Tanzania: Nchi inayo ongozwa kwa nguvu ya migomo

Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,481
564
kila mahali utasikia kuna mgomo kule ama huku na kuna baadhi ya maeneo migomo ya wananchi haiwekwi wazi angalia baadhi migomo hii
  • kigoma - wananchi wanagoma kupandishiwa ushuru ili hali huduma ni mbovu (RFA jana)
  • Walimu wanajiandaa kugoma nadhani kesho wanaanza mgomo rasmi
  • kisa cha madaktari kinajulikana
  • Ndaga, Mbeya mgomo wa kupinga ongezeko la ushuru hii ilikuwa juzi tu

IMG_0004.JPG
Je, tutafika salama kwa mwendo huu na nini kifanyike?
 
IMG_0007.JPG

kinacho nishangaza baada ya mgomo mara nyingi ndiyo mambo hukaa vema kulingana na matakwa ya wananchi

"je, migomo ndiyo suluhu kwa kila tatizo china ya utawala bora na serikali sikivu tuliyo nayo"
 
Leo nimeamini hii seeikali bila mashinikizo maandamano na migomo viongozi wanajisahau.
Kumekuwa na kelele za muda mrefu za madereva serikali ilikaa kimya na kufanya matisho kwa kutumia polisi bughudha za kutosha ati Waziri ndio anatoa tamko.
Turudi kwa wafanya biashara serikali inaendelea na ubabe bila kufikiria migomo yao inapotezaje mapato.
Tumeona bungeni wabunge wenye qeledi wanapinga sheria kandamizi Ccm wanazipitisha.
 
Dr Slaa aliposema nchi haitatawalika hawakutaka kumwelewa! Sasa watamwelewa tu!!
 
Leo nimeamini hii seeikali bila mashinikizo maandamano na migomo viongozi wanajisahau.
Kumekuwa na kelele za muda mrefu za madereva serikali ilikaa kimya na kufanya matisho kwa kutumia polisi bughudha za kutosha ati Waziri ndio anatoa tamko.
Turudi kwa wafanya biashara serikali inaendelea na ubabe bila kufikiria migomo yao inapotezaje mapato.
Tumeona bungeni wabunge wenye qeledi wanapinga sheria kandamizi Ccm wanazipitisha.
hivi karibuni serikali imekuwa ikijitengenezea precedents mbaya sana. Hivi ni kweli kabisa kwamba vyombo vya serikali vilishindwa ku scan environment juu ya huu mgomo na kuishauri serikali itoe tamko jana na kuzuia hii aibu? Hali inakuwa tete, waziri anaenda anasema tamko la mkuu wa NIT si tamko la serikali bali tamko lake mwenyewe. Serikali ingeyasema haya jana kusingekuwa na haja ya kutokea yote yaliyotokea.
 
Back
Top Bottom