Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,284
KUKUPA TENA SAHAU!
1.
Ulinidharau wangu, maudhi kunitendea,
Na ule wivu mwenzangu, siwezi kukurejea,
Kutonesha donda langu, kiumbe umezoea,
Fahamu nina matungu, yote sitaelezea.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
2.
Nimezipata salamu, na barua zako pia,
Haina kazi kalamu, na wino ulo tumia,
Kusalimu si muhimu, ila sitakununia
Hujatubu nafahamu, makosa utarudia
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
3.
Sio mwezi ufahamu, ni wiki tumeachana,
Nina akili timamu, najua wataka tena,
Unaukosa utamu, wa usiku na mtana,
Umeshapata wazimu, nakwambia hutopona.
Umekuimbuka ndizi, kukupa tena sahau
4.
Utulivu si hisani, jua hauji wenyewe,
Kila mvuna tufani, pepo kapanda mwenyewe,
Tafuta mwenye imani, mie naomba nituwe,
Lala pako kitandani, rasini mwako nitowe.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
5.
Leo waniangukia, na kesho waendelea,
Mimi kulia kulia, ndio ulo yazoea,
Mja ulidhamiria, ushenzi kunitendea
Niwache nimetulia, kifo 'sije niletea.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
6.
Magoti wanipigia, kiumbe wata utani,
Acha kuyafikiria, tulofanya maishani,
Silitaki neno dia, ukome kunita hani,
Nishapata maridhia, bado kuchoma ubani.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
7.
Imekuzuzua gari, na vitu venye thamani,
Unapenda ufahari, kiasi ukose soni,
Hivyo vyote si sukari, hupati raha moyoni,
Namshukuru Qahari, kwa ujuzi wa shambani,
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394
Morogoro Tanzania.
1.
Ulinidharau wangu, maudhi kunitendea,
Na ule wivu mwenzangu, siwezi kukurejea,
Kutonesha donda langu, kiumbe umezoea,
Fahamu nina matungu, yote sitaelezea.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
2.
Nimezipata salamu, na barua zako pia,
Haina kazi kalamu, na wino ulo tumia,
Kusalimu si muhimu, ila sitakununia
Hujatubu nafahamu, makosa utarudia
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
3.
Sio mwezi ufahamu, ni wiki tumeachana,
Nina akili timamu, najua wataka tena,
Unaukosa utamu, wa usiku na mtana,
Umeshapata wazimu, nakwambia hutopona.
Umekuimbuka ndizi, kukupa tena sahau
4.
Utulivu si hisani, jua hauji wenyewe,
Kila mvuna tufani, pepo kapanda mwenyewe,
Tafuta mwenye imani, mie naomba nituwe,
Lala pako kitandani, rasini mwako nitowe.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
5.
Leo waniangukia, na kesho waendelea,
Mimi kulia kulia, ndio ulo yazoea,
Mja ulidhamiria, ushenzi kunitendea
Niwache nimetulia, kifo 'sije niletea.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
6.
Magoti wanipigia, kiumbe wata utani,
Acha kuyafikiria, tulofanya maishani,
Silitaki neno dia, ukome kunita hani,
Nishapata maridhia, bado kuchoma ubani.
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
7.
Imekuzuzua gari, na vitu venye thamani,
Unapenda ufahari, kiasi ukose soni,
Hivyo vyote si sukari, hupati raha moyoni,
Namshukuru Qahari, kwa ujuzi wa shambani,
Umeikumbuka ndizi, kukupa tena sahau
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394
Morogoro Tanzania.