Halima Mdee Nipepee

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,286
HALIMA MDEE NIPEPEE.


12742764_1245532452128257_513502422631009296_n.jpg


Ewe Halima Mdee, leo nataka kunena,
Simama niendelee, tuweze kumalizana,
Waonaje usogee, Njano nipate nong'ona,
Yanifukuta waona, sijiwezi nipepee

Naomba yakuelee, haya ninayo yanena,
Nyonda sinipotezee, usiku hata mchana.
Wewe ndio wa pekee, mwenzio niliye kuona,
Yanifukuta waona, sijiwezi nipepee.

Sitaki nikuchezee, lengo tupate oana,
Tupate wana tulee, kwa uwezo wa Rabana,
Mizigo wanipokee, ufurahi wao nina
Yanifukuta waona, sijiwezi nipepee

Alifu kisha ni tee, mambo yataka somana,
Nambie nitegemee, nipate poa kijana,
Hadi lini ningojee, subira yauma sana
Yanifukuta waona, sijiwezi nipepee.

Mapenzi ni ukengee, chunga tusije uana,
Pamoya tuyatetee, kwa waja wenye fitina
Wote tufike uzee, kweli sioti mtana,
Yanifukuta waona, sijiwezi nipepee.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
0622845394
 
Kweli mapenzi upofu, kamba waita mkufu
Mi hunitia kichefuchefu, kwa Doto kawa mtukufu
Mwana apenda kujisifu, kisa anaumaarufu
Wacha nitie fitna, hufai kupepewa nawe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom