PreGE2025 Tanzania ni mali ya nani?

PreGE2025 Tanzania ni mali ya nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
529
Reaction score
1,494
Hii serikali ya Tanzania imekuwa ikituzarau! Tume ya Uchaguzi ni chombo kinachopaswa kuwa huru kabisa—lakini leo hii, ni kama idara ya chama tawala! Tunawauliza:

1. Kwa nini Rais, ambaye ni mshiriki wa uchaguzi, awe na mamlaka ya kuteua Mwenyekiti wa Tume? Huu siyo mgongano wa maslahi?

2. Kwa nini Tume haijawahi kutoa matokeo yanayopingana na maslahi ya chama tawala?

3. Kwa nini vyama vya upinzani havina uwakilishi wa maana katika Tume?

4. Kwa nini hatuna utaratibu huru wa kushirikisha wananchi kwenye mabadiliko ya sheria za uchaguzi?

Huu ni mzaha na mchezo mchafu dhidi ya demokrasia! Watanzania si wajinga—tunataka Tume huru, siyo wakala wa CCM!
 
Tanzania ni mali binafsi ya viongozi wakuu wa ccm na vibaraka wao.
 
Back
Top Bottom