Tanzania Nakupenda Sana

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
TANZANIA NAKUPENDA SANA.

Mama Tanzania, nakupenda sana,
Nakupigania, usiku mtana,
Zitaangamia, husuda fitina,
Za walo pania, watu kuchinjana
Nakupenda sana, wangu Tanzania.

Siwati kulia, tunapo zozana,
Huomba Jalia, tupate patana,
Tusiwape ndia, wafanya hiyana,
Wapate kimbia, wasirudi tena.
Nakupenda sana, wangu Tanzania.

Siasa ni njia, ya kuongozana,
Katu si jambia, roho kutoana,
Yataka sikia, kushauriana,
Mambo hutimia, kwa kusikizana.
Nakupenda sana, wangu Tanzania.

Ninajivunia, kuwa wako mwana,
Katika Dunia, hata kwa Rabana,
Mi husimulia, Ulaya na China,
Mola kajalia, vitu vingi sana.
Nakupenda sana, wangu Tanzania.

Dotto Rangimoto Chamchua (Njano5)
0622845394/0784845394 Morogoro.
 

Attachments

  • TANZANIA..jpg
    TANZANIA..jpg
    7.1 KB · Views: 76
Twataka kutulia,katu si kupigana
eeh mola jaalia,wanasiasa wache sigana
mengi twawavumilia,lakini hawana hiyana
nchi watatuchafulia,tukose vyote vyamana
 
Shairi zuri message nzuri. Wanaoandika na kupost upuuzi halafu wanafikiria wakati kile kilichoandikwa kimeshasomwa, hawawezi kuelewa mantiki ya shairi hilo. Wakati mwingine shairi ni sawa na sala ya wazi, kwani hilo wazo ungeweza kubaki nalo moyoni lakini umeona ni kheri likasomwa na watu.
 
Vizuri nafurahia lugha ya Kiswahili kwa kuyasoma. Ila yananikumbusha kutotaka kusikia mwalimu anatoa testi au mtihani wa kuyaandika haya nikijua yakija itabidi tu yaandikwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom