Tanzania ni nchi ya kodi na matumizi ya kodi?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
1,391
1,258
WanaJf, Salaam!

Nimefanya utafiti mdogo kwenye sekta ya viwanda nikagundua mrundikano wa tozo, kodi, na ushuru vinavyotozwa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kwa mfano kwa wilaya ya Bukoba mmiliki wa kiwanda cha kuongeza tofali za block hukutana na kodi, ushuru na tozo hizi:-

(i). Ushuru wa mchanga kijijini,
(ii). Ushuru wa mchanga ofisi za madini,
(iii). Ushuru wa taka halmashauri,
(iv). Lesseni ya biashara Halmashauri,
(v). Kodi ya biashara TRA,
(vi). Ushuru wa taka Halmashauri,
(vii). Ushuru wa saruji ununuapo zaidi ya mifuko 25 dukani Halmashauri,
(viii). Kodi kila uuzapo tofali,
(ix). Hapo bado kodi zinazolipiwa kwenye huduma i.e nunuzi wa vipuli, mafuta, umeme, nk nk.

Ushauri:-
Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ifanye mapitio kwenye sekta hii ya viwanda ili kupunguza utitiri wa kodi, tozo na ushuru - hizo ni mzigo kwa mfanyabiashara lkn pia kwa mlaji.

Sijui biashara zingine zikoje lkn huku ni mwisho wa matatizo.
 
KODI KIBAO na UPIGAJI wa Kasi ya 4G nyumba ya Mil.7


20210922_083456.jpg


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Dawa imeanza kuingia eh??

We si kada wa Lumumba na ndio mlimpigia upatu Jiwe! Samia ni mrithi wa jiwe , kwahiyo lao ni moja.

Mitano tena , au nasema uongo ndugu zangu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom