Tanzania ni miongoni mwa nchi chache sana ktk bara la Afrika kama sio duniani yenye Amani ambayo imedumu kwa takriban miaka 35 tangia kupaikana kwa Uhuru.
Tangia miaka zaidi ya 20 ya utawala wa Rais wa kwanza wa Tanganyika Mwl Julius K Nyerere na miaka 10 ya utawala wa rais wa pili Alhaji Hassan Mwinyi,Tanzania ilikua ni nchi ya mfano kwa Nchi za Afrika na Dunia kwa ujumla.
Baada ya Utawala wa awamu ya tatu chini ya rais mstaafu Benjamin Mkapa Amani yetu ilianza kutoweka taratibu huku tukishuhudia 2001 maelfu ya Wazanzibar wafuasi wa CUF wakiuawa na Polisi kwa kisingizio cha kuandamana bila kibali. Si hivyo tu lakini matukio mengi ya hapa na pale yakitokea yakiwemo ya watu mmoja mmoja kupigwa risasi na polisi.
Utawala wa awamu ya nne wa chini ya Mh,Kikwete(CHAGUO LA MUNGU) nao ukaingia madarakani kwa NGUVU,ARI,NA KASI MPYA huku yale yale ya utawala wa tatu yakiendelezwa kwa Kasi,Ari,na Nguvu mpya.
Tofauti na tawala zote zilizotangulia utawala huu wa nne tumeshuhudia Mmomonyoko wa maadili ktk viongozi,tumeshuhudia nyufa ya UDINI ukikua kwa kiwango kikubwa hali iliyosababisha baadhi ya viongozi wa Dini kuuwawa na tumeshuhudia pia milipuko ya Mabomu ktk nyumba za ibada na ktk mikutano ya Siasa kitu ambacho hatukuwahi kukishuhudia.
Ni ktk utawala huu wa awamu ya 4 tumeendelea kuona Chombo kikuu cha kuisimamia serikali (yaani Bunge) likipoteza heshima kwa kutumika na serikali kuitetea.
Tumeendelea pia kushuhudia CCM chama tawala na chenye Serikali kikitumia Jeshi la polisi kuendelea kunyanyasa vyama Pinzani na wafuasi wake hususan CDM kwa kuwaweka Rumande mara kwa mara Viongozi na wafuasi wake na hata kuwaua,kuwajerihi na Kuwafungulia kesi za Ugaidi ili tu kuwaogopesha.
Tumeendelea kuona Chama kikuu cha Upinzani CDM kikitumia Nguvu ya Umma kwa maandamano na mikutano ya hadhara kupinga unyanyasaji wanao fanyiwa na Ccm kwa kutumia jeshi la polisi huku wafuasi wake wakipoteza maisha na wengine wakiishia kupata vilema vya maisha.
Ni miaka hii hii ya utawala wa awamu ya 4 tunashuhudia Mwenyekiti wa taifa CUF pro Ibrahim Lipumba akifanya siasa Misikitini kiti ambacho hatukuwahi kukishuhudia ktk awamu za tawala zote zilizopita.
Ufike sasa wakati Viongozi na watawala wajue kwamba Tanzania ni zaidi ya CCM,CDM na CUF. kwani kuendelea kuviruhusu vyama hivi kufanya haya wanayofanya kwa sasa ni kupoteza tunu hii ya Amani ambay inakaribia kupotea. Japo kuna wale wanao sema Tz hakuna amani ila kuna Utulivu lakini basi tuendelee kuiyenzi huu utulivu ulioko.
Ccm + Cdm + Cuf = Kutoweka kwa Amani Tz.
Mungu ibariki Tanzania!!