Tanzania Nchi Yangu

Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
18,119
9,049
Tanzania nchi yangu, yenye uso wa kung’aa,
Afrika na Ulimwengu, sifa tele tapakaa,
Wahindi nao wazungu, hakuna wa kuhadaa,
Jinsi ilivyo sifika, kwa uongozi thabiti.

Ilijulikana pote, Tanzania ya mwalimu,
Iliheshimu yoyote, aliyependa nidhamu,
Kaunda naye Obote, na asiye kichwa ngumu,
Tanzania ya mwalimu, nchi yenye msimamo

Umoja wetu wa ndani, kamwe hukutisika,
Utaifa akabuni, ukabila kufutika,
Akaipa uthamani, ikawa ya kutuka,
Ndivyo ilivyosifika Tanzania nchi yangu.

Akatua madaraka, ili kuipa uwezo,
Maendeleo haraka, demokrasia kigezo,
Yeye kote akawika, kwa hizo zake sifazo.
Mwalimu akang’atuka, kutuachia mfumo

Nini kimetetereka, hata kufikia hapa,
Rushwa imetuchakaza, sasa tunatapatapa,
Viongozi wasowaza,kula fujo kama papa,
Nchi inaharibika, rushwa tele zimejaa.

Tamaa iso kipimo, ya mali na madaraka,
Viongozi waliomo, utajiri wa haraka,
Wamelisahau somo, mambo yameharibika,
Tunatengeneza bomu, ambalo litalipuka,

Bomu litaja lipuka, kwa kukosa msimamo,
Watu wataja wehuka, wakijua yaliyomo,
Tubadilike haraka, rushwa iwe na kikomo,
Bado tunaweza fika, salama bila madhara

Uongozi ni kigezo, kile kinahitajika,
Kutujengea uwezo, tuweze tena sifika,
Kwa siasa na michezo, popote tutaja fika,
Turudishe tunu yetu, ili kuongoza vema.

Tusione vyaelea, tukasahau vyaundwa,
Mwalimu kapigania, wetu uhuru kulindwa
Malengo alifikia, maadui wakashindwa
Tanzania iling’aa , pande zote za dunia.

Tujichunguze makini, tujue nini tatizo,
Tuache huu uhuni, tunaleta machukizo,
Tatizo lipo jamani, tutatue kwa mawazo,
Tanzania tufanyaje, kuboresha yetu hali
 
Nipe kalamu nishike, nimjibu Ndahani,
Niseme nieleweke, nijenge hoja makini,
Ya kwangu niyaandike, ya Tanzania jamani,
Wameshindwa kuongoza, sasa wanatuburuza!

Vile vinavyoelea, hivyo kweli vimeundwa,
Sasa tunakodolea, jinsi gani wameshindwa,
Tumebaki kuzomea, viongozi wanapondwa,
Wameshindwa kuongoza, sasa wanatuburuza!

(litaendelea..)
 

Shairi zuri. lakini unaongolea nini Bwana, Tanganyika au Tanzania. Acha kujizonga!! -nashauri katika shairi lako kila penye neno Tanzania futa na weka Tanganyika.
 
Tujichunguze makini, tujue nini tatizo,
Tuache huu uhuni, tunaleta machukizo,
Tatizo lipo jamani, tutatue kwa mawazo,
Tanzania tufanyaje, kuboresha yetu hali

Tatizo sisi wenyewe, nakukumbusha Ndahani
Wengi wetu kama mwewe, hasa walio chamani
Wanapatwa na viwewe, wawapo madarakani
kutochagua vilaza, mwanzo mzuri nasema!
 
Shairi zuri. lakini unaongolea nini Bwana, Tanganyika au Tanzania. Acha kujizonga!! -nashauri katika shairi lako kila penye neno Tanzania futa na weka Tanganyika.

Mbona na wewe paka hueleweki ?Tanganyika ndio nini?juzi tu hivi kiongozi wetu Mr seif bin khatib aliweka wazi kuwa hakuna Tanganyika wala Zanzibar ni TANZANIA ,hivi wengine huwa mnatia (weka)pamba za masikio pale viongozi wetu wanapohutubia?
 
Back
Top Bottom