Tanzania ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nginda, Dec 2, 2011.

 1. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jamvi nimejaribu kujiuliza mara nyingi kuwa Tanzania ni nini???
  Kutokana na historia niliyofundishwa ni kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili ambazo ni Zanzibar na Tanganyika.
  Lakini swali linakuja, Je baada ya muungano Tanganyika ilikwenda wapi? Bona zanzibar ipo? Na hata wazanzibar wanatambua kuwa Zanzibar ni nchi? (nikumbushe kauli ya mtoto wa mkulima ambaye kiuelewa anapaswa kuuelewa muungano lakini kidogo limtokee puani baada ya kutamka kuwa Zanzibar siyo nchi).

  Je naweza kuamini kuwa baada ya muungano basi Tanganyika iligeuzwa kuwa koloni la zanzibar??

  Je leo muungano ukifa sehemu ya bara tutaiita jina gani? Nasema hivyo kwa sababu wanasiasa wanatuhadaa kuwa huu muungano ni wa nchi mbili - ni zipi hizo kwani mimi naifahamu Zanzibar lakini kwa sasa hakuna taifa linaloitwa Tanganyika. Naomba ieleweke kuwa hakuna document yeyote inayothibitisha kuwepo kwa taifa linaloitwa tanganyika zaidi ya historia ya vitabu.

  Kimsingi yapo mambo yanayotambulisha taifa .
  Bendera ya nchi
  Wimbo wa taifa
  Raisi wa nchi
  Kutoa uwakilishi wa mabalozi na mengine ambayo pengine wengi tunayaona.
  Kupigiwa mizinga
  Zaidi zanzibar wako kwenye mchakato wa kupata katiba. Vyote hivi Zanzibar vipo.

  Swali: Leo muungano ukifa Kikwete atakuwa raisi wa nchi gani? Sehebu ya bara itatumia bendera gani, katiba gani na wimbo wa taifa upi? na taifa litakalobaki litaitwa jina gani au historia itajirudia?


  Naomba kuwakilisha
   
Loading...