Ni hatari ambayo hata ccm yenyewe hamkuitambua hatari hii sio nyingine bali ni anguko la ccm na serikali yake. Anguko hili la ccm, si la bahati mbaya bali ni kusudio lao kabisa,kama hawajui basi naweza kusema wahalijui wala hawakulitambua kwa kuwa na fikra mgando na uvivu wa kufikiri.
Kama kawaida ya ccm,wao hufanya siasa kwa matukio.Hii ni hataari sana,na ndio anguko kuu la ccm.Baada ya kuona chadema ikivuma na kuungwa mkono na vijana hususani wasomi,ccm bila kufanya utafiti hata wa kutumia akili ndogo walijiachia kichwa kichwa kufuata mkumbo.
Hii ilipelekea kupigwa chini kwa mzee makamba,baadae mukama,huku wakiweka vijana akina Nape na Mwigulu wakidhani kuwa wataungwa mkono. Badala yake tunashuhudia anguko kubwa la ccm.Hili ndilo KOSA KUBWA AMBALO CCM WALILIFANYA NA NDIO CHANZO CHA ANGUKO LA CCM.
Huwezi kuweka vijana wote kwenye siasa ambao ni wachanga ambao hakuna hata mmoja mwenye historia ya kuwa na wadhifa katika chama.Nafasi hizi zilifaa kuchukuliwa na akin Nchimbi waliokaa kwenye chama wenye uzoefu.
Siasa za majitaka zinazofanywa na Nape na Mwigulu haziwezi kushindana na chadema kamwe.Kama kawaida ya ccm kukurupuka,walipoona chadema inaungwa na vijana wengi hawakuwa na budi ya kuwaweka hawa vijana.
Baada tu ya kuwekwa kwa hawa vijana,ndipo tumeanza kushuhudia sera za udini,ukabila na ugaidi kitu ambacho katika vipindi vya akina Makamba jambo kama hili halikuwepo,kwani walijua athari ya haya yote.
Tumeshuhudia mauaji ya watu huko Arusha,yakitanguliwa na kauli ya Mwigulu ya kuwa WATU WA ARUSHA MSIPOICHAGUA CCM HAKIKA MTAKUFA.
Wananchi wanajua kipi kibaya,kipi kizuri,kwa hiyo msitumie sera za zamani za kudanganya watu siku hizi watu wana reason and they are rational in decision making.Kwa hiyo,kauli ya Nchemba na zingine nyingi kama za akina Pinda,Nape,Lukuvi,wassira nk.Wananchi wanajua kuargue.
Na daima chadema itaungwa mkono na wananchi hata kama mtasema nini,keep in your mind that people are rational in making decisions.
Na hakika kauli zote za kipuuzi wananchi wanajua,ccm msiwafanye wananchi kuwa ni wajinga,they know make arguments zipi ni hoja na zipi ni propaganda.
Kama kawaida ya ccm kufanya siasa za matukio,mwaka 2010 wakati Dr Slaa anagombea urais walizusha mambo mengi sana juu ya ndoa yake.Lakini haya yote yaliishia wapi? Wananchi wanahoji!kama sio uzushi ni nini?
Ccm mjitathimini,chadema sio saizi yenu,mtatafuta mchawi,mtafanya kila aina ya uzushi,uovu lakini wananchi wanajua mbivu na mbichi.Mwisho wenu umefika,mmejiloga wenyewe.