifadhi ya taifa akiwa na majeraha ya risasi na dalili za kuteswa.


Mwakabela, maarufu kwa jina la Sativa, alisema waliomteka walimtesa katika kituo cha polisi na kumhoji kuhusu jukumu lake la kuandaa mgomo wa wafanyabiashara dhidi ya kile walichoona kuwa ni kodi na ada nyingi.

Mwakabela alisema matukio ya aina hiyo yalikuwa na lengo la kuwatia hofu watu kabla ya uchaguzi wa urais. "Ni sehemu ya kuwafahamisha watu kuwa anaongoza na kuwatia hofu wale ambao watajaribu kushindana naye katika uchaguzi," alisema.


Gazeti la The Guardian limewatafuta wasemaji wa polisi na serikali ili kutoa maoni yao.
Katika kujibu tamko la pamoja la balozi za nchi za magharibi mnamo Septemba kulaani ripoti za ghasia na kupotea na vifo vya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu, rais Hassan alionya dhidi ya "kuingilia" masuala ya ndani ya Tanzania. Alisema: "Ni jukumu letu wenyewe kujua ni kwanini yanatokea kwa wakati huu."


Chama cha rais Hassan, CCM chama kongwe dola, kimeiongoza Tanzania tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1961.

Upinzani na jumuiya ya kiraia AZAKI mara kwa mara wamekuwa wakitaka marekebisho ya katiba ambayo yaliundwa kwa ajili ya kuunga mkono mifumo ya kimabavu ya serikali ya chama kimoja. Lakini Rais Hassan amesema mabadiliko yatafanyika baada ya uchaguzi wa urais 2025.

Naye wakili wa haki za binadamu, Tito Magoti, alisema rais Hassan alikosa nafasi ya kujenga taasisi za kidemokrasia zitakazolinda haki za binadamu na kuruhusu wananchi kushiriki katika serikali. "Ilikuwa ni fursa iliyokoswa ambayo hatimaye imefanya serikali ionekane kama mfano wa kile John Pombe [Magufuli] alifanya," alisema.


Rais Samia Hassan aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2000 wakati CCM ilipomteua kwa kiti maalum katika baraza la wawakilishi la Zanzibar. Akiwa naibu wa zamani wa Magufuli na ambaye amelelewa kisiasa kupitia mfumo wa CCM, nia yake ya msingi ilikuwa "kuhakikisha CCM inasalia", alisema Aikande Kwayu, mchambuzi wa masuala ya kisiasa. "Uchaguzi unapokaribia, sasa tunamwona yeye katika uhalisia wake Samia Hassan, na tunaendelea kutambua kwamba mabadiliko yoyote aliyokuwa akizungumzia ikiwemo 4R yalikuwa ya urembo tu," alisema.


Licha ya matukio ya hivi karibuni, Lissu bado ana matumaini kuhusu mabadiliko. "Ninabaki na matumaini kwamba tutapata aina ya Tanzania ambayo tunastahili," alisema. "Hata hivyo, niongeze kwamba haitakuwa rahisi. Utawala wa Tanzania umekuwa madarakani bila usumbufu wowote tangu uhuru miaka 63 iliyopita. Wamejichimbia mizizi na hivyo kungoa kisiki na mizizi inaweza kuwa kazi ngumu lakini inawezekana kama vile mkulima anapojitolea kutengeneza shamba jipya bora.
Well written report. Suppression methods used by Gov. Is very dangerous; abduction and killing the opposition is not good. That shows all promise of reform from Gov is just false,
 
Back
Top Bottom