Tanzania ni nchi masikini sana

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Huenda uliposoma kichwa cha habari ukawa umejipanga kuja kunikosoa haraka kwamba nchi ina hifadhi nyingi za wanyama, mafuta, gesi, madini yaliyojaa tele nchini na hata kuwa na Tanzanite ambayo ipo hapa tu duniani kote, mlima kilimanjaro na vitu vingi ardhi hii iliyosheheni rasilimali.

Umaskini naozungumzia hapa ni ule mbaya kuliko wote, Nazungumzia umaskini wa maarifa, yani umaskini wa kichwani unaofanya baraka za ardhi hii kutufanya tuomekane wajinga na wasio na hizi baraka.

Hata pale napojaribu angalau kujipa matumaini kwamba kuna wahitimu walimaliza vyuo wengi naona nakosea kwa sababu hata elimu ya huko vyuoni ni elimu ya kukariri na hata kutoa rushwa na michezo mingine michafu ili mradi tu mtu awe na cheti na kwa tathmini niliyoifanya baada ya kuhitimu vyuo watanzania wengi hawana muda tena na elimu, kwa kifupi hawaiihitaji elimu na maarifa kwa sababu ya kuwa na kiu ya maarifa bali ni kwajili ya cheti tu mradi mtu ajulikane tu ana degree, masters, ni profesa, n.k kwa lengo la kuajiriwa na wengine kuwaza jinsi watavyoiba kwa kupokea rushwa.

Mbaya zaidi maarifa haya katika elimu ni ya kikoloni sana, elimu tuliyoachiwa na mkoloni tunaendelea nayo hadi leo na nikiri tu ya kwamba hii elimu ilibuniwa ili iwe inatupoteza ukijumlisha na watu wanavyogeuza maneno takatifu yazidi kutufanya kupotea ndio kabisa, mfano nakumbuka shuleni tulisisitiziwa sana mstari moja wa biblia kwamba "usimwache elimu aende zake" basi karibu kila mtu akawa anadhani elimu inayozungumziwa ni ya darasani ile ya kusoma historia yetu iliyoandikwa na mzungu alietuficha vitu vingi, kujua kuandika meseji za maneno matatu kwa njia ya fax katika kizazi hiki ambacho fax sio kitu, mwanafunzi kuingia form one na kusoma masomo tisa, n.k.

Na wakati huo huo tunapima akili kwa kipimo cha darasani kwamba nani ana alama nyingi huku tukisahau kabla ya elimu hii mababu zetu walikiwa pia wana akili bila hata hii elimu (common sense)

Mtu ana PHD kwenye cheti lakini hata kiingereza kinampiga sarakasi si kitoto na hapo ndo naamini kwamba yaelekea alikariri tu kujibu kiingereza cha kujibu mtihani ili apate cheti tu hakuwa na kiu ya marifa, Mtu ni profesa wa uchumi lakini yeye nje ya mshahara wake mradi alionao ni mbuzi 3 na ngombe 2 na vikuku huko kwao kijijni na ndie anaeweza kuwa mshauri wa nchi kwenye mambo ya uchumi huyu 🙄.

Wenzetu mtu hata akimaliza chuo anajiendeleza kuongeza maarifa na ndio maana si ajabu kukuta nyumba za wenzetu huko nje kuna library kabisa na anaweza akawa ameweka bajeti ya kununua vitabu kila mwezi, kwa huku mtu akimaliza chuo ndio imeisha hio hnaa haja tena ya kushika kitabu maana anachojua ni kusomea vyeti tu.

Kwa hali hii niseme tu ya kwamba ardhi yetu ya Tanzania ndio ina mali asili kibao tu lakini watu wanaoishi kwenye hii ardhi wameyapuuza maarifa na matokeo yake ndio aibu, maana wenzetu wanatushangaa sana nchi inakiwaje maskini hivi wakati rasili mali zimerundikana.

Kwa mfano mdogo tu, mlima kilimanjaro upo Tanzania lakini wenzetu hapo kenya wanachoweza kufanya ni kuuona tu "view", wazungu wengi sana wanaenda hapo kuuona mlima huo kwasababu wamejiongeza kidogo tu kujitangaza, Kwa hapa Tanzania nilishangaa sana waziri wa utalii alipotumia wasanii hawa wa bongo movie kina steve nyerere na kuwalipia hoteli za bei kali eti ndio watangaze vivutio, nikaona hapa tatizo ni maarifa tu.

Pia kulikuwa na mnunuaji mkubwa wa madini ya tanzanite alienda hadi india kuona mgodi wa tanzanite, La Haula! hakuamini alichokiona kwamba kumbe mgodi upo tanzania ila wahindi ndio wauzaji wakubwa.

Ningependa mno hii nchi tuache ujinga wa kujisifu kwamba nchi ni tajiri wakati vichwani kuna umaskini mkubwa mno, Walimu wawe nguzo kuu ya taifa na hata mfumo huu wa elimu uboreshwe.
 
Wewe umeifanyia nini hii nchi? hujui huko mererani kuna watu wengi sana wamefilisika kwenye biashara ya madini? huyo laizer mwenyewe alifilisika hata uwezo wa kuhudumia mgodi akawa hana akatafuta wafadhili
 
Mkuu sorry Kama nimewahi kucoment kabla ya kumaliza kusoma,nadhani maarifa si ya kikoloni bali mfumo wa elimu yetu na wakikoloni anaozalisha watu tegemezi
 
Ndoto zetu wengi ni kuajiliwa au kujiajiri, kujenga nyumba ya kujiegesha, kumiliki usAfiri, kuoa, kufa.

Hatuna muda ya mapinduzi ya viwanda, hatuna muda wala akili ya mapinduzi ya teknolojia. Kila siku wenzetu wanafanya vumbuzi nyingi tofaut tofaut. Sis mabongo lala tumeahidiwa utajiri wetu upo mbinguni tumeandaliwa majumba, magari na wanawake wazuri....
 
Nadhani Kama nchi tumekosa vitu vitatu.1.akili mkichwa 2.viongozi Bora (3) Elimu Bora.

Kama watu incompetent Kama akina magu ndo wanapigiwa chapuo,Kuna nini tena hapo
 
Nadhani Kama nchi tumekosa vitu vitatu.1.akili mkichwa 2.viongozi Bora (3) Elimu Bora.
Kama watu incompetent Kama akina magu ndo wanapigiwa chapuo,Kuna nini tena hapo
Viongozi wamekaa kiuoigaji tu,, kiongozi wa afrika anaiba mabillion kwao anaenda kuyaficha benk za ulaya kunufaisha wazungu.. wanatia aibu sana.
 
Back
Top Bottom